Ubalozi wa China Tanzania na Barrick (Kampuni ya Twiga) zatoa misaada kwa Serikali kusaidia kupambana na Corona

Ubalozi wa China Tanzania na Barrick (Kampuni ya Twiga) zatoa misaada kwa Serikali kusaidia kupambana na Corona

Na ikumbukwe kuwa:

1. Wanatutuhumu kuwa tunatoa data zisizo sahihi za maambukizi

2. Wanataka chanjo zao wajaribie kwetu (Africa) ambapo cases ni chache zaidi.

3. Wanakimbilia kutupa misaada wakati juzi kati tu taarifa zilizagaa kuwa China kuna uhaba wa barakoa (masks).

4. Wanahimiza tuapply lockdown


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa jamaa vichwa sana yaani wanapiga vi hwani sio miguuni.

Wanamaliza kwanza wauguzi na madaktari ili ugonjwa ujishakolea tywe tunaanguka km nzige hakuna wa kutibu ....Nimejikuta nawaza ndotoni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mamayoyo1,
Misaada mingine inafedhesha sana Africa, mask 100,000 ambazo hata Bakhresa anaweza akanunua na kutawanya bure. Angalia hizo mask 100,000 na propaganda inayoendelea China kuwa inassidia Africa. Shame on Tanzania.

mwaka 1995 wajapani walirudisha dollar 2000 walizotoa Senegal kisa kutunza heshima. Tumekuwa kama jalala la nchi nyingine kujipatia sifa.

jana na leo kule Guangzhou waTanzania wamefukuzwa kwenye nyumba zao eti wanaambukiza corona huku tunapokea mask laki moja. Tanzaniaaaaaaaaaa
 
Na ikumbukwe kuwa:

1. Wanatutuhumu kuwa tunatoa data zisizo sahihi za maambukizi

2. Wanataka chanjo zao wajaribie kwetu (Africa) ambapo cases ni chache zaidi.

3. Wanakimbilia kutupa misaada wakati juzi kati tu taarifa zilizagaa kuwa China kuna uhaba wa barakoa (masks).

4. Wanahimiza tuapply lockdown


Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe afadhali umeona, na Mungu akubarik, bahati mbaya Tanzania watu wengi hawako informed, wajing, sometimes I doubt ni suala la IQ. Kwa nini waafrika wote ni wajinga na backward in thinking? To me is mind boggling! you can’t believe
 
Ubalozi wa China nchini Tanzania, umeipatia serikali msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona).

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akipokea msaada huo jana jijini Dar es Salaam, alisema utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini ambao serikali imewapa kipaumbele cha kwanza ili kuwakinga na maambukizi ya Covid-19.

“Kwa niaba ya serikali tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu na niendelee kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania, msaada huu tutaupeleka kwa watumishi wa afya, kipaumbele ni kuwakinga watumishi wa afya wasipate maambukizi,”alisema Ummy.

Ummy alisema msaada huo uliotolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona, barakoa (mask) 100,000 pamoja na vipima joto vya mkono (thermal scanner) 150.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke, alisema nchi yake na Tanzania ni marafiki kwa muda mrefu na ugonjwa huo ulipoikumba nchi yao kwa mara ya kwanza, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono dhidi ya mapambano hivyo na wenyewe wamejitoa kuisaidia kukabiliana nao.

Wang Ke alisema Serikali ya China kwa sasa imechukua hatua na kujitoa rasmi kuwa nchi itakayoisaidia Tanzania katika misaada ya dharura ya vifaa kinga kukabiliana na ugonjwa wa corona.

Katika mwendelezo wa kuisadia vifaa kinga Serikali, kwa mara nyingine tena inatarajia kupokea msaada wa vifaa tiba vya kusaidia wagonjwa kupumua (Ventilator) 500 kutoka kwa mfanyabiashara raia wa China Jack Ma.

Hadi sasa jumla ya wagonjwa waliogundulika kuwa na virusi vya corona nchini ni 24, akiwamo mmoja aliyepoteza maisha, watano wamepona na wengine 18 wanaendelea kupatiwa matibabu katika vituo maalumu vilivyopo maeneo mbalimbali nchini.
 
Kama taifa tunapaswa kuwa makini sana na misaada toka nje ili kupambana na Covid-19. So far bado kuna wingu zito kwao sijajua wamefikiaje hatua ya kutoa msaada.

Tusipo kuwa makini tunaweza kujikuta maambukizi yakiongezeka sana baada ya 'misaada' hii kuingia nchini.

Mungu awajalie hekima hawa viongozi wetu, sioni sababu ya Tz kuwa kipaumbele cha misaada wakati hali ya maambukizi ipo chini sana (kwa mujibu wa takwimu zetu) ukilinganisha na maeneo mengine huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una akili sana kifaa.
Sio msaada tu but particularly from China

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom