Ubinafsishwaji Bandari tatizo la Watanzania ni lugha ya Kingereza, Mkataba upo sawa

Ubinafsishwaji Bandari tatizo la Watanzania ni lugha ya Kingereza, Mkataba upo sawa

2. Vyama vya serikali vinakubaliana kwamba utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya mradi na DPW unategemea kuhitimishwa kwa makubaliano thabiti ya mradi, haki za ardhi, na HGAs kwa kila mradi husika.
 
Hilo linaeleweka binadamu wote atuwezi kuwa na mtazamo sawa.

Muhimu ni kuhakikisha hitimisho lako la kukataa ni kutokana na kupitia habari sahihi. Sio kwenda kwenye mijadala ya space moderator anaepinga uwekezaji hajui hata ‘berth’ ni kitu gani.

Provided wewe mwenyewe umejiridhisha kwa kupitia facts, mimi nani nikulazimishe kukubali.
Mkuu kama unao huo mkataba naomba niusome tafadhali🙏🙏
 
ELimu, Elimu, Elimu ni kitu muhimu sana. Tanzania tuna tatizo kubwa ya lugha ya Kingereza kwa watu wetu. Lugha ya Kiswahili haina maneno na misamiati iliyojitosheleza, hivyo tafsiri toka Kingereza kwenda Kiswahili mara nyingi kumejaa ukanjanja na uwongo.

Tatizo kubwa kubwa ni watu kutafsiri Kingereza kwenye lugha zao mama, halafu baadae kutafasiri kwenda Kiswahili!

Article 23 kati ya Mkataba wa Emirates of Dubai na Serikali ya Tanzania kuhusu usimamiaji na uendeshaji wa bandari unapotoshwa hapa JF.

Article 23 inazungumzia Termination and Duration, hakuna sehemu yeyote inayosema serikali ya Tanzania au Emirates of Dubai hawaruhusiwi kuvunja mkataba. Mkataba utaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili, ndio kilichoandikwa.

Artcle 20 inazungumzia dispute settlement, Mkataba unazungumzia ikitokea kuna kutokuelewana kwenye article 23 basi usuluhishi ufuate Sheria za Kimataifa na mazungumzo yafanywe kwa Kingereza, yafanyike Johanesburg Afrika ya Kusini kwa pande zote kuwa na wawakilishi.

Tuache kupotosha raia kwa mihemko ya kisiasa na wengine kufikia hatua ya kumtukana Rais, tatizo sio Mkataba tatizo ni watu kutokuelewa lugha ya Kingereza.
Tuambie na unapovunjwa fidia yake inakuwaje?
 
Una utindio wa ubongo wewe.
Nani kakwambia watanzania hawajelewa mkataba.

Hebu tutafsirie wewe mwingireza tuone labda utakuja na uelewa tofauti na walivyoelewa watz wengine

Mbunge wako mdee aliushika mkataba ila matatizo akawa anayatoa kichwani.anaambiwa aonyeshe ye yuko na hisia tuh.
 
Wewe umetafsiri vip mkuu?
Alafu lugha na elimu wapi na wapi?
 
wewe unaejua kingereza ungetoka na kuuelimisha umma nadhani ungekuwa umefanya jambo la msingi sana

sasa umeishia kulalama hapa kwamba mamaako alitukanwa ungekuja kumtetea kwa hoja nadhani ungeeleweka sana

tofauti na hapo mtoa post hatukutofautishi na chawa wengine 😎
 
ELimu, Elimu, Elimu ni kitu muhimu sana. Tanzania tuna tatizo kubwa ya lugha ya Kingereza kwa watu wetu. Lugha ya Kiswahili haina maneno na misamiati iliyojitosheleza, hivyo tafsiri toka Kingereza kwenda Kiswahili mara nyingi kumejaa ukanjanja na uwongo.

Tatizo kubwa kubwa ni watu kutafsiri Kingereza kwenye lugha zao mama, halafu baadae kutafasiri kwenda Kiswahili!

Article 23 kati ya Mkataba wa Emirates of Dubai na Serikali ya Tanzania kuhusu usimamiaji na uendeshaji wa bandari unapotoshwa hapa JF.

