Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Ubalozi wakanusha habari za uongo zinazodai kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo

Huwezi kushinda uchaguzi/au kuongoza nchi kwa kushirikiana na KABURU. Tundu Lisu angekuwa mzalendo wa nchi hii angeunda chama chake safi kabisa ambacho hakina mahusiano na hao Makaburu. Alitakiwa kuwa na chama cha kizalendo na kuzungumza mambo muhimu kwa ukweli na kugusa shida za watu kwa ukweli kabisa watu wangemuelewa kwasababu watu ndio wenye kuhitaji maendeleo na watu ndio wapiga kura.

Ila kwa hesabu zake za ajabu za kutetea mambo ya kishenzi yaliojaa ukaburukaburu, kuweka rehani rasilimali za Taifa kwa Makaburu ili kupewa misaada yenye masharti ya ajabu ni kujidanganya yeye na roho yake.

Watanzania sio wajinga kama mnavyodhani, kuna elimu ndogo,kati na kubwa. Watanzania wengi wanajitambua na wanauwezo wa kuelewa hata pale kiongozi anapozungumza sio mpaka waende darasani.
Huyo Mr Mzungu hawezi chochote cha maana, achilia mbali kuanzisha chama cha siasa. Anachoweza tu ni kutukana, kukashifu, kuzusha, kusema uongo na kupinga kila hatua ya ustawi & maendeleo ya nchi yetu. Halafu ni mwepesi sana kulialia kama kifaranga.
 
Huyo balozi wa Ubelgiji siyo mzalendo hata kidogo. Kwanini anaendelea kulilia pesa za mabeberu? Mnadanganya wananchi eti wanalazimishiwa ushoga na mabeberu.

Halafu anasema “hatupokei msaada kila mwaka”, na hapo hapo anasema “msaada haujasitishwa”
wewe ni kenge jamii ya nyani
 
Mimi kuna mambo namSupport Jiwe na mengine simSupport.Mfano namSupport jinsi alivyoDeal na corona baada ya kujiona hana ubavu akamuachia Mungu.
SimSupport kwenye wizi wa kura na jinsi anavyominya upinzani!
 
Huyo balozi ni muongo, na Pia ni kilaza! Eti anathubutu kubeza maoni ya wabunge 5?! Tena wa kamati ya mambo ya nje? Eti kuwa siyo bunge lote, hajui kuwa bunge lote husikiliza hizo kamati? Ama anadhani ni bunge la Ndugai?
kwa wenzetu, wengi hupewa, wachache husikilizwa. hao wabunge watano hoja zao zinaweza kuwa mwiba kwetu.
 
wewe ni kenge jamii ya nyani
Mbona? Au hoja za wale wabunge watano zimekukoroga? Hebu subiri waongee wote 705 labda utarukwa na akili kabisa! Shangwe zinakwenda kukata Kama stimu ya bangi!
 
JamiiForums members and public at large dont miss out on this important meeting at the EU HQ
19 November 2020
Brusssels, Belgium

45 minutes were assigned for the EU Parliament Committee on Foreign Affairs discussion on Tanzania

Full 45 minutes of delibaration by the EU foreign affairs council , dub the most important agenda of the day, agenda number eight scrutinizing in detail what is going in Tanzania, a country that is under the leadership of John Pombe Joseph Magufuli . Focusing on geopolitics of Tanzania, security problems in the south of Tanzania, Tanzania preference towards Splendid isolation from international community, Democracy, human rights, 'one' party parliament in Dodoma, Members of Opposition MPs boycotting to be sworn-in and donor funded projects in Tanzania etc.
source : Lafit Amars
 
Nimemsikiliza Balozi Jestas Nyamanga akitolea ufafanuzi wa kile alichokiita upotoshaji kuhusu mjadala unaoendelea katika bunge la Ulaya kuhusu Tanzania.

Anadai kilichoketi ni kamati sio bunge zima. Na kwenye kamati waliozungumza ni wabunge watano tu. Hivyo anahitimisha kuwa maoni ya wabunge watano hayawezi kuhesabiwa kuwa ya bunge zima.

Kitu ambacho Balozi hajataka kusema ni kwamba mjadala wa kuhusu Tanzania ni lazima uanzie kamati. Ukitoka kwenye kamati ndipo utaenda kwenye bunge zima. Kwahiyo balozi kusema ni kamati tu imejadili, ni kama anataka kusema mjadala utaishia hapohapo kwenye kamati. Si kweli.

