Ubaya wa kuwa na dhana mbaya kwa Binadamu wenzako

Ubaya wa kuwa na dhana mbaya kwa Binadamu wenzako

Hakika katika kumtaka Allah pasina kutoa sauti inajuzu Sana na ni Jambo linalo pendeza zaidi.

Tuangalie dalili ifuatayo kutoka katika Qur'an

Allah (Subhanahu wataala) anasema kumwambia Mtume wake (swallallahu Alaih Wasallam) : "Na mtaje Mola wako Moyoni mwako Kwa unyenyekevu na khofu Bila kupiga makelele katika kauli ( na mtaje Mola wako) asubuhi na jioni!na wala usiwe miongoni mwa wenye kughafilika."
[Al Aaraf : 205]
Allaha akuhifadhi kaka, wallah nafaidika na elimu
 
Allah akuhifadhi, msichoke tu maswali yangu kwan badi napambana nami kuipata elimu
Naam nashukuru kwa kuniita hapa, ama kuhusu dhana ni bora kujiepusha nayo kabisa kwasababu nyingi katika dhana ni wasiwasi kutoka kwa shetani na ni uchochezi wake, ila sisi umma wa mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yake tumesamehewa muda wa kuwa hatujatamka ni kitu kimepita tu katika fikra.

Kuhusu adhkaar hili jambo pana muongozo kutoka kwa mola wetu mtukufu allah tabaaraka wa ta'alaa hivyo nitakunukulia hapa chini maneno yake na uyaingize katika utekelezaji kwa kujengea msingi swali lako.

Anasema allah tabaaraka wa ta'alaa
"Na mtaje mola wako katika nafsi yako kwa unyenyekevu na khofu, na bila ya kupiga kelele kwa kauli {mtaje} asubuhi na jioni, wala usiwe miongoni wa walioghafilika."
7:205

Hivyo utakachofanya ni kuchezesha midomo kwa unyenyekevu kwa sauti ya kunong'ona pasi na kuinyanyua au kuificha sana kwani allah si kiziwi wala hayuko mbali bali yuko karibu mno na ni msikivu mwenye kujua.

Hivyo wanawachuoni wakagawanya daraja za adhkaar kwa moyo, ulimi na moyo pamoja na ulimi basi hii ya mwisho ndio namna bora zaidi pale utakapomtaja mola wako kwa sauti ya chini kwa ulimi wako kisha ukahudhurisha moyo kwa tafakuri na mazingatio.

Wallahu a'alam.
 
Nurain Ni jina alilopewa Saidna Othman (radhiaLLAHU Anhu )kutokana na kupata watoto wawili ,,Hassan na Husein ndio akamuita Nuru mbili (Nurain) I stand to be corrected. Allah a'alam
Hassan na husein ni watoto wa Ali bin abi twalibu na fatma bint rasul llah ,Othaman ameitwa dhu nurain nikutokana na kuwaowa bint wawili wa mtume kwa nyakati tofauti
 
Hassan na husein ni watoto wa Ali bin abi twalibu na fatma bint rasul llah ,Othaman ameitwa dhu nurain nikutokana na kuwaowa bint wawili wa mtume kwa nyakati tofauti
Nje ya mada ndugu naomba unikumbushe kisa Cha Ummu Salama (radhiaLLAHU Anhu) baada ya kufiwa na mumeo na jinsi alivyokuja kuolewa na mtume....@Nyoka ..mzee
 
Back
Top Bottom