Article 23 inazungumzia Termination and Duration, hakuna sehemu yeyote inayosema serikali ya Tanzania au Emirates of Dubai hawaruhusiwi kuvunja mkataba. Mkataba utaweza kuvunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili, ndio kilichoandikwa.

Artcle 20 inazungumzia dispute settlement, Mkataba unazungumzia ikitokea kuna kutokuelewana kwenye article 23 basi usuluhishi ufuate Sheria za Kimataifa na mazungumzo yafanywe kwa Kingereza, yafanyike Johanesburg Afrika ya Kusini kwa pande zote kuwa na wawakilishi.

Tuache kupotosha raia kwa mihemko ya kisiasa na wengine kufikia hatua ya kumtukana Rais, tatizo sio Mkataba tatizo ni watu kutokuelewa lugha ya Kingereza.
Mwenye tatizo kubwa kwenye hicho kiingereza, lazima.mojawapo ni wewe.

Mkataba unazungumzia kuwa termination ya mkataba inaweza kufanywa kwa makubaliano ya pande zote mbili. Umejiuliza, kama upande mmoja ukitaka kufanya termination, upande mwingine hautaki, kutatokea nini?

Na halafu unatakiwa kutofautisha kati ya contract termination na life of the contract. Watu hawaongelei termination, wanauliza life of the contract. Mkataba ni lazima uwe muda wake wa maisha, mambobyanayoweza kusababisha kukoma mkataba kabla ya muda wa mkataba kwisha.

Kwenye huo mkataba wamesema life ya the contract ni muda gani?
 
Hakuna ata hiyo mikataba, as yet. Hiyo ni framework tu. Ata hiyo agreement inataka HGA zikisainiwa ziwe siri.

Mambo wanayopigia kelele Article 20 na 23; ni mambo ya kawaida if anything ni aspects za ‘stabilisation clauses’ ata sijui kwanini wameziweka tofauti.

Na hakuna mkataba wa kimataifa popote duniani usio na ivyo vipengele. Nimeskiliza Lissu contract
law inaonekana is not his thing, maelezo yake yana upotoshaji mkubwa. Sio kwa makusudi, ila uelewa.
Usijiona unajua sana kumbe wewe ni kisoda kwenye pipa.

Mimi binafsi nimeshiriki kuandaa mikataba zaidi ya 30 ya multinational comapanies, ikihusisha makampuni na serijali, nje ya Tanzania. Mimi sikusomea sheria, lakini kwa namna nilivyofanya kazi kwenye haya masuala ya mikataba, mara nyingi nimekuwa na uelewa mkubwa maradufu ya wanasheria wengi nadharia. Na mara nyingi tulivyokuwa kwenye vikao vya mikataba, mara nyingi wengi walidhania nimesomea sheria, wengine hata nilipowaambia kuwa hiyo siyo fani yangu, hawakuamini. Ufahamu kuwa practice ndiyo iliyotengeneza theory ambayo wanaenda kufundishwa wale ambao hawajawahi ku-practice.

Hiyo unayosema ni framework, ukweli ndiyo mother contract. Mikataba mingine yote midogo midogo ni lazima iwe ndani ya mkataba mkuu.

Mkataba huu ndio unatoa mwongozo wa mikataba midogo itakayofuata. Hivyo mkataba mwongozo unatakiwa kuwa detailed and elaborative well eneough ili kuhakikisha hakutokei madudu kwenye mikataba midogo.

Yawezekana wewe ni mwanasheria nadharia. Watafute practical lawyers wakueleweshe.
 
Shida ni watu ambao wanasoma bila ya background knowledge, article 23 (4) inaelezea uwezi kuvunja mkataba kiholela.

Article 20 inaelezea taratibu sahihi za kufuatwa kunapo migogoro kwanza inapendekezwa diplomatic dialogue, ikishindikana ndio baraza la usuluhishi S.A; hiyo sehemu uchaguliwa na kukubaliwa na pande zote.

Shida ni uelewa tu
Nakubaliana nawe kuwa wenye matatuzo ya uelewa mpo wengi sana.

Maana kama u ashindwa kuelewa umujimu wa mkataba mkuu, unasema eti hiyo ni framework tu! Kazi ya framework ni nini?

Kipi ni kikubwa kati ya hiyo unayoiita framework na mikataba midogo itakayosainiwa baadaye?
 
tatizo si lugha kama unafikiri hivyo basi wewe ndo unatatizo.huwezi kugeneralize kwamba watz hawajui lugha na ati kiswahili hakijitoshelezi hiyo ni fikra finyu.hizo article ulizozitaja tayari zina matatizo.kwa nn setlement ifanyike nje ya nchi na siyo ndani ya nchi!huko nje ndo tunakopigiwa hiyo mikataba.na kwa nini serikali inaulazimisha huo mkataba?kama kuna tatizo la uendeshaji kwani hawaezi kufanya maboresho mengine badala ya kubinafsisha?historia inaonyesha kwa tz ubinafsishaji unapofanyika huwa hautuachi salama na mifano ipo,TICTS nk.haya makampuni ya waarabu huwa hayalipi wananchi wetu ujira mzuri na hilo liko wazi kabisa.kama wananchi walalamika huyo mradi uachwe kwa sababu bandari ni mali ya watz.kagame aliishatukejeli kuwa angepewa yeye hiyo bandari hata kwa siku tatu tungeona maajabu.aliishatujua watz ni wapigaji tu na hatuna uchungu na hii nchi.
Huyu ni mwanasheria koko. Hajui kuwa kuna sheria inayozuia migogoro ya kiuwekezaji kuamliwa na mahakama za nje ya Tanzania. Halafu anajifanya eti ni mwanasheria.

Huenda ni hakimu wa mahakama ya mwanzo.
 
Kuvunjika kwa mkataba maana yake ni matokeo ya kutofautina hivyo hakuna makubaliano. Kama hukuna makubaliano inawezekana vipi tena makubaliano ya pande mbili ndio ya uvunje huu mkataba???

Ingetakiwa iwe hivi mkataba utavunjika kwa sababu ya kutokubaliana kwa pande mbili. Baada ya hapo zianishwe sababu zote za kushindwa kukubaliana kama vile mkandarasi kushindwa kufikia ufanisi wa utendaji nk nk nk.

Mkataba unakuwa je na kipengele eti mali za mkandarasi hazitataifishwa, Mambo ya ajabu sana haya kama kunafidia anatakiwa alipe na akashindwa ama kukaidi kulipa, unafanya nini ukikatazwa kutaifisha mali??? Kama ni kweli kuna hivi vipengele ndani ya huu mkataaba basi walio uandaa walikuwa ni watu wasiojali maslahi mapana ya nchi/Watanganyika.

Walikuwa na mitazamo na zile akili za kudharau, wakisema hivi vitu vya machogo haituhusu kutilia maanani na umakini kihivyo. Tuna uchungu gani hata hivyo zaidi ya maslahi yetu binafsi.
Upo sahihi kabisa. Kwa watu makini, mkataba ulistahili kuainisha ni mambo gani yatasababisha termination ya mkataba kabla ya muda wa uhai wa mkataba. Lakini mpaka sasa hakuna hata muda wa uhai wa mkataba.
 
Basi na mkataba kutohusisha bandari za Zanzibar ni tatizo letu la kielemu au kiingereza kama unavyotamani ionekane hivyo mtoa mada.
 
Hakuna mkataba usioweza kuvunjwa, ila sio kila contract breach ni ya kuvunja mkataba.

Kuna two main breaches:
Conditional: ambayo ina deprive one part main contractual agreement. Mfano umeahidi kuleta vifaa miaka miwili hakuna kitu. Hapo unaweza vunja mkataba.

Warranty: umeahidi kufanya kazi kwa miezi sita; umechelewa. Hiyo sio sababu ya kuvunja mkataba ni kudaiana fidia tu.

Kwa ivyo material breaches inaweza kuwa sehemu ya warranty pia; na nyingi sababu zake sio kuvunja mkataba.
Unaamua kuandika chochote ulicho nacho kichwani!!

Tunataka useme kwenye mkataba na DP, uhai wa mkataba ni miaka mingapi? Mambo gani yatasababisha contract termination prior life of the contract.
 
Back
Top Bottom