Ubinadamu unapo ingia kwenye maslahi ya wakubwa, na kupelekea tafrani

Ubinadamu unapo ingia kwenye maslahi ya wakubwa, na kupelekea tafrani

Episode 3.

Sometimes May 1988 Leninsky Prospekt, Moscow Tower 8th Floor, Apartment No. 103 Naam! Ni katika ghorofa maarufu kabisa kwa jina la Moscow tower Jijini Moscow Urusi. Wote wanaoshi kwenye ghorofa hili ni majasusi wa KGB pamoja na familia zao.

Sisi tupo kwenye ghorofa la nane, nyumba namba 103 katika jengo hili lililoko mtaa wa Leninsky Katika nyumba hii namba 103, inawachukuwa chini ya dakika moja tu kwa watu fulani kufungua mlango mkuu wa nyumba hii kwa funguo malaya. Walipofungua mlango, watu wawili ndani ya mavazi ya Overalls na mikononi wakiwa na gloves, wanaanza kuipekua kwa umakini vyumba hii. Wakati hawa wakifanya hivi, wengine wawili ambao ni mafundi wanaendelea kufunga vifaa vya kunasa sauti kwa visivyoonekana kwenye karatasi za ukutani, skating, na kwenye mkonga wa simu.

Pia wanafunga camera za siri kwenye taa sebuleni,chumbani na jikoni. Kazi hii waliimaliza ndani ya saa moja, hakuna sehemu ndani ya nyumba hii ambayo haikuwa kwenye sikio au macho yao. Naamanisha hakuna ambacho wasingeona au kusikia. Kisha watu hawa wanafaa masks usoni na kuanza kupulizia vumbi linalotoa mionzi kwenye nguo na viatu ndani ya kabati.
Wanakuwa makini kupulizia vumbi chache ili lisimdhuru atayevaa lakini pia liwe la kutosha kuweza kujua kila hatua anayotembea wanayemuwekea kwa kutumia kifaa cha Geiger Counter.

Watu hawa wanaondoka baada ya kufunga mlango wa mbele. Lakini wakiwa wamefanya kosa moja la kiufundi. Masaa machache yaliyofata, afisa wa juu wa KGB alitua katika uwanja wa ndege wa Sheremetyevo jijini Moscow kwa ndege aina ya Aeroflot akitokea London Uingeleza. Afisa huyu alikuwa amepanda vyeo haraka haraka baada ya kuwafurahisha mabosi wake kwa kazi zake nzuri zilizotukuka. Ni muda mfupi tu alikuwa amepewa Promotion hadi rank ya Kanali na mkuu wa KGB London.

Alikuwa anarudi Moscow baada ya kupewa wito kuwa wakuu wake wanataka kumpa baraka kwa cheo chake kipya. Kiufupi afisa huyu alijua sababu za wito huu ilikuwa ni hadaa tub ali lazima kuna kitu tofauti kisichohusiana na Promotion yake. Mwanaume huyu wa miaka 46 mwenye mwili uliojengeka kimazoezi, akiwa na na mafunzo yote ya kunusa hatari iliyo mbele yake, alitembea kwenye jengo la Airport kusogelea ofisi za uhamiaji.
Akamkabidhi afisa wa uhamiaji hati yake ya kusafiria ambaye aliitizama kwa muda mrefu isivyo kawaida. Muda huu mwanaume huu akautumia kushangaa kwa nini hakuna aliyekuja kumpokea japo kuonyesha heshima kwa kanali wa KGB anayetokea ughaibuni? Pamoja na kumkosa wa kumpokea aliamini kabisa kuna mtu au watu wapo pale uwanjani wakimfatilia nyendo zake.

Alipopewa Passport yake akatoka nje ya jengo huku akijiuliza nini sababu za kuitwa kwake? Akaita taxi na kuipanda Akaendelea kujiuliza akiwa garini! Je wamemshuku kwa lolote? Kama ingekuwa hivyo si ilipaswa akamatwe punde tu alipofika? Akafika nyumbani kwake kwenye jengo la ghorofa mtaa wa Leninsky, Moscow tower. Akapandisha mpaka floor ya nane ilipo nyumba yake Namba 103 ambako hakuwepo kwa zaidi ya miezi minne tangu January. Akafungua kitasa cha kwanza kikafunguka, na cha pili hivyohivyo Shida ikawa kwenye kitasa cha tatu

Kwanza kitasa kile hakuwa hakukifunga na funguo, pili hakuwa na funguo zake Sasa leo akashangaa kukuta kimefungwa. Kwa mafunzo yake ya kijasusi akawa ameshajiridhisha kuwa alipata “ugeni” usio rasmi. Kwa kuwa lile ni jengo la KGB akajua lazima ndio walikuwa wageni. Akajionya ajipe utulivu ingawa kengele ya hatari ilishamlilia kichwani.
Akaomba msaada wa mmoja wa majirani ambaye alikuwa mtundu wa vitasa na aliwasaidia kila milango inapojifunga. Akaingia ndani ambako aliamini hadi muda huo anasikilizwa na kutizamwa na watu kutokea sehemu asiyoijua.

