SoC04 Ubora wa usajiri wa vijana kwenye mradi wa kilimo wa Build Better Tomorrow (BBT) ili kuleta tija kwa vijana na taifa kiujumla

SoC04 Ubora wa usajiri wa vijana kwenye mradi wa kilimo wa Build Better Tomorrow (BBT) ili kuleta tija kwa vijana na taifa kiujumla

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Jun 10, 2024
Posts
1
Reaction score
1

Mradi wa build better tomorrow (BBT)
Ambao serikari kupitia wizara ya kilimo ulianzisha mwaka 2022/2023
Lengo kuu ni kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo na ufugaji na kupunguza tatizo la ajira nchini

Yafuatayo yafanyike ili kuboresha mradi huu uwe endelevu na wenye tija Kwa vijana na taifa kiujumla
  • vijana waliomaliza shahada stashada na astashada za kilimo na ufugaji katika vyuo vikuuu na vyuo vya kati kama vile SUA na vyuo vya kati ( vyuo vya MATI) wapewe kipaumbele Cha kusajiliwa Kwenye huu mradi wa bbt na sio kila mtu mwenye nia apate nafasi​
Ili mradi uwe endelevu unahitaji vijana wenye taaluma ya kilimo na ufugaji Kwa 100% Kwa sababu mradi ndio unaanza kutumia vijana wenye taaluma kutafanya mradi ufanyike kwa ufanisi zaidi kuliko kuwatumia watu waliopewa mafunzo ya muda mfupi​
  • Zifuatazo ni faida za kubadilisha mfumo wa kusajiri vijana Kwenye mradi wa bbt
  •    a) Itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa mafunzo Kwa vijana Kwa muda mrefu kama kuwaweka kambini Kwa miezi minne na kuwaghamia chakula matibabu makazi na posho kitu ambacho kinaongeza gharama za kuendesha mradi wakati gharama hizi zinaepukika kirahisi zaid​
  • Kwa sababu vijana wenye taaluma hawahitaji kuwaweka kambini Kwa miezi minne ili kuwapa mafunzo hivyo gharama za chakula maradhi na makazi ambazo serikari imetenga zitapungua kuzielekeza kwenye maeneo mengine kama kununua vifaaa vya kisasa vya kilimo​
  • b)Pia itasaidia wizara ya elimu kupima na kutathmini ubora na viwango vya elimu inayotolewa kupitia taasisi zake za vyuo vikuuu na vya kati kama una matokeo chanya na yanaendana na uhalisia​
  • c)Itasaidia kupunguza tatizo la ajira Kwa vijana wengi waliomaliza elimu ya vyuo vikuuu na vya kati nchini​
d)Itasaidia kupunguza hatari zinazoweza kujitokeza wakati wa shughuri za uzalishaji Kwa zitokanazo na kutumia vijana wasio na taaluma na uzoefu Kwa asilimia kubwa

HITIMISHO
Mwisho niiombe serikali kupitia wizara ya kilimo ili mradi huu uwe endelevu unaliwa ukusanye vijana walio hitimu mafunzo ya kilimo na ufu
gaji katika vyuo vyote nchini ili kufanya uwe endelevu Kwa sababu utasimamiwa na vijana wenye taaluma ili baada ya misimu kadhaa kupitia na kujiridhisha sasa mradi umesimama vizuri ndipo serikali ichukue na vijana wengine walio mtaani
 
Upvote 6
Back
Top Bottom