Taarifa ya kamati itapelekwa bungeni ili kuwa na mjadala wa bunge zima. Hata Tanzania tunafanya hivyo. Skendo zote kubwa za Richmond, EPA, Escrow etc mjadala wake ulianzia kwenye kamati na baada ya kamati ndipo bunge zima likajadili. Kwahiyo Balozi angejipa muda ili mjadala utakapohamia kwenye bunge zima asikose cha kuwaambia watu.

Balozi anadai hata kwenye kamati walioongea ni wajumbe watano tu. Na anataka kuitumia idadi hiyo kupuuza maoni ya kamati. Hii si sahihi. Kwanza kitendo cha Mwenyekiti wa kamati hiyo David McAllister kuongea, huo ndio msimamo wa kamati, hata wengine wasipoongea.

Nimkumbushe Balozi kwamba wakati wa skendo ya Richmond, Kamati teule ilikua na wajumbe 11, lakini walioongea public ni watatu tu ambao ni Stella Manyanya, Lucas Selelii na Mwenyekiti wao Harrison Mwakyembe. Je yale mapendekezo yalipuuzwa kwa sababu waliongea wajumbe watatu?

Jambo la muhimu kujiuliza ni je, tuhuma dhidi ya Tanzania ni za kweli au uzushi? Kamati imesema Uchaguzi ulivurugwa. Vyombo vya dola vilitumika kukandamiza upinzani na kukipendelea chama tawala. Baadhi ya watu waliuawa na wengine kuwekwa jela. Je tuhuma hizo ni kweli au uzushi? Hizi ndio hoja za McAllister na kamati yake. Kwahiyo Balozi ajibu hizo hoja sio kusema walioongea kwenye kamati walikua watano tu. 🤣

Halafu Balozi amekwepa kusema ukweli kwamba ni Kamati hiyohiyo iliyotaka maelezo ndani ya saa 48 kwanini Tanzania ilipokea zaidi ya TZS Bilioni 75 za kupambana na athari za corona. Kwanini Balozi hakuishauri serikali igome kutoa maelezo kwa sababu wanaotaka maelezo ni wajumbe watano tu wa kamati? Paradox.!

Wakati akijaribu kujieleza Balozi amejikuta akijikanusha mwenyewe. Amesema Tanzania hatupewi €626M kutoka EU. Halafu hapohapo akasema pesa hizo hazijazuiwa, tumekuwa tukipewa na tutaendelea kupewa kwa sababu zinasaidia miradi ya maendeleo. Sasa kama amekanusha kuwa hatupewi pesa na EU hizo zinazotusaidia kwenye miradi ya maendeleo ni za EU ipi? Liars must have a good memory.

Halafu tuache hii tabia ya kuamini kwamba kila taarifa anayoitoa kiongozi ni ya kweli. Mnakumbuka SACP Zombe alipoua wale wafanyabiashara na kusema ni majambazi, nchi nzima ilimuamini. Kama sio Kikwete kuingilia kati na kuunda kamati, tungeendelea kuamini waliouawa ni majambazi.

Mmesahau kuwa ndege yetu ilipozuiwa Afrika kusini, Bwana Kabudi alijitokeza na kukanusha vikali. Akasema ndege haijazuiwa na wanaoeneza taarifa hiyo ni waongo na wazushi? What happened later?

Tusubiri kamati ya mambo ya nje ya EU imalize vikao vyake ipeleke mapendekezo kwenye bunge zima. Lakini tuache kuhusisha nchi yetu tukufu na "uhuni" wa viongozi wachache. Tanzania yetu ni kubwa kuliko viongozi. Hawa viongozi watapita lakini Tanzania itadumu. Kiongozi akiamua kufanya uhuni, tunapaswa tumlaumu yeye, si kulaumu wanaotaka kutuwekea vikwazo kwa sababu ya uhuni wa viongozi wetu.

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema "Mpumbavu hutizama alipoangukia na kulaumu bali mwerevu huchunguza alipojikwaa na kujisahihisha" Tuangalie tumejikwaa wapi. Kuwatukana mabeberu ni kutizama tulipoangukia. Tuangalie kilichofanya hao mabeberu wakatugeukia ghafla. Mimba haifichwi kwa kuvaa nguo kubwa.!
Wewe ndiye unajichanganya. Kuanzia mwanzo ukisoma ajenda za kikao kile ilikuwa ni kikao tu cha kubadilishana mawazo na siyo kikao cha maamuzi. Balozi amewakomesha wazandiki na watengenezaji wa uongo.
 
