Ubalozi wa Marekani: Tumetiwa moyo na hakikisho la Rais Magufuli kwamba uchaguzi mkuu 2020 utakuwa huru, wa haki na wenye uwazi

hii statement ni TEGO, hiyo tume huru watu hata habari nayo hawana sasa inakujaje humo?
 
Chakaza,
Ah ah ah... Hawa wamarekani nadhan they are just kidding.
Hivi hawajui kuwa:-
- Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi NEC ni kada wa CCM.
- pia hawajui kuwa kuwa wasimamizi wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi ni makada wa CCM.
- Pia hawajui kuwa tayari uchaguzi wa serikali za mitaa ulinajisiwa naye kwa kutumia bunduki za polisi??
Wamarekani wajue kama hakuna tume huru ya uchaguzi hatutajitkeza kupiga kura katu
 
(1)Kama ni la kweli basi Jamaa atakuwa anajutia tamko lake lile.

(2)Kama ni kweli basi sanasana itawasaidia baadhi ya Wabunge wa upinzani waliokuwa hatihati kupoteza, Wabunge kama Sugu, Mnyika, Mdee n.k..kwa upande wa uraisi sidhani kama wana hofu kuuuuubwa.
 
Dah! Binafsi naumia kutochagua Mwenyekiti wangu wa Mtaa. Ningeweka record ya KUSHIRIKI uchaguzi kwa Mara ya kwanza lkn sasa sitarajii tena Kushiriki uchaguzi wooote wenye maamuzi yoyote ya kisiasa.

Yaani graduate Kakosea kujaza fomu halafu std 7 anapatia, halafu Mkoa mzima unatangaza CCM Imepita kwa bila kupigwa, kweli?

Kiongozi wa Mtaa tungeweza kumchagua hata kwa kukutana kwenye uwanja wa michezo na kusimama nyuma yake, tunawafahamu hawa! Halafu tunajipongeza kwa makofi meeeeengi. Mungu aendelee kutulinda maisha yaendeleeee! Lkn dhamiri zetu tunazitesa bure na kujisababishia magonjwa na hofu kwa Mungu wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania leo Ijumaa Januari 31, 2020 umempongeza Rais John Magufuli baada ya Rais Magufuli kueleza kuwa uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 utakuwa huru na wa haki.

Mbali na pongeza hizo, ubalozi huo umetaka kuharakishwa kwa uanzishwaji wa tume huru ya uchaguzi.

“Tunatoa wito wa kuharakishwa kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura lenye uwazi, kuanzishwa kwa tume huru ya uchaguzi na kuteuliwa mapema kwa waangalizi wa uchaguzi wa kitaifa na wa kimataifa wa kuaminika watakaofuatilia uchaguzi kwa kipindi kirefu na kipindi kifupi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Ubalozi huo pia umesema unatarajia kuwepo kwa uchaguzi wa amani ambao wagombea wote watakutana kwa amani wakieleza mawazo yao na kampeni zitakazofanyika katika misingi ya usawa.

Januari 21, 2020 Rais Magufuli aliwahakikishia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na wa haki, alipokuwa akizungumza nao Ikulu Dar es Salaam.
 
Mabeberu wanaakili kushinda wazalendo uchwala waliojazana ofisi za Lumumba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…