Akajiambia ajipe utulivu wala asifanye matendo ya kutia mashaka ikiwemo kutafuta vinasa sauti au cameras. Akalala Kesho yake akaenda kazini lakini hakuitwa na wakuu wake kama alivyotarajia Zikapita siku nne hali ikiwa vilevile huku akiwa ameanza kuchoshwa na hali ile. Siku ya tano akaitwa na mkuu wake wa idara na kuambiwa anahitajika kwa mahojiano kwenye jengo moja mbali na pale. Wakiwa kule wakaja maafisa wawili wa KGB ambao hakuwajua lakini wao wakajitambulisha kama mkuu wa Department K na mwingine akiwa ni mkuu wa uchunguzi wa ndani. Si unaijua Moscow kwa baridi na Pombe kali? Basi pale ikaletwa mzinga wa Vodka na sandwich jamaa akamiminiwa kinywaji na wale maafisa hivyo hivyo. Wakagonga cheers na kubugia Ugimbi.

oh! Dakika chache tu jamaa akaanza kuona ulimi wake mzito na kizunguzungu Yeye kama KGB akabaini kilichotokea! Ni kwamba alinyweshwa kinywaji tofauti na wenzake, Yeye alinyweshwa kitu kinaitwa “Truth serum” kwa kiswahili kiite “Msemakweli”. Kwa majasusi wa KGB wao walikiita SP-117 au wafamasia wanakiita PENTOTHAL mbayo kikemia ni Sodium Thiopental. Kinywaji hiki hutumiwa na majasusi kuhoji watu wanaokuwa wagumu kutoa ushirikiano au wenye uwezo mkubwa wa kufaulu kipimo cha kugundua muongo(Polygraph) Matumizi ya kinywaji hiki kwenye mahojiano yanapingwa sana na wanasheria kwa kuwa yanakihuka haki ya mtuhumiwa ya ku “remain silent” Katika ulimwengu wa kijasusi hawajali mambo ya kisheria bali wanajali matokeo.
Tuendelee! Jamaa akaanza kuhojiwa kwa nini anaisaliti nchi kwa kuuza taarifa kwa adui? Akakana katakata madai yake! Jamaa alikuwa anaijua KGB ndani nje pamoja na mbinu zake za kuhoji. Alipoona hajapelekwa kwenye selo ya mateso ya KGB alijua atahojiwa kwa njia hii ukizingatia yeye ni afisa wa ngazi ya juu.

Pia alijua lazima watu hawa hawajathibitisha tuhuma dhidi yake ndio maana hawajamuua tangu anatua Airport. Kwa kuwa alijua atahojiwa kwa kutumia mbinu ya Truth serum basi alipoambiwa tu anaenda kwenye mahojiano akameza ya “ Pep pills” ambazo zilikuwa zina uwezo wa kupambana na truth serum.

Mahojiano haya hayakuzaa matunda. Afisa huyu akaambiwa hatatoka tena Russia kwenda kufanya kazi ughaibuni, asijaribu milele kupiga simu na akitaka kuomba likizo ndani ya Urusi anaruhusiwa. Jamaa bado hakuhadaika, inawezekanaje mtu anayeshukiwa kwa uhaini kama yeye aendelee kupewa mshahara na ruhusa ya likizo? Akaamini bado kuna uchunguzi dhidi yake unafanywa kukusanya ushaidi, na ukipatikana kifo kinamnyemelea. Akiwa bado anashangaa, familia yake aliyoiacha London ikarejeshwa Urusi. Akajua familia yake imerudishwa kimkakati.

Akaona sasa inatakiwa aanze kukumbuka Mission moja ya hatari ambayo mwanzoni aliidharau kuwa haiwezi kufanikiwa. Akaichukua kamusi fulani ya Oxford na kuiloweka kwenye maji kisha kwenye cover lake la akabandua karatasi fulani ya plastic aliyoanza kuikalili kama msaafu.

Naam! Mission PIMLICO Hii mission ilikuwa imeandaliwa kwa ustadi mkubwa na kachero wa Uingeleza mwanadada Veronica Price. Kutokana na umuhimu wa kachero Oleg kwa serikali ya Uingeleza ikaonekana awekewe mkakati wa ulinzi kumuokoa endapo serikali yake ya Urusi itambaini kuwa anauza taaria zao kwao.
Hadi wakati ule hakukuwa na historia ya mtu yeyote kutoroshwa kutoka Urusi sembuse tu kwa afisa wao wa KGB wanayemshuku kwa uhaini. Mission hii ilionekana kama ndoto ya mchana hata mbele ya macho ya Oleg mwenyewe. Hata hivyo Veronika alimsisitiza Oleg kui revise na kuifanyia rehearsal akiwa Moscow Signaling point ikapangwa iwe duka la mikate.
View attachment 2919057

I will be back, I mean no malice to nobody.
Safi Sana.
 
Back
Top Bottom