Ubishi kuhusu share za Wasafi Media naona umeisha sasa

Ubishi kuhusu share za Wasafi Media naona umeisha sasa

Kusaga anamuhitaji zaidi diamond kwenye biashara kuliko diamond anavyomuitaji kusaga imagine akiondoka diamond ikawa Kusaga tv itakuaje?
Ofcoz itakufaaa...So sasa itabdi wasanii wotr wamuabudu Mond maana wengi wanashangilia kudondoka kwa clouds...
 
Ofcoz itakufaaa...So sasa itabdi wasanii wotr wamuabudu Mond maana wengi wanashangilia kudondoka kwa clouds...
Wakimuabudu itakuwa ni upumbavu wao na Diamond kama lengo lake ni kuabudiwa na sio mapinduzi aliyojinasibu nayo basi na yeye ataangukia pua tu. Kikubwa ni kuhakikisha kila msanii anapata support ya Media bila matabaka sio unagombana na mfanyakazi wa media fulani basi nyimbo zako hazipigwi au anakuwekea figisu flani flani hiki ndicho cha kuepukwa.
 
upo sawa kabisaa...! Na mond anaweza kuwa mbaya mara 2 zaidi ya clouds maana Mond nae anatafuta bado na ni mwanamziki so awezi kubali wengne wang'ae zaidi yake...
 
unazu
Baada ya sintofahamu ya umiliki halisi wa hisa za wasafi media leo kila kitu kipo wazi, kuna kipindi watu walikadiria diamond kumiliki asilimia 8 ila imekuwa wazi sasa kwamba kijana wetu nembo ya Tanzania Diamond Platnumza Anamiliki hisa asilimia 45 katika wasafi media

Kwa hisa asilimia 45 diamond ana nguvu hizi

1.Kuwepo kwenye Bodi wa kampuni ya wasafi (hapa pia ni c.e.o wa wasafi)
2.Kushiriki katika kutengeneza sera za kampuni
3.kuhusishwa katika mijadala ya mienendo ya kifedha katika kampuni
4.uwezo wa kuuzianna bidhaa na kampuni ya wasafi
5.uwezo wa kupachika mameneja katika kampuni ya wasafi media
6.kuweza kutoa ushauri wa kitaaluma unaoweza kuisaida wasafi media

Tukirudi katika mapato atayopata Diamond ni kwamba mfano wasafi media imetengeneza faida inayobakia kwa wanahisa ya bilioni 1 basi Diamond anachukua milioni 450 huku kusaga akichukua asilimia 53 (milioni 530) na nyingnine asilimia 2 (milioni 29 ) itaenda kwa mwengine ambaye hajajulikana vizuri.

Ikumbukwe kwamba katika makampuni ni kawaida sana kuwa na wanahisa wengi na kuna kipindi hata alieanzisha kampuni huwa na hisa chache kuliko wengine kama ambavyo mwanzilishi wa facebook anavyomiliki asilimia 25 tu za hisa katika kampuni, Vile vile hata kampuni ya Microsoft wengi wamekuwa wakidhani kwamba yupo Bill Gates peke yake ila kuna wanahisa wengine, Ni jambo la kheri mno msanii ambae ni moja ya nembo ya Tanzania kuleta chachu ya wasanii kujikomboa na kuanza kutumia umaarufu na jitihada zao ili wafike mbali.

KAMA IMEKUKERA HAMIA POST NYINGINE
bilioni unaizungumzia kirahisi rahisi utafikiri hekaya za Mwanri
 
Ambacho wengi mnakwepa kusema ni kuwa Kusaga mwenye 53% kimsingi ndiye anayeweza kufanya maamuzi (majority shareholders) ya Wasafi Media. Technically, Wasafi Media ni mojawapo ya makampuni ya Kusaga.

Wale wanadhani CMG inapambana WM na hivyo kuchukua upande, hawajijui tu kuwa wanatumika kwenye biashara za Kusaga.
 
Domo na Zari ni wasanii kwahiyo maisha ya wasanii 90% ni maigizo,10% ndio uhalisia............Domo anajua kucheza na social media,anatumia fan base yake na vijana timu yake aliowaajiri kujipromote kwenye mitandao ambapo kwake inamuongezea dau la kwenye mikataba,hivi promoter ukisikia domo kanunua jumba la milioni 400 hivi ukitaka kumpa show utafikiri utampa ofer ya mili 2 au 3? Kwahiyo hayo majumba wanayonunua kwenye instagram na facebook ni za kiinstagramu tu,They are doin for the instagrammers and facebookers tu,ndio maana pamoja na utajiri mkubwa wa domo alionao kwenye instagram na facebook still anaishi kwenye kiwanja cha 25 kwa 25 madale.
Acha gubu
 
Watu wanapagawa na maisha yake ya kwenye mitandao...Hajajiulizi kama ni Bilionea kweli kwanini mpaka Leo nyumba yake inayojulikana mpaka anaiimba kwenye nyimbo zake za Utanipenda na Baila ni Ile Ile ya Madale kwanini hana nyumba nyingine?!

