Ubeberu wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar ni wa kiwango kisichostahamilika

Ubeberu wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar ni wa kiwango kisichostahamilika

ZebraPlus

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
635
Reaction score
330
Wakati Tanganyika inafanya figisufigisu ya kile ambacho kwa sasa tunakiita muungano, Nchi ya Tanganyika na Zanzibar zote zilikuwa huru na kila moja na mamlaka yake kamili ndani ya mipaka yake.

Muda mfupi tu baada ya Muungano taratibu tanganyika ikajiona sasa ni Baba mwenye nyumba kuanza kuweka sheria zilizoikandamiza na kuidumaza Zanziba katika kila hali na katika kila nyanja.

Balaa kubwa zaidi lilotengenezwa na Tanganyika ni kuunganisha vyama vya siasa, TANU na ASP. Hapa ndio wazanzibari walipowekewa goti la shingo sawa na George Floyd kule US. Kwa hakika Tanganyika kupitia njia hii imejifanya kuwa yeye ndie BABA wa Zanzibar na Wazanzibari.

wazanzibari hawawezi tena kubreath. Hawana tena Haki ya kuamua nn wanataka bila ya BABA lao kuamua.
Tanganyika ambayo ni nchi sawa na zanzibar imejipa mamlaka na uwezo wa kuamua nani awaongeze wazanzibari.

Wazanzibari MaCCM amkeni kutoka usingizini mrejeshe heshima ya nchi yenu Watanganyika wanaimaliza!
 
Nafikiri wewe ni kitukuu cha historia, fungamano la nchi na nchi ni kubwa sana kwako kwa hivyo usijichoshe badala yake jifunze mafungamano madogo madogo kama ya mtu mke na mtu mume ambao wameamua kuishi kinyumba basi. Suala la Muungano walishamaliza Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume, vitukuu mnapaswa kuuenzi tu!
 
Tumefunga ndoa ya mkeka na Zanzibar.
Acha tuwatawale kwa mahaba kama mume anamtawala mkewe.
 
Hujui historia.
Inabidi urudishe ujira uliolipwa na beberu wako
 
Yaonekana wewe bado “HISBU” kwa hiyo sahau yale ya Sultan kwani sasa ni mapinduzi daima!! ASP mpya(CCM) mbele kwa mbele!
 
Hakuna nchi inayoitwa Tanganyika , kutaja nchi iliyokufa na kuoza ni utovu wa nidhamu, Zanzibar ni nchi kamili ni suala la muda tu watu wataheshimiana
 
Hakuna nchi inayoitwa Tanganyika , kutaja nchi iliyokufa na kuoza ni utovu wa nidhamu, Zanzibar ni nchi kamili ni suala la muda tu watu wataheshimiana
We ni Mtanganyika wa ajabu kweli.
 
Nafikiri wewe ni kitukuu cha historia, fungamano la nchi na nchi ni kubwa sana kwako kwa hivyo usijichoshe badala yake jifunze mafungamano madogo madogo kama ya mtu mke na mtu mume ambao wameamua kuishi kinyumba basi. Suala la Muungano walishamaliza Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume, vitukuu mnapaswa kuuenzi tu!
Vitukuu mazuzu.
Muungano ni useless kwa pande zote mbili
 
Zanzibari msikubali kutawaliwa na tanganyika,haiwezekani mchaguliwe raisi na watanganyika ,msikubali
 
Mkata kwao ni mtumwa.

Kwanini watu mnaliogopa sana jina la Tanganyika,
Ni ujinga kukataa Tanzania bara isiitwe Tanganyika.
Hapo ndipo ile katiba (rasimu) ya Mwananchi inapotakiwa...
Serikali tatu ndio ufumbuzi na kuaminiana kutaanzia hapo...
Vinginevyo tunafuga bomu ambalo halitatuacha salama
 
Taja faida za muungano hasa kiuchumi, usikwepe swali hili.
Uzalendo ni kuweka maslahi ya Taifa mbele hasa kiuchumi

Maslahi ya Taifa kiuchumi pekee, na hata hivyo dhana ya ‘kiuchumi’ ni pana.
 
Vitukuu mazuzu.
Muungano ni useless kwa pande zote mbili
Its too late leo kudai kwanini babu yako alimrubuni na kumuoa bibi yako ilihali wewe tayari ni mwanafamilia wa unayemlaumu.. Huwezi kuvunja ndoa uzeeni, whether ni use less au use more ila ndo basi tena... na Technic aliyoitumia mzee jiwe basi amekua Genius kuzidi mwalimu so Muungano mbele kwa mbele, asiyeridhika atafute nchi nyingine ahamie huko!
 
Back
Top Bottom