Ubinafsishwaji Bandari tatizo la Watanzania ni lugha ya Kingereza, Mkataba upo sawa

Mkuu umewahi fanya biashara kweli wewe?

Unawezaji kuvunja mkataba bila makubaliano
kuna aina mbali mbali za ku terminate contract, mutual agreement ni mojawapo sio njia pekee

huhitaji kuwa Mfanyabiashara kujua masuala ya kimkataba …

kwa leo nenda ka google hili neno

'force majeure ' halafu rudi hapa nikupe darsa la kimkataba na njia mbali mbali za kuvunja mkataba zaid ya ile uliyokariri ya mutual agreement
 
Siyo kwenye bandari tu bali kwenye maeneo mengi hatuna watu wenye uchungu na nchi hii. Watu wengi ni mafisadi na wezi hawafikirii kuijenga nchi kwa maslahi ya wote bali matumbo yao tu. Naunga mkono uamuzi wa Serikali kuwapa wageni bandari nikiamini uamuzi huo una tija kwa taifa.
 
Kama umesoma basinulitoka kapa bado hiyo article uonibtatizo lako unatusema kutojua kiingereza wakati wewe ndo hujaelewa?

Ati unasema kama wakitaka kuvunja mkataba kuwepo na makubaliano? Huu ndo ujinga wenyewe.

So wakae mezani ati sasa tuvunje mkataba upuuzi gani huu hamani hatankama mnalipwa ila mmezidi.
 
Kwa vyovyote vile nendeni mkauze Bandari yenu huko Unguja.

Sisi tuacheni na Bandari zetu hivi hivi zilivyo, ni zetu tunazipenda
 
Ulisoma wapi. Nchi imepanic unaongea upuuzi
 
Mkataba uvunjwe kwa pande mbili mmoja akichemka akakataa kuvunja mkataba nini kinatokea ?? Hebu andika iko kiingereza unachohisi unakijua kuliko wengine tuone.
 
Mkataba uvunjwe kwa pande mbili mmoja akichemka akakataa kuvunja mkataba nini kinatokea ?? Hebu andika iko kiingereza unachohisi unakijua kuliko wengine tuone.
Huwezi kuvunja mkataba bila makubaliano ,kama unataka kuvunja unafuata article 20
 
Acha bangi wewe
 
Hizo rushwa mlizokula hamtozikwa nazo
 
Mkataba uvunjwe kwa makubaliano ya pande mbili …kwa hiyo anae under perform au asietekeleza wajibu wake halafu akakataa hayo " Makubalino ya pande mbili ' nini kinatokea ?

tunataka TOR za Mkataba sio blaa blaaa
Ukitaka kuvunja fuata sheria za kimataifa kwenye article 20 ndio kilichoandikwa ,

Sasa unataka uvunje vunje hovyo mkataba

Mkataba sio ndoa ile
 
Kwa vyovyote vile nendeni mkauze Bandari yenu huko Unguja.

Sisi tuacheni na Bandari zetu hivi hivi zilivyo, ni zetu tunazipenda
Hakuna bandari inayoenda kuuzwa, kuna uwekezaji mkubwa unaotaka kwenda kufanyika kuhakikisha kuna maximum output ya kuhudumia ndani na nchi zinazoizunguka Tanzania.

Hakuna ata hayo makubaliano ya muda.

Watanzania inabidi mjikite kwenye maswali ya msingi ya terms za huo uwekezaji hizo ndio info za msingi kwenye kuamua yale yale ya ovyo kama Bagamoyo na mchina. Au huku kuna terms nzuri.

Hii tunayojadili ni framework tu, itakayotumika kutengenezea terms za mkataba.

Inaelezea implied terms za sheria zetu za kodi, land na nyingine kama za mazingira ndio zitatumika. Mikataba yenyewe ya HGA ikishatemgenezwa itatafsiriwa kwa English law, sasa kwenye English serious breach inavunja mkataba.

Shida ni uelewa tu na upotoshaji wa wachambuzi uchwara; hakuna ata hizo HGA as yet zilizosainiwa.
 
Mkuu kuna watu wanajitoa fahamu kwa ubinafsi tu

Bandari ingekuwa mali yao binafsi wangeweza kuingia mkataba wa namna hii?
 
Africa hapawezi kuwa salama forever. Sis waafrica tumekuwa na bahat mbaya.
 
wewe sio mtanzania bila shaka, kiujumla huo mkataba wenu niwa kimabavu , pelekeni huko
 
Bandari ya Dar es salaam, ni mali ya waTanganyika, sio mali ya waZanzibar, sasa waTanganyika tunapaswa kuamua juu ya mali zetu...
HAIKUBALIKI!
HAIKUBALIKI!
HATA KIDOGO!
Zanzibar pia wana Bandari...
 
Kwa hiyo wewe kwa Tanganyika hii ndiye unayejua kiingereza tu?

Kuongea kiingereza siyo kuijua lugha ya kiingereza na hasa hii inayotumika kuandika mikataba, sheria, mou etc.

Hata kama mikataba ingeandikwa kwa kiswahili, bado ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuelewa kwa ufasaha kilichoandikwa.

Hili swala la mkataba wa kukodishwa kwa bandari ya DSM kwa DP World halistahili majibu mepesi.
 
Viongozi wetu na watu wetu wenye mamlaka hawana uwezo kiakili wakudeal na vitu kama hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…