Kawaida umbile la mwanaume ni ushupavu, ujasiri na ukakamavu. Kwa umbile hili mwanaume akapewa jukumu la kutafuta na kurudi kuiletea familia chakula, kuisimamia na kuitunza.
Unapouliza "Ni nani mwenye haki kuliko mwingine... " swali hili ni pungufu unatakiwa kulimalizia ili ufikishe ujumbe ulio kusudiwa, sababu hapo lazima nitakuuliza "Mwenye haki kuliko mwingine kwenye nini ?"
Hapa hujasoma ibara vizuri ukaielewa, niliandika ya kuwa hakuna hora zaidi ya mwingine isipokuwa yule ambaye ni mtiifu kwa Mola wake, hata kama ni mmachame kama ni mchamungu yeye ni bora kuliko myahudi popote alipo, kwahiyo haijalishi mwanaume, au mwanamke,haikalishi ni mweupe au mweusi au mwekundu.
Majukumu ya sisi wanaume ni kumsimamia mwanamke na kuhakikisha anapata stahiki katika haki zake, mapenzi, huruma na matunzo.
Hapa inabidi uniambie, hao watu wanajuaje lipi baya na lipi zuri, na uniambie akilo inamuongoza vipi mtu katika mema na mabaya peke yake ? Hilo ulitakiwa ulifikirie kwa umakini ndiyo ujenge hii hoja.
Wema si kufanya lile linalo onekana jema kwa watu, wema ni kupatia katika lile jema unalo lifanya.
Mfano nikikuuliza wewe, unaujuaje uzuri wa kula kwa adabu au kuvaa kwa mwanamke ? Au wewe ukila unakula kwa mkono gani ?
Juzi nilikufundisha jambo moja naimani kama ungemakinika nalo, usiandika hayanilikwambia imani nazo hithibitishwa na kuna imani sahihi, ambazo zimejengeka katika elimu na ushahidi na kuna imani potofu ambazo zimejengeka katika ujinga, hawaa za nafsi na ushirikina.