Ubeberu wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar ni wa kiwango kisichostahamilika

Ubeberu wa Tanganyika dhidi ya Zanzibar ni wa kiwango kisichostahamilika

Wakati Tanganyika inafanya figisufigisu ya kile ambacho kwa sasa tunakiita muungano, Nchi ya Tanganyika na Zanzibar zote zilikuwa huru na kila moja na mamlaka yake kamili ndani ya mipaka yake.

Muda mfupi tu baada ya Muungano taratibu tanganyika ikajiona sasa ni Baba mwenye nyumba kuanza kuweka sheria zilizoikandamiza na kuidumaza Zanziba katika kila hali na katika kila nyanja.

Balaa kubwa zaidi lilotengenezwa na Tanganyika ni kuunganisha vyama vya siasa, TANU na ASP. Hapa ndio wazanzibari walipowekewa goti la shingo sawa na George Floyd kule US. Kwa hakika Tanganyika kupitia njia hii imejifanya kuwa yeye ndie BABA wa Zanzibar na Wazanzibari.

wazanzibari hawawezi tena kubreath. Hawana tena Haki ya kuamua nn wanataka bila ya BABA lao kuamua.
Tanganyika ambayo ni nchi sawa na zanzibar imejipa mamlaka na uwezo wa kuamua nani awaongeze wazanzibari.

Wazanzibari MaCCM amkeni kutoka usingizini mrejeshe heshima ya nchi yenu Watanganyika wanaimaliza!
Muungano Uvunjwe tu hauna manufaa yeyote kwa wazanzibar!! Ma CCM bara yanafaidika sana na uwepo wa muungano!!
 
KWA HIYO RAIS WA ZANZIBAR NI RAIS HADI MBEYA? MBEYA WAPO HADI WATU WA MALAWI NA ZAMBIA. ULIWAHI KUONA WAMALAWI NA WAZAMBIA WANAMCHAGUA MGOMBEA WA URAIS TANZANIA? RAIS WA ZANZIBAR MIPAKA YAKE NI ZANZIBAR TU, ENEO LAKE LA UTAWALA HALIVUKI BAHARI. SASA INAKUWAJE WATU WA NGÁMBO YA BAHARI WAWACHAGULIE MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR? KWANZA HUKU TANGANYIKA HATA KURA HATUMPIGII MGOMBEA WA ZANZIBAR. SASA INAKUWAJE TUWACHAGULIE MGOMBEA?
Unapajua vikindu?
 
Zanzibar na Tanganyika zilishaungana na kuzaliwa hayo mengine ni mbwembwe tu!
Faida ya muungano niionayo mimi ni umoja wa kitaifa unaomnyima raha vijukuu vya sultan. Bila kuwa na Zanzibar tulivu, Tanzania yatatukuta kama yanayomkuta kenya tokea Somalia
 
Zanzibar ipo adi Rais wanae , nakuuliza kipi kinaitambulisha Tanganyika ?
 
Zanzibar ipo adi Rais wanae , nakuuliza kipi kinaitambulisha Tanganyika ?
Wewe unaitaka Tanganyika wakati tulishaizika??
Hakuna nchi inaitwa Tanganyika kwa sasa, unataka ipate utambulisho upi??
 
Nchi zilizoungana ni Tanganyika na Zanzibar, mpaka leo Zanzibar ipo ebu tuonyeshe kipi kinaitambulisha Tanganyika ?
Kwa mfano huo inadhihirisha zenj inaitawala Tanganyika?!
Tulikubaliana Tuue mama zetu! mama yako Tanganyika ukamuua ila mama yangu zenj nikamficha sikumuua!
Ulipo gundua mama yangu zenj sikumuua ila nimemficha!
Ukaja na wazo kuwa na ww umuue mama yako zenj ima nimfufue mama yangu Tanganyika!
Likaja jibu la kibabe kwamba mama yangu zenj simuui!, na mama yako kafa, si ruksa kumfufua😲
😭😭😭
 
Huu ndio ukweli ambao sisi Wa huku Bara tumekataa kuukubali , Muungano haupaswi kuzika nchi yako kama ilivyozikwa Tanganyika
 
Sisi upinzani huku Zanzibar kampeni yetu nikuwatetea mashehe wetu waliowekwa ndani huu ni mwaka 8
 
Mkata kwao ni mtumwa.

Kwanini watu mnaliogopa sana jina la Tanganyika,
Ni ujinga kukataa Tanzania bara isiitwe Tanganyika.
It was Tanganyika, it's still Tanganyika and it will go on being Tanganyika no matter how many people continue to be in denial of this fact.
 
Nafikiri wewe ni kitukuu cha historia, fungamano la nchi na nchi ni kubwa sana kwako kwa hivyo usijichoshe badala yake jifunze mafungamano madogo madogo kama ya mtu mke na mtu mume ambao wameamua kuishi kinyumba basi. Suala la Muungano walishamaliza Mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume, vitukuu mnapaswa kuuenzi tu!
Wamemaliza kwani nchi zinamilikiwa na hao ?
 
Hao kila siku nawaambia mbaya wao huko zanzibar ni CCM lakini hawasikii.
Kabla ya kuomba zanzibar HURU . WAITOE KWANZA CCM

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
CCM haina ubaya!
Ujue nguvu ya mtu hailiwi! Kama utaila vumilia kuliwa 😀😀😀
Hebu rejea nchi ndogo kama zenj ina wabunge wangapi ndani ya Bunge la Muungano, na inao wangapi bunge la zanziba?! Mna haki ya kuwa hata wajumbe wa nyumba kumi bara+udiwani, ubunge,....wakati wabara hawana hiyo Haki!
Hao ndio mti ulio ingia kwenye shoka 👍 acha msitu uishe 😭😭😭
 
Back
Top Bottom