Ubaguzi wa kisiasa, mikoa ya Kusini ni Soweto ya Tanzania

Ubaguzi wa kisiasa, mikoa ya Kusini ni Soweto ya Tanzania

Wabaguzi wanasema eti maendeleo hayana chama wakati maneno yao yako kinyume na usemi wao wanabagua kiitikadi na kikanda

yani Jiwe alisisitiza kabisa kwenye kampeni ukichagua upinzanibsiwaleteinmendeleo
 
Vilifungwa vyote hivyo ukiacha cha ualimu cha Miaka mingi na Major Seminary Peramiho ambayo Serikali hawana uwezo wa kuifunga. Hakuna kusomea madigiriiiii tena Songea, labda open university. Lile buuum haliliwi tena Songea. Mazuri yote uliyotaja yalikuwepo kabla ya vyuo ongeza na uwingi wa upatikanaji wa MAJI kwa sasa, kongole serikali. Issue vyuo vikuuu! Au waweza tusetia vikarejeshwa wana Songea iwe rahisi kunaongeza madigiriiii mengine- masters na pihd ??
Wewe umenena sababu mtoa maada nadhani haijui songea vzr.Namshauri awe anatembea mikoani ili ajiridhishe kabla ya kutoa uzi wake.songea mzunguko wa pesa ni mkubwa ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara,kuna machimbo mengi ya madini.sekta ya afya iko vzr,mbali na serikali wakatoliki wabenediktini wamewekeza Sana,peramiho,litembo,Lituhi mission nk.huduma za maji iko vzr.Mjini songea huhitaji kuchimba vyoo vya shimo.mifumo ya maji Safi na taka yameunganishwa.Mabwawa makubwa yamejengwa kiblang'oma na sijajua Kama hata tawi la St Augustine Kama lilifungwa ila St Joseph lkn bado kuna vyuo vingi vya Kati vingi vinavyotoa taaluma mbalimbali mikoani ruvuma,Lizaboni umeme ni muda wote.Sijajua mtoa maada Kama ana ufahamu mkubwa kutoka mikoa hiyo
 
Mleta mada hebu tuambie:-
= Kutokuwepo kwa Chuo Kikuu kuna vijana wamekosa Elimu ya Chuo Kikuu? na iwapo hoja yako ni muhimu hebu tuambie mikoa ya magharibi (kigoma, tabora na katavi) kuna Chuo Kikuu?

Tunajenga kwanza Chuo cha Utumishi wa Umma Chato.
 
Uzi wa kijumla sana..yaani unataja mikoa halafu unakuja kutumia sampuli ya Kata yako..hovyoo kabisa.
 
Huo uliouandika Hapo ni ujinga mtupu na hiyo ni akili mgando.Kama wangeendekeza ngono basi karibu wote wangekuwa HIV positive.wangoni wako kila sekta nchi hii na wameshika nyazifa kubwa na Kama wangeendekeza ngono hata shule wangekuwa nyuma basi.Kwa nn ruvuma ni among the big five?
Wangoni huwa hawarudi kabisa kwao ila wako ktk nyazifa kubwa Lindi ushirikina ndyo shida aisee daah
 
Hakuna ubaguzi wowote kusini.

Kusini kucheleeee.....
 
Tukubali tu kwamba hapo nyuma taasisi zilianzisha vyuo vikuu ktk mazingira ya kujipigia fedha - Chuo hakina wakufunzi, miundombinu, laibrari, nk nk

Sasa wajibu wa Serikali ni pamoja na coordination - haviwezi kuachwa viendeshwe kiholela
 
Nimeshakwambia huko Kigoma hata hizo za msaada hakuna,Hadi leo hii tunaongea ukitaka kufika Kigoma na Katavi lazima ule tope
Wee bwana murongo kweri mchana kweupe? Unajua Daraja la Malagarasi? Unajua historia ya Suez Canal kabla ya hapo Liverpool hadi Mombasa ilibidi uzunguluke kupitia Cape Town na Mtwara? Mbunge wenu fundi kujitapa ana hela ya world bank za mimba darasani na za kujenga uwanja wa michezo na wa kulima michikikichi na kujenga University. Kwa nini usianze naye? Kikwete kawapa daraja hilo, angekuwa kama nyie lingejengwa Bagamoyo au Kimandolu.
 
Huo uliouandika Hapo ni ujinga mtupu na hiyo ni akili mgando.Kama wangeendekeza ngono basi karibu wote wangekuwa HIV positive.wangoni wako kila sekta nchi hii na wameshika nyazifa kubwa na Kama wangeendekeza ngono hata shule wangekuwa nyuma basi.Kwa nn ruvuma ni among the big five?
Kwa uliyoyaandika tu hapa yamesadifu yale Madhaifu yote kuhusu Makabila ya Kusini na hiyo Mikoa ambayo nimeyaainisha hapo mwanzoni. Pole!
 
Tukubali tu kwamba hapo nyuma taasisi zilianzisha vyuo vikuu ktk mazingira ya kujipigia fedha - Chuo hakina wakufunzi, miundombinu, laibrari, nk nk

Sasa wajibu wa Serikali ni pamoja na coordination - haviwezi kuachwa viendeshwe kiholela
Hayo mapungufu si inawezekana wakarekebisha?
 
