Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Ubahili, silaha ya siri wanayoitumia matajiri wengi ambao walikuwa masikini

Hii ni dhana tuu. Ubahili unaweza kuwa ni sehemu ndogo sana ya sababu zinazochangia mtu kuwa tajiri.

Huwezi kuwa tajiri kwa kuwa mbahili. Huku ni kuwaponza watu.

Matokeo yake ni kutesa watu tuu. Jamaa yangu mmoja aliumwa akalazwa siku mbili tuu, naenda kumbelea akaanza kunipa wasaa nisiwe mbahili. Jamaa alikuwa anaongea kama vile anajutia kurundika hela. Ulikuwa ni woga tuu, mpaka kesho nikimkbusha tunacheka.

Huwezi ushinda umasikini kwa kuwa mbahili, ni majuto ndio huguata baadae.

Utajiri ni illusion guys. Huwezi fundishwa kuwa tajiri ukubwani. Tutakufa kwa madeni, sio kila mwenye hela ni tajiri. Na Ubahili sio utajiri.

.......................
Mkuu soma tena. Ubahili umetajwa kama moja kati ya njia kuu za kuwa Tajiri. Kwenye mada kuu, jambo la kuwekeza pia limetajwa.

Kweli ubahili sio = Utajiri lakini Ubahili unachangia kuleta utajiri. Pia ubahili unalinda utajiri.
 
Mwenyewe nimedhani hapo kwenye ubahili angeweka ubinafsi ingewa na mantiki manake mbahili ni mtu ambaye hatumii kipato chake na hivo hata kuwekeza sijui manake sinibahili lakini mbinafsi ndo anaweza kuwekeza kwa sababu chake ni chake na chako ni chake pia yaani hata kama ana bilioni lakini buku yako anaitaka pia!
Mkuu kwanza jua kutofautisha ubahili na kuwekeza. Ubahili ni jambo moja na kuwekeza ni jambo lingine. Unaweza ukawa mbahili lakini hela ukawa unaweka kwenye kibubu tu bila kuwekeza, kwahiyo kuongezeka kwake kukawa kwa taratibu sana

Lakini unaweza ukawa mbahili na ukawa unawekeza na faida huitumii ovyo, unawekeza tena na mali yako itakua mara dufu

Kimsingi ubahili unampa mtu Mtaji na Unalinda Mtaji
 
Mkuu kwenye jambo gani. Kwa mifano ya ulaya/marekani nimelenga kuonesha kwamba hata matajiri wakubwa wanaishi maisha ya chini tofauti na ukubwa wa kipato wanachopata. Na penginevwangeishi maisha extravagant life wasingekuwa hapo walipo.

Na hiyo ninayoongelea ni culture ya kutumia below your means ndio jambo la msingi. Angalia kina bill Gates wanavyovaa.

Kama huamini angalia watumishi/wafanyakazi wanavyovaa, wanavyokula, magari wanayoendesha, matumizi yao bar n.k halafu fananisha na maisha ya wafanya biashara. Kisha angalia maisha ya watumishi uzeeni walio wengi utakuja kugundua, wanaishi magumu kutokana na utamaduni walijiwekea wakati bado wanafanya kazi.

Ubahili unaleta vitu viwili vikubwa. Kwanza unasaidia kulimbikiza mali, pili unaweza kukufanya uishi maisha ya aina yoyote.
ninavyo fahamu Mark Zuckerberg anavaa nguo zinazo fanana sio sababu ya ubahili bali alisema anafanya hivyo kupunguza maamuzi yasio ya lazima kwake ie kuama asubuhi na kuwaza leo avae nini..!
na Amancio Ortega japo hula mgahawa wa ofisini kwake na kuvaa ma-jeans mara kwa mara laini jamaa ana private jet ya gharama sana...sio ya kampuni bali yake binafsi!
 
kuwa na utajili sio mpaka uwe bahili mana hata mama muuza karanga nae ni bahili utajili nikuweka mipango na mazingira yakupa faida kubwa kwenye biashara
 
kuwa na utajili sio mpaka uwe bahili mana hata mama muuza karanga nae ni bahili utajili nikuweka mipango na mazingira yakupa faida kubwa kwenye biashara
Na wewe upo sahihi. Lakini mama muuza karanga asingeweza hata kujenga kijumba chake cha kuishi kama angekuwa ponda mali kufa kwaja attitude. Ana kajumba kake sababu anajibana, na ubahili ni kujibana.
 
mada nzuri nimejifunza kitu mie inapidi niwafumbie macho wapiga mizinga
 
ninavyo fahamu Mark Zuckerberg anavaa nguo zinazo fanana sio sababu ya ubahili bali alisema anafanya hivyo kupunguza maamuzi yasio ya lazima kwake ie kuama asubuhi na kuwaza leo avae nini..!
na Amancio Ortega japo hula mgahawa wa ofisini kwake na kuvaa ma-jeans mara kwa mara laini jamaa ana private jet ya gharama sana...sio ya kampuni bali yake binafsi!
Na hiyo private jet tangu anunue ametumia mara chache sana muda mwingi anatumia ndege ya abiria. Lakini pia licha ya hivyo vitu kiujumla Ortega amekuwa akiishi maisha ya kawaida sana.

