Tetesi: Ubalozi wa Ufaransa wajadiliwa ndani ya Ofisi ya IGP na baadhi ya wanausalama kwamba umemficha Polepole

GWajima alikemea utekaji kesho wakaizingira kanisa, TLS imelaani wakili wao kuonewa leo wamezimgira ofisi zao.

Kama wanajua yupo hapo mbona maamuzi ya kuzingira huwa hawachelewi, kulikon katika hili. Wazingire wamtoe nje
Hiyo hawawezi ni against international laws na norms za kidiplomasia.HawaweZi wanaufyata
 
Siku si nyingi tukikombolewa! Nitakutafuta tunywe Supu ya Kende za kitimoto kwa furaha.
 
Unajua kuna muda nabaki nashangaa watu ambao wanaoshauri hivyo vyombo ni vilaza wa hali ya juu , huo upuuzi wa kusema Polepole aliuanzisha yule mbilikimo aliyekuwa anagombea kule Wanging'ombe anaitwa Enock Kiswaga .

Sasa kama watu wa jinsi ya huyo ndio think tanks wa CCM na polisi sishangai yule jamaa aliyekuja bongo akakopa kisha akatimkia ughaibuni na akawaacha kwenye mataa.

Hawa ndio vidampa wanaolamba miguu na kujipendekeza huko CCM mwisho wanapenyezwa hadi vyombo vya dola ambavyo vilitakiwa kuwa huru na kuwa na uweledi katika ufanyaji kazi wake.


View: https://x.com/TheRealEkiswaga/status/1958629502352846982?t=DpjQ_DBdGzXfNNMt10aHVg&s=19
 
Tatizo ni confirmed intel kama TL alivyokua hosted German Embassy.
Ile issue ilikuwa wazi baada ya Lissu kuona amefuatiliwa mara 2 kila aendapo na zile gari ndio alipopiga hesabu ya haraka kulinda usalama wake ni kwenda ubalozini baada ya kufanya contact balozi na halikuwa jambo la siri hata siku anaenda airport balozi alimsindikiza na kuhakikisha kapanda ndege kabisa .Hivyo kwa muktadha huo Lissu hakujificha kama ambavyo polisi wamemsaka Polepole miezi miwili sasa na wasijue alipo.

Polisi ninachoona kwa sasa imegawanyika kuna watu wamelambishwa mipesa na mafisadi na kuna wasiopenda yanayoendelea ukitaka kuamini ni hivyo ukisoma ule wito wao kwa Polepole waliandika "baada ya juhudi za muda mrefu kukutafuta kushindikana"

Maana yake walikuwa wanamsaka kimya kimya hivyo kuna waliokuwa wanawambia yupo hapa wakienda hayupo mwisho wa siku ni miezi miwili wameamua watoke tu na kusema kuwa walikuwa wanafanya juhudi kumtafuta.

Hizo juhudi kwanini hawakufanya kuwapa wito kina Mdude, Sativa na Soka ambao nao walikuwa wakosoaji mitandaoni na walijua walipokuwepo ukiachalia Mdude ambayw hadi waliahidi kutoa pesa mtu akiwaambia alipojificha katika makazi mapya na hatimaye wakafanikisha nia yao ovu na kama kawaida yao wakaja kukanusha na kusema uchunguzi unaendelea.
 

Yaani wewe kiumbe mwenye jina kama biscuts uwa nakukubali sana. Yaani hata kikao kikifanyika chooni unapekenyua na unawaweka wazi tu
 
 
Kosa la Polepole ni nini mpaka serikali inamutafuta au kaongea yale wasiyoyapenda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…