Ubalozi wa Marekani: Tumetiwa moyo na hakikisho la Rais Magufuli kwamba uchaguzi mkuu 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye uwazi

Ubalozi wa Marekani: Tumetiwa moyo na hakikisho la Rais Magufuli kwamba uchaguzi mkuu 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye uwazi

Na kwa kauli hiyo ya "Beberu mkuu" kumbe tume huru yaweza kuundwa muda huu kabla ya uchaguzi mkuu wa Octoba.
Kazi kwenu viongozi wote wa upinzani, kazi kwenu Wabunge na wananchi. Hapo ndio pa kukamatia na kwa kujitoa kwenu tutapata uchaguzi safi wa viongozi waliochaguliwa na wananchi wenyewe bila kujali ni wa chama gani.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hamuiwezi CCM bila mbeleko ya " msaada wa Marekani"?
Sio uongo hatuiwezi. Maana ukifurukuta hivi risasi, ukijigeuza kesi ya uhujumu, mkutano kidogo hata chumbani uchochezi!
Huku Muruto yuko na mbwa na virungu huku Mambosasa na bunduki hadi anaua wanafunzi kwenye mabasi!
Watu wafanyeje kama sio kumfuata Beberu na kumwambia mbona mbuzi "jike"wako anatumia pembe kujeruhi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza,
Aibu sana kunyooshewa kidole namna hii sisi kama taifa huru. Yale yote yaliopiganiwa enzi za harakati za ukombozi yanaelekea mwambani. Si tu kwamba juhudi za ukombozi wa fikra zinelekea kwa muflisi bali hata ule uhuru wa bendera kwishnee.

Mmarekani yuko bize kunyanganya wasiokua BASUNGU uhalali wao kupiga kura alafu anatuharishia kwenye kipeperushi yale afanyayo yeye. Shame asipoitwa Balozi wao akemewe kisawasawa. Dadeki😈
 
Back
Top Bottom