Valuhwanoswela
JF-Expert Member
- Jun 27, 2019
- 1,228
- 1,127
Ka
Kama Tanganyika ilikufa Zanzibar nayo ilikuwa ife Tanzania izaliwe kama kweli hizo zilikuwa nchi mbili huru vinginevyo nchi bado ni mbili yaani Zanzibar na Tanganyika iliyobadili jina na kuitwa Tanzania for convenience tu. Zimbabwe ilikuwa Rhodesia na Zambia pia ilikuwa Rhodesia. Senegal na Gambia ziliungana na kuitwa Senegambia lakina walipopeana talaka wakarudia majina ya awali hadi leo. Tanzania tukipeana talaka wa bara tutaitwaje kama Tanganyika ilikufa na kuzikwa miaka karibu 60 iliyopita?Hakuna nchi inayoitwa Tanganyika , kutaja nchi iliyokufa na kuoza ni utovu wa nidhamu, Zanzibar ni nchi kamili ni suala la muda tu watu wataheshimiana