Episode 4.
Ni kwamba Oleg aliambiwa akiwa anahitaji kuokolewa anatakiwa atume ujumbe kwa kwenda kwenye duka la mikate la Kutuvozsky lililopo opposite na ofisi ya siri ya MI6 jijini Moscow kila jumanne saa 1 asubuhi.
Akifika pale anatakiwa asimame akiwa amevaa kofia ya kijivu na trouser ya kijivu (rangi hii ilichaguliwa kwa kuwa haiinekani kwa uraisi kwenye majira ya muda mrefu ya barafu ya Moscow) Akaambiwa anatakiwa awe amebeba mfuko wa “rambo” ulioandikwa neno “safeway”. Mifuko iliyoandikwa hivi ilikuwa ni kutoka supermarkets za safeway jijini london. Akifanya haya yote,
hii ingekuwa ni ishara tosha kuwa anahitaji kuokolewa kutoka mikono ya KGB Pia akapewa ishara ambazo nazo zingeonyesha kuwa maafisa wa MI6 wamesoma ishara yake.
Ni kwamba saa 1 na nusu angepita pale afisa wa MI6 akiwa amevaa skirt au trouser ya kijivu naye akienda kwenye duka la mikate.
Afisa huyu angempita oleg akiwa amebeba mfuko kutoka kampuni ya Harrods Luxury pia ya Uingeleza uku akimtizama Oleg machoni .
akitumbukiza mdomoni chocolate kutoka kampuni ya Mars au KitKat za Uingeleza Baada ya ishara hizi ilitakiwa baada ya siku tatu majira ya mchana Oleg alitakiwa apande treni hadi katika mji wa Leningrad makao makuu ya wilaya ya vyborg.
akifika pale apande basi ashukie kwenye kibao kinachosoma Kilometer 285 kufika moscow. Akifika hapo ajue hapo ndio RV yaani sehemu ya makutano hivyo atafute sehemu karibu ajifiche.
Akiona gari imefika maeneo yale ikasimama na kufungua buti basi ajue ndio imemfata kumuokoa akapande kwenye buti. Mpango huu ukifanya kwa mahesabu makali sana ya timing kwani maafisa wa MI6 walijua kulikuwa na sheria kwa urusi maafisa ubalozi wakitaka kuvuka
Mipaka waombe kwanza kibali siku mbili kabla na magari yao yafungwe namba za kibalozi.
Walijua mchakato huu wote ungetumia siku mbili, hivyo Oleg akitoa Ishara Jumanne mpaka Ijumaa ndio wangekuwa tayari kwa safari. Kwa hiyo Oleg angefika RV siku ya Jumapili jioni na wao wangefika RV usiku baadae na kumchukua.
Hivyo siku ya Ijumaa tarehe 19 July 1985 Oleg alijifanya anafanya Jogging na kuwatoroka maafisa wa KGB waliokuwa wanamfatilia kisha akapanda treni na kutokomea kama mpango ulivyochorwa.
VYBORG ,RUSSIA Kwenye Buti iliyofungwa vizuri ya gari ya Saloon aina ya Ford Sierra kuna mwanaume wa miaka 46. Kwa kweli kwenye buti hii kuna joto kali sana hali inayomfanya mwanaume huyu avue Jacket alilovaa. Lakini bado joto ni kali sana. Unahisi labda mtu huyu ni mateka? La hasha, Ingawa naamini ulianza kuamini hivyo!
Mtu huyu alifanikiwa kufika hapa kwa usafiri wa treni baada ya kuwatoroka watesi wake jijini Moscow.
Alipofika hapa VYBORG, mtu uyu alichagua mwenyewe kufungiwa ndani ya buti hii Lakini nikushangaze tena? Unaweza kuamini kuwa ingawa mtu huyu ndiye aliyeamua mwenyewe kufungiwa kwenye buti hii, hakuwa ameonana kabisa na waliokuwa wanaendesha gari hii? Wala waliokuwa kwenye gari nyingine inayowasindikiza.
Hii inawezekana vipi Ati..? Kaa kwa kutulia! Mazingira ya aina hii yalikuwa yameshapigiwa mahesabu miaka michache nyuma.