Gari ya ndoto zake ni Royce Rolls kwanini kama kweli ni Bilionea mpaka Leo hana hiyo gari?!
Kwani lazima ataje nyumba zote?
 
Kijana kajitahidi ingawa ndo kishauza brand, hiyo 450 anayopata bado hajagawana na kina babu tale, salaam, mkubwa fella n.k. Ajitahidi siku moja amiliki kitu chake kwa asilimia mia.
ni ngumu kumiliki asilimia 100 hizi biashara zinataka lazima ushrikiane na watu ndio utafika unapokwenda. angalia BILL GATE uliza anamiliki hisa kiasi gani ndo utajua uzuri na ubaya wa HISA. Japo utaitwa wewe ndio mwenye mali lakini ndani ya mali hiyo wapo wanaokuzidi kipato.
 
Ubilionea ni jina tu.....ondoa cost of production....na kodi....na kama kampuni ipo kwenye hasara....basi kiwango cha uwajibikaji ni hicho hicho kwenye asilimia.....sema wtz kwasababu shule ni ndogo..... wanadhani hiyo pesa inabebwa tu.....
Mkuu kwa faida ya wengine;
Cost of production hapa haimhusu Diamond. Hii gharama ya uzalishaji inatolewa kwenye mapato (sales) za kipindi husika.
Gharama ambayo Mondi atakatwa ni kodi ya gawio (dividend) ambayo kitaalamu inaitwa "With holding tax".
Yeye ni mwanahisa, baada ya kulipa gharama zote ikiwemo na kodi ya makampuni/mashirika kitaalam inajulikana kama "corporate tax", utaitishwa mkuu (AGM) kwa lengo la kukubaliana kama kuna ulazima wa kutoa gawio kwa mwaka husika au la. Wakikubaliana kutoa gawio ndiyo kila mwenye hisa atapata kulingana na idadi ya hisa zake na kila gawio litakatwa with holding tax ya 5%.
 
upo sawa kabisaa...! Na mond anaweza kuwa mbaya mara 2 zaidi ya clouds maana Mond nae anatafuta bado na ni mwanamziki so awezi kubali wengne wang'ae zaidi yake...
Kama angekuwa na roho ya kukataa wengine wasing'ae leo asingekuwa na WCB, asingekuwa na Rayvany aliyeshinda tuzo ya BET ambayo yy hana. Alafu mbona unapenda kumuwekea ugumu Diamond, Diamond hana roho ya ubinafsi, hajasoma lkn ni genius na ana roho ya kizungu.
 
Nitajie Kampuni inayomilikiwa na mtu mmoja 100%, tatizo wengi tunajiona wajuaji hata kwenye mambo tusiyokuwa na ufahamu nayo. Kampuni yoyote ili ipige hatua inahitaji wadau (ShareHolders) hata kama ni ya familia utakuta humohumo ndani ya familia kila mmoja ana asilimia (share) zake.
Kijana kajitahidi ingawa ndo kishauza brand, hiyo 450 anayopata bado hajagawana na kina babu tale, salaam, mkubwa fella n.k. Ajitahidi siku moja amiliki kitu chake kwa asilimia mia.
 
Nitajie Kampuni inayomilikiwa na mtu mmoja 100%, tatizo wengi tunajiona wajuaji hata kwenye mambo tusiyokuwa na ufahamu nayo. Kampuni yoyote ili ipige hatua inahitaji wadau (ShareHolders) hata kama ni ya familia utakuta humohumo ndani ya familia kila mmoja ana asilimia (share) zake.
Umaskini unawasumbua, mimi mwenyewe tajiri namiliki kampuni yangu kwa asilimia 100. Acheni mawazo ya kimaskini.
 
Nitajie Kampuni inayomilikiwa na mtu mmoja 100%, tatizo wengi tunajiona wajuaji hata kwenye mambo tusiyokuwa na ufahamu nayo. Kampuni yoyote ili ipige hatua inahitaji wadau (ShareHolders) hata kama ni ya familia utakuta humohumo ndani ya familia kila mmoja ana asilimia (share) zake.
Rationale ya kuwa na shareholders wengi ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom