Ubaguzi wa kisiasa, mikoa ya Kusini ni Soweto ya Tanzania

Daraja la Busisi kule Misungwi kuelekea nyumbani kwa Mutukufu ni la tsh 700 BILLION ,mikoa yenu yote haina mfano hata mmoja Kama huu
Kwa sasa huwezi abadan kufananisha kimaendeleo ya vitu Chatto na Songea ,Lindi wala Mtwara miji iliyokuwepo hata kabla Karl Peters hajazaliwa
Mlie tuu 'mitano tena', au nasema uongo ndugu zangu?
 
Kata ya Tanga iko manispaa, ingekuwa kijijini stand kuu ya mkoa ingekua apo Tanga?Cc Huliza
 
Makosa makubwa ya Watu wa hiyo ( hii ) Mikoa tajwa ni....

1. Kuendekeza Majungu
2. Kupenda Ushirikina
3. Ngono kutawala sana Akili zao
4. Uvivu uliokomaa
5. Kupenda Lawama na Visasi

Na katika Kukuthibitishia hili hata Ndugu zao akina Hayati Mkapa na Premier Majaliwa wamefanya na wanafanya makubwa bado Wanawadharau.
 
Inakuaje sehem waskotoka viongozi? Wao hawastahili maendeleo?

Huoni huu ni ubaguzi?
 
Halafu Lindi hawana shukrani kipindi hiki wamepata waziri mkuu lakini kuna Mila dalili kabisa unaona ni Kama hawatoi ushirikiano ni lawama,ushirikina n k
 
Mleta mada hebu tuambie:-
= Kutokuwepo kwa Chuo Kikuu kuna vijana wamekosa Elimu ya Chuo Kikuu? na iwapo hoja yako ni muhimu hebu tuambie mikoa ya magharibi (kigoma, tabora na katavi) kuna Chuo Kikuu?
Vyuo vilivyokuepo awali vilianza kuleta mafankio sababu ilisaidia hata mzunguko mkubwa wa pesa, wageni wanaokuja wanakuja na changamoto ya kimaendeleo.

Wamefungia vile vyuo vyote mkoa wote hakuna chuo hata kimoja, hii maana yake nini au imefanyika kwa malengo maalumu.
Mfano mkoa wote wa Arusha kusiwepo na chuo hata kimoja, inawezekana hii?
 
Inakuaje sehem waskotoka viongozi? Wao hawastahili maendeleo?

Huoni huu ni ubaguzi?
Akili kumkichwa bwashee.
Sio lazima viongozi,hata jamii husika wana nafasi ya kujiletea maendeleo wenyewe.
Kikubwa kwanza ni kujitambua.
Changamoto ndogondogo zinaweza kutatuliwa na watu husiki wa eneo kama wakijitambua alafu serikali itakuja tu kuunga mkono.
Mara nyingi wananchi wanaanzisha vitu vya maendeleo kama zahanati,shule,barabara,vituo vya polisi,mwisho wa siku serikali inaona na inatoa suport na jambo linakuwa.
 
Way forward! Tuendelee kulalamika au nini tufanye
 
Msidanganyike jamani! Nenda Chemba Dodoma karibu na HQ ya serikali ukaone hali ya maji na maisha ya watu!
Priorities mbovu za mipango na ukosefu wa hela ndiyo sababu kubwa! Hakuna kingine!
 
Kwanini wanatoza kodi? Kodi inafanya kazi gani? Kama hayo yote wanalazimika kufanya raia nini maana ya kuwa na uongozi
 
Kwanini wanatoza kodi? Kodi inafanya kazi gani? Kama hayo yote wanalazimika kufanya raia nini maana ya kuwa na uongozi
Basi kama ni swala la kulipa kodi,nchi nzima watu wanalipa kodi na bado kuna changamoto,kila mkoa wananchi wanamalalamiko yao sio kusini tu hata kwengineko.
Popote uendapo hapa Tanzania utakutana na changamoto wananchi wa eneo husika wanalalamika.
Akuna mkoa uliojitosheleza kwa kila jambo"mwenye hili hana lile,asie na lile ana hili"
 
Kusini maendeleo yako duni sana kulinganisha na mikoa mingine.
Angalia Mtwara wanavyolia tukianzia na korosho, Lindi, Ruvuma hii mikoa imesahaulika.

Unakumbuka sakata la gesi ya Mtwara?
Mambo yanayonesha kua huko kumebaguliwa mifano ni mingi.

Hata muda wa kujiandaa na uchaguzi niambie mikoa ambayo mgombea mmoja ambaye sasa yuko ofisi kuu hakutembelea. Naomba nitajie hiyo mikoa
 
Huko imejaa CCM tangu enzi na enzi mtakoma mpaka mpate akili
Mambo ya vyuo sio jambo la msingi ,inawezekanaje Kila sehemu serikali ijenge chuo? Vyuo vinajengwa kimkakati.

Hoja ingekuwa kama mumenyimwa maendeleo mengine sawa lakini hiyo mikoa pamoja na mambo mengine ina uhakika wa mtandao wa barabara za lami kuunganisha mkoa na mkoa

Sasa nyie mkilalama watu wa Kigoma watasemaje maana hawana barabara hata moja ya lami ya kuunganisha mkoa huo na mikoa jirani yaani toka uhuru Hadi leo hii ukienda Kigoma lazima uchezee matope
 
Pamoja na jamaa kuunga mkono juhudi lakini hakuna kilichofanyika? Hivi hii nchi swala la umeme usambazaji wa umeme tu bado tatizo?🙉🙉
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…