Mkuu kwa faida ya wengine;
Cost of production hapa haimhusu Diamond. Hii gharama ya uzalishaji inatolewa kwenye mapato (sales) za kipindi husika.
Gharama ambayo Mondi atakatwa ni kodi ya gawio (dividend) ambayo kitaalamu inaitwa "With holding tax".
Yeye ni mwanahisa, baada ya kulipa gharama zote ikiwemo na kodi ya makampuni/mashirika kitaalam inajulikana kama "corporate tax", utaitishwa mkuu (AGM) kwa lengo la kukubaliana kama kuna ulazima wa kutoa gawio kwa mwaka husika au la. Wakikubaliana kutoa gawio ndiyo kila mwenye hisa atapata kulingana na idadi ya hisa zake na kila gawio litakatwa with holding tax ya 5%.