Usisahau pia, Zuckerberg pia anatumia gari ya Volkswagen, gari ya kimasikini tu
 
Heshima kwenu wakuu wangu

Kama kawaida leo nakuja tena katika jukwaa muhimu kwangu hapa JF.

Hakika kuna mambo mengi sana yanayochangia mpaka mtu kuwa na mali nyingi ama utajiri. Ukiachilia mbali matajiri waliorithi mali, waliopata utajiri kwa bahati kama michezo ya bahati nasibu na wale waliojikusanyia mali kutokana na vipaji vyao kama Sanaa na soka, matajiri wote waliobaki ambao walikuwa masikini na wakawa matajiri wana sifa kubwa ya UBAHILI.

Lakini bila kujali umepata vipi utajiri wako, kama hutakuwa mbahili, hakika utafilisika, hakika hutadumu na mali zako, hakika ipo siku watu watakucheka na kusema umefulia. Kiufupi, matajiri wote unawaona duniani ambao wamedumu kwa muda mrefu ni mabahili. Ni vyema pia ujue kwamba ubahili wa mtu kama Warren Buffet hauwezi ukafanana na ubahili kama wa yule Mkinga wa Kariakoo, wote ni ubahili ila tofauti ni mmoja anafanya ubahili kulingana na matrilioni alionayo na mwingine anafanya ubahili kulingana na mamilioni alionayo.

Naomba pia ieleweke kwamba, ninaposema tajiri natambua kwamba unatofautiana ngazi. Kuna wanaomiliki duka moja kubwa la jumla wakati anaanza maisha alianza kuuza duka la kaka yake, kisha kiosk baadae akamiliki duka kubwa namuita tajiri. Kuna yule ambaye ana estate labda Chicago naye namuita tajiri. Ana hisa timu ya Barcelona, naye ni tajiri.

Nikiri kwamba hii mada imekuja kichwani baada ya mara kwa mara watu, waume kwa wake kupenda kuniita bahili. Ki ukweli huwa nafarijika sana, sababu kwangu bahili ni kinyume cha mfujaji, kwangu bahili ni mtu anayetumia rasilimali zake kwa uangalifu, kwa akili ama mtu anayetumia mali yake baada ya kushirikisha ubongo kuamua na si moyo. Kwangu ubahili ni hatua moja muhimu kwenda kwenye utajiri. Pia ni hatua muhimu sana, kubaki na utajiri.

Ubahili ni kuishi maisha chini ya kipato chako, na si kuishi maisha sawa na kipato chako, au zaidi ya kipato chako. Ubahili ni ku save. Sijawahi kuona mtu aliyeanzia chini kwa kipato na baadae akawa tajiri halafu akose sifa ya ubahili.

Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook, huvaa t-shirt na jinsi, vazi la bei raisi kazini na katika sehemu kubwa ya maisha yake. Amancio Ortega (ana mali zenye thamani ya $ 66 Billions) huwa anakwenda mgahawani kula na wafanyakazi wake chakula cha kawaida sana. Charlie Ergen (anamiliki $14 bilioni) huwa anabeba chakula kutoka nyumbani kila siku kwenda nacho ofisini kwake (kwenye kampuni yake). Warren Buffet kila siku hutengewa na mke wake kati ya $2 na $3 kwa ajili ya chai.

Hii ni kweli hata kwa Tanzania au Africa, tunawafahamu watu wengi waliofuja mali na sasa hivi wamebaki masikini na kituko kwenye jamii zetu hususani wale waliorithi ama kupata mali kwa ghafla. Nawakubali Wachaga wengi, wapare wengi sababu hii silaha huwafikisha mbali sana kimaisha.

Ubahili sio sifa mbaya. Lakini usiwe mbahili kula, ukawa mfujaji kwa mademu, usiwe mbahili kuitunza familia yako, ukawa mfujaji kwenye mitungi. Ishi maisha ya kawaida, kipato unachopata wekeza.

HATA UWE UNAINGIZA HELA NYINGI KIASI GANI, UKIWA MTU WA KUFUJA MALI UTAKUFA MASIKINI. NA HATA UWE UNAINGIZA PESA NDOGO KIASI GANI, UKIWA BAHILI NA KUWEKEZA UTAKUWA TAJIRI ENDAPO MUNGU ATAKUPA UZIMA.
Kuna haja gani ya kuwa na mali nyingi kisha huzitumii?
 
Na hiyo private jet tangu anunue ametumia mara chache sana muda mwingi anatumia ndege ya abiria. Lakini pia licha ya hivyo vitu kiujumla Ortega amekuwa akiishi maisha ya kawaida sana.