Wazungu tunawategemea ila kutwa kuwasimanga kwa kuwaita mabeberu! Kuweni na shukurani na sio kuleta kejeli na dharau huku watu wenyewe sisi ni tegemezi.

Kwa jinsi tunavyowakejeli, wazungu hawa wangekuwa na mavichwa kama yetu, hata hiyo misaada na mikopo wangeshaisitisha, ila wamegundua baadhi ya watu wetu ni wajinga na wameamua kuwapuuza ili kusaidia masikini wa hii nchi wasio na hatia.

Isitoshe kwa hapa JF, uzi uliopo unaongelea kamati na si Bunge zima.

Alafu elezeni pia mlikopeleka hela za Covid.

Sisi tunasubiri taarifa rasimi ya hilo Bunge ila mpaka sasa teyari ni aibu tosha kwani hatukwahi kuwa na status mbovu na mbaya kiasi hiki.

Awamu hii ni shida tupu!

No wonder hata JK aliwahi sema watu waache "kujimwambafai."
Una akili za kutumwa tumwa tu. Mbowe kawafanya mazezeta.
 
Huyo Mr Mzungu hawezi chochote cha maana, achilia mbali kuanzisha chama cha siasa. Anachoweza tu ni kutukana, kukashifu, kuzusha, kusema uongo na kupinga kila hatua ya ustawi & maendeleo ya nchi yetu. Halafu ni mwepesi sana kulialia kama kifaranga.
Tundu Lisu na wafuasi wake ni vituko ndani ya nchi mpaka nje ya nchi.
 
Acha uongo we jamaa...

Tuwekee chanzo cha hi taarifa yako.
Msome uzuri Abiy tangu akiwa jasusi wa kijeshi hadi kuishi na kufanya kazi Rwanda mpaka kuaminika na mabeberu kucheza michezo yao michafu.

Halafu, mimi pia usinisome juujuu na kwa wasiwasi.

Nisome uzuri khasa.
 
Ubalozi wa Tanzani Ubelgiji umekanusha habari za uongo zinazoenezwa mitandaoni kuwa Bunge la Umoja wa Ulaya limeazimia kuifutia Tanzania misaada na kuiwekea vikwazo.

Ubalozi umeeleza kuwa ni wabunge watano tu kati ya wabunge 71 wa Kamati ya Mambo ya Nje ndiyo walitoa mawazo yao na hakuna azimio lolote lililowekwa dhidi ya Tanzania na Kamati hiyo. Imeelezwa kuwa Mbunge yeyote anaweza kutoa mawazo yake binafsi na na siyo kila wazo binafsi la Mbunge ni azimio la Bunge.

Bunge lote la Ulaya lina wabunge 705 na waliotoa mawazo yao binafsi walikuwa ni wabunge watano (5) tu. S
Sikiliza clip hii

Zaidi soma:


Yaani sikutegemea kama tunaweza kuwa waoga kiasi hiki sasa kwanini tulichakachua uchaguzi kama tunaogopa hivi... Ukimsikiliza huyu Muwakilishi wetu utaona anajikanganya mwenyewe kwanza anadai eti ni wabunge watano (5) kati ya 71 waliochangia kuhusu hayo mambo ya aibu tuliyoionyesha dunia .Hivi kwani pale mjengoni Dodoma kabla ya Wabunge wa CCM hawajapitisha jambo lao kwani huwa ni wabunge wangapi wanachangia zaidi ya Msukuma,Kibajaji, Mkamia, Nape na Hamis. arafu baadae hoja ikapitishwa na wabunge wengine zaidi ya 300 kwa kishindo?. Pili kumbuka katika kamati ya bunge la EU aliyetoa tamko hilo ni (Ndugai) wa Kamati yao (Mwenyekiti)kwa hiyo uzito wa tamko lake ni kubwa saana.
 
Yaani sikutegemea kama tunaweza kuwa waoga kiasi hiki sasa kwanini tulichakachua uchaguzi kama tunaogopa hivi... Ukimsikiliza huyu Muwakilishi wetu utaona anajikanganya mwenyewe kwanza anadai eti ni wabunge watano (5) kati ya 71 waliochangia kuhusu hayo mambo ya aibu tuliyoionyesha dunia .Hivi kwani pale mjengoni Dodoma kabla ya Wabunge wa CCM hawajapitisha jambo lao kwani huwa ni wabunge wangapi wanachangia zaidi ya Msukuma,Kibajaji, Mkamia, Nape na Hamis. arafu baadae hoja ikapitishwa na wabunge wengine zaidi ya 300 kwa kishindo?. Pili kumbuka katika kamati ya bunge la EU aliyetoa tamko hilo ni (Ndugai) wa Kamati yao (Mwenyekiti)kwa hiyo uzito wa tamko lake ni kubwa saana.
Wabunge wengine "see-tea-knee" na kitu waliobaki wameipiga chini hiyo kitu yenu. Msilazimishe.
 
