Wewe unaongelea Tanga kata Ruvuma, Huko ni maporini kama mapori mengine ya Tanzania
Je, Lizaboni, Majengo, Mahenge, Makambi hakuna umeme?
Kila nchi ina vijiji hata Marekani kuna vijiji havina umeme na lami wanatumia Solar power
Ruvuma hasa hapo Songea pameendelea sana huwezi linganisha na Singida, Dodoma au Manyara
Wewe hujatembea nchi hii, Songea kuna maji ya kutosha, Huduma za afya bora na umeme wa kutosha kwa sasa, kuna kila aina ya vyakula hapo ili uwe na afya bora
Nenda Dodoma ukaone maji ni shida hakuna mfano, Kila kitu kimepelekwa Dodoma lakini bado hapabebeki
Huko kata ya Tanga ni Songea vijijini taratibu Mtakuja kupata huduma
Hata Dar es Salaam kuna mitaa kama Buguruni, Mwananyamala, Sinza na mingine mingi ni hovyo huwezi kuishi mtu smart
Ni shida kila kona hapo Dsm maji ya shida kwenye madumu, uchafu kila kona mpaka mlangoni
Songea na Mtwara ni miji imepangwa
Mtwara mitaa kama Ligula, Raha Leo au Shangani pamepangwa kuliko mkoa wa mbeya
Mbeya mitaa kama kalobe, Iwambi, Nzovwe kufika gari nyumbani kwako tu ni shida
Hiyo ni mifano kidogo tu
mkoa wa Mbeya ni hovyo yaani slam huwezi linganisha na Mtwara au Ruvuma