Waache kukimbilia sehemu zingine km Dar wajenge kwao na wapunguze ujuaji.
Sijui nikutukane lakini nimekusamehe maana najua akili yako ni ya ndezi. Watu wa Lindi Mtwara hususan vijana walikimbilia Dar es Salaam na sehemu nyingine katika kutafuta maisha bora kama wafanyavyo watu wengine. Hata hivyo, wewe ndezi hujua historia ya mikoa hiyo na uonevu mkubwa uliofanywa na serikali zoote za CCM hasa tukianza na ile ya Nyerere ambaye ndiye alitandaza msingi wa uonevu dhidi ya watu wa mikoa hiyo ya kusini.

Sera ya Nyerere kwa mikoa ya kusini ilikuwa kuifanya Ngao dhidi ya mashambulizi ya nchi zilizokuwa zinadai uhuru wao za Msumbiji Zimbabwe Afrika Kusini na Angola. Nyerere hakutaka mikoa hiyo isonge mbele kimaendeleo. Akaitenga kiuchumi na kijamii. Akainyima fursa zote. Akajenga makambi ya Jeshi na kuweka vituo vya rada tu.

Akatumia uchumi wa watu wa mikoa ya kusini kunufaisha watu wengine. Kumbuka zao la Mkonge lilipoanguka miaka ya 70 zao la korosho lilichukua nafasi ya kuleta fedha za kigeni kwa nchi. Pamba ilipoporomoka korosho ilifidia. Kimsingi watu wa kusini hawakufaidika na zao la korosho kwa sababu walinyonywa vibaya sana na serikali kupitia Board ya Korosho. Ni dhahiri kwamba unyonyaji na ukandamizaji huu uliendelea na kurithishwa na watawala waliofuata labda kwa sababu ni chama kilekile.

Hakuna mtu anayekimbia kwao kwenye manufaa. Tazama leo hii vijana wengi wamerudi Mtwara na Lindi hasa katika miaka ya 2014, 2015 na 2016 ambapo korosho ilianza kuleta tija kabla ya maamuzi yaliua kabisa zao hili mwaka 2018.

Sina uhakika wewe mbulula unaandika message hii ukiwa kwenu Malampaka huko au na wewe sawa sawa tu na hao unaowaita wakimbizi wa kiuchumi. Ila cha kuzingatia katika mada hii ni Mikoa ya kusini inaonewa!!!@

Be careful kijana
 
Mikoa mingi inayopatikana kusini mwa Tanzania iko nyuma kimaendeleo.

Ruvuma, Lindi, Mtwara hii mikoa ni imetengwa na kupuuzwa kwa miaka mingi.

Nitaelezea kwa Ruvuma, mkoa wa Ruvuma makao makuu Songea hakuna chuo cha elimu ya juu hata kimoja, vilivokuepo vyote vilifungiwa na ikawa mwisho wake.

Yanayotokea huko mengine yanastaajabisha.

Kata ya Tanga manispaa ya Songea uchaguzi mkuu 2015 walichagua upinzani kwa nafasi ya udiwani.
Yule diwani alikuja kujiunga na upande wa chama kilicho madarakani kwa sasa.

Alikuwa kati ya viongozi wa kwanza kujiunga kwa kudai kuunga juhudi. hii ilisababisha tafrani kubwa kwa wakazi wa huko.

Kwa kua watu walichagua upinzani wakaambiwa sasa mtaona cha mtemakuni kimaendeleo mtatengwa adi mtapojirekebisha yani wachague wale wa chama kilicho madarakani.

Sasa kuna mtaa ambapo yule diwani anatoka umeme umewekwa kata nzima isipokua hapo tu kwenye huo mtaa wameruka lakini ilipokaribia uchaguzi mkuu 2020 wiki moja kabla walileta wafungwa kuekea nguzo wakidai wanafunga umeme hii ilikua zuga sababu adi leo hakuna huo umeme na wanaambiwa tunawakomesha, sababu walichaguaga diwani kutoka upinzani mwaka 2015 ambae nae alijiunga na ule upande wa chama kinachotawala 2017.

Kosa la hawa watu ni nini?

Hii mikoa imekosa maendeleo miaka mingi sehemu nyingi hakuna hata umeme, maji, hospitali etc. Wameleta umeme lakini nao unawekwa kwa ubaguzi hawa watu wanapandikizwa chuki kwa lazima hilo muelewe.

Yale ya Soweto miji iliopuuzwa, iliotengwa kimaendeleo sababu walikua wanaishi watu weusi kule Afrika ya kusini, yanatokea na Tanzania.

Afrika ya kusini ulikuwa ubaguzi wa rangi uliofanywa na makaburu, Tanzanaia ni ubaguzi wa kisiasa unaofanywa na watu wanaofikiri taifa hili ni mali ya chama chao.
Mkuu kuhusu vyuo vinavyotoa elimu ya juu mikoa hiyo mbona ipo.
Sema hakuna chuo kikuu ila vyuo vinavyotoa elimu ya juu vipo.
 
Yes, wanaweza ndiyo maana Serikali baada ya ukaguzi walipewa muda wa kurekebisha dosari - muda ulipopita ikalazimu hatua kuchukuliwa
 
Back
Top Bottom