Usisahau pia, Zuckerberg pia anatumia gari ya Volkswagen, gari ya kimasikini tu
boss gharama za kumiliki private jet hazipo kwenye matumizi tu...gharama za matunzo yake ndo shetani hasa na ndio maana kuna matajiri wengi wanakwepa kuzinunua!
na kuhusu Zuckerberg kutumia VW sio jambo la kushangaza.. ule sio ubahili hasa kwani yule jamaa ni 'geek' na geeks ndivyo walivyo. wao huwaza sana kuhusu mambo ya teknolojia na sayansi kuliko vitu vidogo kama magari.
 
Mkuu bandiko lako zur ila kumbuka life expectancy yetu mie naamin tumia kulingana na uwezo wako ila ubahili mwingine hauna faida tabu upate wwe kufaid wafaid wengine tena it wont last longer nimeona wengi
 
boss gharama za kumiliki private jet hazipo kwenye matumizi tu...gharama za matunzo yake ndo shetani hasa na ndio maana kuna matajiri wengi wanakwepa kuzinunua!
na kuhusu Zuckerberg kutumia VW sio jambo la kushangaza.. ule sio ubahili hasa kwani yule jamaa ni 'geek' na geeks ndivyo walivyo. wao huwaza sana kuhusu mambo ya teknolojia na sayansi kuliko vitu vidogo kama magari.
Mkuu unataka nikuorodheshee matajiri mabahili na namna wanavyoishi? Wapo wengi sana. Tena matajiri kama hawa Tanzania tunasema ni utajiri wa ndagu.

Kifupi matajiri wengi sana wana discipline kubwa ya matumizi ya rasilimali zao, na kuwa na discipline ndio ubahili, ndio frugality ndio thriftiness. Kama unataka nikuorodheshee matajiri na ubahili wao nitakuorodheshea hata hamsini.

Lakini pia hoja sio Zuckerberg ni bahili ama laa (japo ni bahili bila kujali vitu vinavyomsababisha aishi kibahili). Hoja ni matajiri wengi wanaishi kibahili (kuishi maisha chini ya vipato vyao).

Ndio maana tunaweza muita Bakhresa bahili kama akiwa anatembelea paso, lakini tutamuita karani wa ofisi serikalini mfujaji (sio bahili) akiwa anatembelea hiyo hiyo paso.

Kwahiyo kwa jamaa mwenye utajiri Dola milioni elfu sitini na sita ($66bilion) si ishu kwake kumiliki private jet yenye thamani ya $ 45 million, just a drop of water in the sea.

Pia kikubwa, huyu jamaa maisha mengine anayoishi ni ya kibahili sana (kawaida sana) ukilinganisha na mkwanja anaomiliki. Na mara nyingi haitumii hiyo ndege, anatumia ndege za abiria tu.

Back to the point, huwezi kutoka chini kwa kipato na kuja kuwa na mali nyingi kama si bahili. Pia, huwezi kubaki na mali zako/utajiri kama si bahili (discipline katika matumizi). Tuna mifano mingi hata hapa nchini ya watu waliofulia kwa kushindwa kuwa mabahili.
 
Embu tujikumbushe nasaha za Dalai Lama hapa chini:

“Man. Because he sacrifices his health in order to make money. Then he sacrifices money to recuperate his health. And then he is so anxious about the future that he does not enjoy the present; the result being that he does not live in the present or the future; he lives as if he is never going to die, and then dies having never really lived.”

Kimsingi hakuna maisha mengine zaidi ya haya, ishi kwa kiasi, usijibane sana wala usitumie vibaya pesa zako. Sisi wote hapa duniani tunapita njia, utaacha hizo pesa alafu wale utakao waachia watazipiga kiberiti bila ya huruma. Jenga misingi imara ya kibiashara, ili iwe sustainable, wafundishe watoto wako pesa zinatoka wapi, wataelewa na kuziheshimu. Ishi vizuri, kula vizuri, vaa vizuri, endesha gari zuri of cause hayo ndiyo malengo ya kutafuta pesa.
 
Kwa nguvu hiyo hiyo ya kuheshimu maneno ya watu wazito kama Dalai Lama, ninashauri nguvu hiyo itumike kujifunza kutoka kwa wazee wetu wastaafu ambao sasa hivi wanazalilika kutokana na kufuja mali walipokuwa wanafanya kazi.

Na wengi wao walikuwa wanasema, kama natafuta pesa ili inipe furaha kwenye maisha kwanini nisile maisha kwa pesa ninayopata.

Mwisho, nakubali kwamba hutakiwi kuwa mbahili kiasi cha kudhuru afya yako. Kula, lakini kwani lazima kila siku ule kuku tena sio nyumbani bali bar? Vaa, lakini kwani lazima kila fashion ya nguo inayotoka ununue. Pumzika, lakini kwani lazima kila likizo uende vacation Zanzibar?
 
Back
Top Bottom