Ubongo Baada ya Kifo: Je, Bado Unawaza?

Inatokana na imani yako kama ni abrahamic religion utaenda kuzimu kujiandaa kwenda aidha peponi au motoni, kama budha na hinduism utakuwa Reincarnated kwenye mwili mwingine au scientifically ndio mwisho wako huo
kwahiyo imani utakayo amini ndio ukweli hukohuko utakapoenda
 
ndo tufute eksi na kunyoa vudhi sio unakufa unabaki kuona aibu
 
 
Nafsi hupachikwa kwenye mwili pindi mtoto afikishapo miezi minne akiwa tumboni, nafsi hutoka kwa Mungu kwani yeye ndiye chanzo cha uhai.
umejuaje kama nafsi hupachikwa kwa mtoto kwa muda huo na pia umejuaje kama inatoka kwa mungu?? ukinipa na evidence nitashukuru
 
umejuaje kama nafsi hupachikwa kwa mtoto kwa muda huo na pia umejuaje kama inatoka kwa mungu?? ukinipa na evidence nitashukuru
Kwanza hakuna anayezaliwa anajua, sote tunajifunza kupitia vitabu hasa vitabu vitakatifu, na mimi sibagui kitabu vyote naviamini kwani vimetoka kwa Mungu.

Hii ni kwa mujibu wa kitabu cha Quran👇👇

Surat As-Sajdah (32:7-9):

"Aliyeumba kila kitu kwa uzuri wake, na akaanza kumuumba mwanadamu kutokana na udongo. Kisha akafanya kizazi chake kitokane na kiini cha maji duni. Kisha akamtengeneza sawasawa na akampulizia roho Yake, na akajaalieni masikio, na macho, na nyoyo. Lakini ni wachache mnaoshukuru."
 
Ubongo ndo organ ya mwisho kuacha kufanya kazi after death, niliisoma mahali, so wanasema unaweza kusikia sauti za watu au pengine kuwa na mawazo fulani, lakini nini hasa utokea wakati wa kifo inabaki kuwa speculation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…