Sasa mmeshindwa nini kupeleka waandishi huko majuu wakaripoti nyie si matajiri ?

Pili wasema ulaya unemployment rate iko juu sababu ya covid je unafikiri hata kama waso na ajira ni wengi utaweza kulinganisha na bongo!? Ulaya matatizo yapo ila hayawezi kufikia matatizo ya bongo

Ndio uone hata hiyo misaada ya chakula na food banks wenzetu wanazo je bongo wapi mnatoa walau chakula bure wakati tunasikia mabillioni yanachotwa na watu wanadunda mtaani tu kama kawaida ! Huku masikini akibaki masikini na tajiri akiendelea kuwa tajiri
Tanzania hakuna shida ya chakula labda kama mtu ahitaji kwashakoo mwenyewe.

Wazungu wana hiyo kitu kwa sababu ya mazingira ya kuwa na tamaduni ya choyo na ubaguzi.

Kwa asili, wazungu hawatupendi sisi waafrika na nashangaa sana watu hapa wanapowasogelea karibu kabisa kwenye eneo la tukio hawa wazungu na kujipendekeza huku na huko.

Wanachofanya ni kutafuta watu wao maalum wa kuwatumia kama Tundu Lissu na wengine ili kutaka kutimiza malengo yao ya kuendelea kuturudisha nyuma.

Ipo video itafute youtube yaelezea jinsi wazungu wanavyojadili kwamba Afrika ni lazima iendelee kuwa nyuma kimaendeleo ili kuendelea kulifaidisha bara ya Ulaya.

Itafute hiyo video uitazame, ukipata muda.
 
Wabunge wengine "see-tea-knee" na kitu waliobaki wameipiga chini hiyo kitu yenu. Msilazimishe.
Kitu ya akina nani kama siyo yenu ...kwani si wanawazungumzia nyie kwa uchafuzi mloufanya October 28. Hii imeshaweka rekodi dunia nzima na haitokaa ifutike wezi nyie
 
Kitu ya akina nani kama siyo yenu ...kwani si wanawazungumzia nyie kwa uchafuzi mloufanya October 28. Hii imeshaweka rekodi dunia nzima na haitokaa ifutike wezi nyie
Wezi ni akina Mr Mzungu ambao si wazalendo hata kidogo, wanataka kuchuuza na kugawa rasilimali za Watanzania kwa mabeberu wao. Hii sijawahi kuona popote. Historia itamkumbuka vibaya sana huyo kibaraka na kuwadai wa Bob.
 
Wazungu tunawategemea ila kutwa kuwasimanga kwa kuwaita mabeberu! Kuweni na shukurani na sio kuleta kejeli na dharau huku watu wenyewe sisi ni tegemezi.

Kwa jinsi tunavyowakejeli, wazungu hawa wangekuwa na mavichwa kama yetu, hata hiyo misaada na mikopo wangeshaisitisha, ila wamegundua baadhi ya watu wetu ni wajinga na wameamua kuwapuuza ili kusaidia masikini wa hii nchi wasio na hatia.

Isitoshe kwa hapa JF, uzi uliopo unaongelea kamati na si Bunge zima.

Alafu elezeni pia mlikopeleka hela za Covid.

Sisi tunasubiri taarifa rasimi ya hilo Bunge ila mpaka sasa teyari ni aibu tosha kwani hatukwahi kuwa na status mbovu na mbaya kiasi hiki.

Awamu hii ni shida tupu!

No wonder hata JK aliwahi sema watu waache "kujimwambafai."
Narudia tena na tena, badala ya ndoto yenu ya viongozi wa Serikali ya CCM na Vyombo vyake ati kupekekwa ICC, ndoto hizo zitakuwa kweli kwa CHADEMA kutoweka kwenye siasa nchini. Kwani kama kesi ICC itafunguliwa, basi mjue wazi kuwa viongozi wa CHADEMA ndio watakuwa washitakiwa kwa mauaji na utekaji unaondelea nchini. Mbowe anajua hilo na viongozi wenzake pia wanawajua washirika.
 
Back
Top Bottom