Nipo hapa kukudadavulia Operation yenye code name “Pimlico” Ndio! Hakuwa ameonana nao lakini watu hawa ndio walikuwa wawakilishi wake pekee wa tumaini lake la kukikimbia kifo. Mbele ya kila gari alikaa afisa mmoja wa ubalozi wa Uingeleza jijini Moscow huku kila mmoja akiwa amempakia mwanamke anayezuga kama mkewe.
Watu hawa wangeshindwa kufanya kazi Yao,mtu aliye kweye buti angerudishwa katika chumba cha giza katikati kabisa ya Makao makuu ofisi za mwajiri wake(KGB) ambako angehojiwa kwa mateso na kuuwawa kwa risasi. Salama ya mtu huyu ni kufika katika mpaka wa Finland na Russia umbali wa maili 24 tu kutoka alipo lakini msafara huu wa magari mawili unapaswa kwanza kuvuka kuvuka vizuizi vitano vyenye walinzi Makini wa Serikali ya Urusi. Katika kizuizi cha kwanza jamaa ndani ya buti analazimika kujifunika kwa space blanket Hili ni blanket la rangi ya fedha ambalo hutumiwa na wanajimu kwa kuwa alipitishi miale ya aina yotote.
Mfano ni huu wa Picha.
Huyu jamaa alishajiandaa kwa kubeba jacket hili kwani alikuwa anaujua mfumo wa ulinzi wa vizuizini ambao ulikuwa na camera zinazoweza kung’amua joto la binadamu.
Kwa kujifunika blanketi hili ndio ikawa pona yake hivyo wakafanikiwa kuvuka kizuizi hiki. Mbele kidogo walisimama baada ya engine ya gari kupata mushkheli, lakini tatizo linatatuliwa na wanasonga mbele. Wakavuka vizuizi vingine viwili na kubakiza viwili.
Katika vizuizi hivi maafisa hawa walitakiwa kushuka na kwenda mwenye majengo ya pale vizuini huku wakiwaacha wake zao kwenye magari. Mtu wa kwenye buti hakuweza kuyaona majengo hayo lakini alikuwa na taswira kichwani jinsi yanavyofanana.
Kuwa hayakukosa waya za seng’enge, Yakiwa na minara mirefu yenye walinzi wenye siraha Wakavuka kizuizi cha kwanza. Tabu ikawa kwenye kizuizi cha mwisho Kama kawaida maafisa wale walitakiwa kushuka kwenye kizuizi cha mwisho huku wakiwaacha wake zao kwenye magari.
Huku nyuma kwenye magari yale wakaachiwa mbwa wa kunusa (Sniffer dogs) aina ya Atlas waanze kunusa magari yale. Hatari kubwa ingewakabili endapo mbwa wale wangebaini uwepo wa mtu ndani ya buti ya gari. Mwanamke aliyekuwa kwenye gari yenye mtu kwenye buti akafanya kitendo kimoja cha ujasili sana.
Ni kwamba alishuka kwenye gari na kwenda kumuweka mtoto wake mchanga juu ya buti ya gari ile kisha akamvua nepi na kuitupa chini akijifanya anambadilishia nepi. Mbwa wakapumbazwa na kuanza kuinusa nepi iliyotupwa.
Mwanamke yule akambadilishia mtoto nepi huku akiomba wasizidi kukaa pale kwa muda mrefu. Mtu wa kwenye buti akawasikia wanawake wale wakipiga story na walinzi wa kizuizi ambao walidai wameelemewa na kazi kwa kuwa wakati ule kulikuwa na walevi wengi kutoka Finland wanavuka border kwenda Urusi kwenye Tamasha la vijana. Laiti walinzi hawa wangejua kuwa wanachati na Majasusi wa MI6 wa Uingeleza, hakika wangeacha kabisa kupiga michapo na kuvaa sura za kazi. Baada ya muda wanaume wao walirudi garini na safari ikaendelea wakaingia Finland.
Alipofika finland, maafisa wa m16 wali msafirisha kwenda uingeleza.
Ilikuwa ndio mara ya kwanza mtu anafanikiwa kutorishwa kutoka mikononi mwa KGB Miaka sita baadae kupitia wanadiplomasia, Urusi iliiachia familia yake ikaungane naye Londoni anakoishi hadi hivi sasa.
Mwisho, I mean no to nobody.