Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya usifumbie macho udhalilishaji huu dhidi ya viongozi waandamizi wa nchi yetu.

Kosoa lakini acha kutukana. Kusema Rais wa nchi amelala na mwanamke nje ya ndoa pasipo kuwa na "concrete evidence" hayo ni matusi mazito sana kwa yeye mwenyewe, familia yake pamoja na Tanzania kwa ujumla.
Kweli, hapo nakuelewa mkuu. Heshima kitu cha muhimu sana duniani. Pia ninachotambua ni kuwa yule mwanadada amesema kuwa sio kweli, picha yake imetumika vibaya pasi yake kuwa na ufahamu. Anadai, hiyo fununu aliiskia kutoka kwa rafikiye, na wala hajui hayo mambo kabisa. So ni propaganda tu za wazee wa 'behind the scenes'.
 
Communication Regulatory Authority ya Tanzania inafungia hii website soon. Iendelee kubaki huko huko Kenya na sio huku Tanzania.
 
Kwa hiyo unasifia matusi ya kwenye mitandao (Cyberbullying)? Are you serious?
Sisifii cyber bullying mkuu, tunaongelea kuhusu kusema ukweli, kama kitu ni kibaya, kinasemwa na kama ni kizuri, vivyo hivyo. Mambo ya cyber bullying sio mazuri kabisa na hiyo story ya huyo dada, ni allegations not real, so mwenye kuonewa hapo sana ni huyo dada coz hata hajui jambo lolote kuhusu tuhuma hizo!
 
Communication Regulatory Authority ya Tanzania inafungia hii website soon. Iendelee kubaki huko huko Kenya na sio huku Tanzania.
Hayo ni maamuzi yenyu, hatuwezi ingilia. Kila mtu atabeba mzigo wake, so it's up to the Tz government to do what it feels right according to your constitution.
 
Hayo ni maamuzi yenyu, hatuwezi ingilia. Kila mtu atabeba mzigo wake, so it's up to the Tz government to do what it feels right according to your constitution.
Tanzania inataka urafiki na undugu wenye manufaa kutoka Kenya, and not the other way round.
 
Tanzania inataka urafiki na undugu wenye manufaa kutoka Kenya, and not the other way round.
I get it, na nafkiri unafahamu sheria zetu zilivyo tight kuhusu media kujiachia mambo mengine, ndio maana recently unaona kuna media stations and some personalities too, wanakula ban ama suspension kwa makosa kadha wa kadha. So hatujalala kwa hayo, serikali iko na macho na maskio kila kona ya nchi.
 
Kama kweli mnafanya hivyo ni vema
 
Kibaya na kizuri kisemwe kukiwa na "concrete evidence" nje ya hapo huo ni udhalilishaji tu
Na unapaswa kujua kwamba, huu udhalilishaji ama Cyberbullying upo duniani kote, ni kitu kinasumbua serikali, ata jamii nyingi tu. Kuna watu "keyboard warriors" wanaofanya yao mafichoni, kuathiri wengine, na ni vigumu kuwapata sababu labda ni wabobezi wa maswala ya IT sana na pia huwa kawaida sio wananchi, wengine wanafanya yao nje ya nchi, ila mkimtafuta mnaona yuko ndani. Technology imekuwa complicated sana hadi inawakoroga serikali zenyewe.
 
Huo mtandao uliomdhalilisha Rais Magufuli wakija kuchapisha classified military documents Kenya itaacha kuufungia?
 
Huo mtandao uliomdhalilisha Rais Magufuli wakija kuchapisha classified military documents Kenya itaacha kuufungia?
Kwa nini tuache, kama tukiwawahi sawa, tunafunga kila kitu, lakini kama ni mfano wa wale jamaa wa Russia, my friend hata serikali za ughaibuni wanatokwa kijasho pale, sembuse serikali zetu za third world?
 
Mleta mada ni miongoni mwa wanaoeneza hiyo Ishu yenye mwonekano wa kumdhalilisha Hayati Rais wa awamu ya tano .
Kuleta humu hiyo taarifa na mpaka kipande cha hilo gazeti ni kueneza hiyo taarifa.
Baada ya kuona Rais wa nchi yangu anadhalilishwa kwenye internet (kumbuka internet imefanya dunia nzima kuwa kama kijiji) ulitaka mimi nifanyeje mkuu? Ulitaka nikae kimya? Au ulitaka nilete malalamiko yangu mbele ya umma wa watanzania bila kuweka ushahidi wa kutosha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…