Kwanza twambie hao watano tu walioijadili nchi yetu ya kusadikika na Uchaguzi wa 28/10/2020 wamesema nini? Pili, hoja kwamba ni wabunge watano tu haina tija, kwa sababu kwenye kikao hata hoja ya mtu mmoja tu inatosha kusikilizwa na kufanyiwa kazi. Kwenye kikao siyo lazima wajumbe wote waseme kuhusu hoja fulani, maana watakuwa wanarudia rudia kile kile, labda kama kuna ubishana hapo wengi wataongea, lakini hoja ikiwa na mashiko mjumbe mmoja tu anatosha. Hivyo kama hoja kuhusu nchi yetu ya kusadikika na uchafuzi wa 28/10/2020 imesemwa na wajumbe watano, basi hao ni wengi sana! Na kama hakuna mjumbe aliyekuwa na mawazo tofauti na hao watano maana yake hiyo hoja imekubaliwa na kupokelewa na wajumbe wote, kinachofuata ni azimio tu kwenye kikao kinachofuata. Cha kufanya sasa ni Tanzania kutoa maelezo ya kina kwa kilichofanyika ili kukiwahi hicho kikao cha maamuzi kitakachofuata. Tukikaa na kuamini hiki cha huyu nyumba kumi ambaye anaonekana hajaiva kidiplomasia itakula kwetu. Tujue wazi kwamba dunia kwa sasa ina picha mbaya sana kuhusu nchi yetu na utawala wake hauna mwangwi mzuri duniani. Hivi bado hatuelewi hili?
Bahati mbaya sana ni kwamba tumempata waziri wa mambo ya nje mwenye propaganda badala ya Diplomasia. Huyu hatofautiani kabisa na Polex2. Waziri mwenyewe hana uhalali wa kuwa waziri maana ameteuliwa kinyume na katiba. Ameteuliwa kabla ya waziri mkuu, na uteuzi wa waziri mkuu unathibitishwa na kiapo ndipo mtu awe waziri mkuu na baada ya hapo katiba inamtaka akae na mkuu wa kaya waunde baraza la mawaziri. Kitu hiki hakikufanyika. Ni aibu ya mwaka. Tunakuwa na waziri wa mambo ya nje mwenye kazi ya kumpamba mfalme kwa maneno biriani na kachori. Kwa namna hii kuirudisha nchi yetu kwenye asili na utamaduni wake ni kazi nzito!