Ubovu wa barabara Kisukulu Maji Chumvi - Segerea ni kero kubwa

Ubovu wa barabara Kisukulu Maji Chumvi - Segerea ni kero kubwa

uchumi2018

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2018
Posts
1,657
Reaction score
2,406
Ndugu wanajamvi Nawasalimuni kwa jina la jamhuri ya muungano.

Nimeona niamke na hoja hii kwani wakazi wa kisukulu tumejikuta kwenye mateso ya muda mrefu. Kwa wale wasiojua kisukulu ni wapi, Kisukulu ni kata inayoangukia kwenye jimbo la uchaguzi la segerea wilaya ya ilala kwa utambulisho zaidi naweza kusema Tabata kisukulu.

Iko hivi. Ukiwa unatokea mabibo external (Mandera road) kuna njia ya lami inayoelekea tabata kimanga,Kimara korogwe,kisukulu na segerea kupitia jeshini.

Ukiendelea mbele kuna daraja maarufu (maji chumvi) pale barabara ya lami inachepuka kwenda kutokea kimara korogwe hiyo yote ni lami,lakini mara baada ya kuvuka daraja ukinyosha kuna barabara ya vumbi ambayo inaenda kuunganika na barabara ya lami (bonyokwa segerea). Hicho kipande japokuwa ni kiungo muhimu sana ni kibovu sana na kinaharibu magari na kusababisha hasara kubwa hasa eneo korofi sana ni pale panapoitwa KAGENYI.

Mbali na kuharibika kwa magari,ikitokea gari limepakia mgonjwa au mama mjamzito au vifaa vyovyote vinavyohitaji uangalifu, unaweza kujikuta umesababisha matatizo zaidi ya lengo lako la kutoa msaada.

Ndugu zangu, kufuatana na barabara hii kuwa ni mkato na inarahisisha kukwepa foleni za magari (Buguruni) yanayotokea
Ubungo kwenda segerea, kinyerezi, majumbasita, kitunda kuelekea Gongo la Mboto na viunga vyake mpaka majohe
Tumejikuta wananchi wa Tabata kisukulu hata tulipojitahidi kutumia nguvu zetu kuziba hayo mashimo haichukui muda kuharibika
kufuatia wengi wa magari yanayotumia njia hii.

Andiko hili lina lengo la kuomba msaada kwa mamlaka husika,kwamba pamoja na ahadi zilizowahi kutolewa
kwamba DMDP watashughulikia, tunaomba matengenezo ya muda mfupi kwa kuweka kifusi angalau barabara ipitike kirahisi.
Pia kuwatahadharisha wakazi wa kitunda, Gongo la Mboto n.k wenye magari madogo wasije haribu magari yao kwa kutafuta njia mkato.

Baba yetu Mh.Isdori Mpango, waumini wenzako tuliosali wote kigango cha Mazda tukitokea kisukulu kwa sasa ni ngumu kufika kama unatumia gari inabidi uende parokia ya makoka japo kuna umbali.

Tunakuomba utuangalie kwa jicho la huruma ututoe kwenye mateso haya. Pia ndugu yetu Mh. Chongolo ,Tunakuomba pia uliangalie jambo hili utusaidie.

Nawashukuru sana ndugu zangu kwa kusoma.

Kazi iendelee.
 
ni inazingua hasa halafu haifanyiwi chochote yani miaka inaenda tu barabara imejaa mashimo.
 
ni inazingua hasa halafu haifanyiwi chochote yani miaka inaenda tu barabara imejaa mashimo.
Ni kweli kabisa mkuu,ukiangalia foleni ya magari eneo hilo asubuhi na jioni,ndipo utaelewa umuhimu wa barabara hiyo.
pamoja na ubovu na kuharibu magari lakini inabidi watu walazimike kuitumia kwa sababu ya kuokoa muda.
 
ngoja kidogo tu erythrocyte atakuja na mawazo ya BAVICHA kuwa katiba ndiyo inasababisha haya
 
Ni kweli kabisa mkuu,ukiangalia foleni ya magari eneo hila asubuhi na jioni,ndipo utaelewa umuhimu wa barabara hiyo.
pamoja na ubovu na kuharibu magari lakini inabidi watu walazimike kuitumia kwa sababu ya kuokoa muda.
Tumeipenda CCM wenyewe. Subirini wakati wa kampeni 2025!
'Kazi iendelee'
 
Haki yako kisha unaiomba kama msaada tena kwa kutaka huruma.

Nyie ndio mnawapa viburi hawa takataka wanaojiita viongozi ile hali ni wahuni wa kisiasa.
Ndugu yangu uyasemayo yana ukweli ila,inabidi kuafakali kuwa haki inakuwa haki pale
inapopatikana bila jasho,kama haipatikani inabidi upaze sauti watoa haki wakusikie upate hiyo haki.
 
ngoja kidogo tu erythrocyte atakuja na mawazo ya BAVICHA kuwa katiba ndiyo inasababisha haya
Toa mawazo yako mkuu,nini kifanyike ili tupate heri,wakati tukimsubiri huyo uliyemtaja.
 
Tumeipenda CCM wenyewe. Subirini wakati wa kampeni 2025!
'Kazi iendelee'
Naamini mbunge wetu,diwani wetu na viongozi wetu wa serikali za mitaa wamekusoma,watafanya kitu kabla ya hiyo 2025.
Wakati mwingine unakuta jimbo ni kubwa mbunge anaishi mbali kutoka eneo hilo lilipo.
Na wakati mwingine hapiti barabara hiyo.
 
Migombani hapo...mmezidi wizi na uchawi kile kiduka cha Dr Mbena karibu na Mawenzi Bar anauzaga na mauchawi tupu! humo humo!! Tena waziwazi

kule nyuma anawekaga nini?? km mnajua??....ndo maana laana haziwaishi. Mnaroga sana sirikali nyie watu.hasa mlioko kando kando ya brbara...Sirikali ikijenga barabara itabomoa kisukuru yoote ile!! Mko barbrni mnoooo!!

Ndo maana mnaroga ma greda! Yansishiwa nguvu!
 
Dah,🙄🙄,kiongozi hii umetoa kali lakini umenisaidia,
sasa naanza kupata mwanga,ila nina swali kidogo,kwani serikali nayo inalogwa?
 
Dah hii barabara sina hamu nayo huwa naitumia kama mchepuko nitokee Segerea kwenda kifuru

Asee imeniharibia gari vibaya sana sitakuja pita tena ule uchafu ila kwa nn barabara nzuri huwa haziboreshwi yani ina mawe mashimo af ni vilima
 
Pole sana mkuu,yaani kiufupi ni majanga,heri yako unayeitumia kama mchepuko lakini kwetu wakazi ni zaidi ya kero.
Kwa kweli hii barabara kama ingeboreshwa ingefungua njia kwa magari yote yanayoenda majumba sita kutokea ubungo.
Ni short cut nzuri sana inaokoa muda na mafuta.
 
Migombani hapo...mmezidi wizi na uchawi kile kiduka cha Dr Mbena karibu na Mawenzi Bar anauzaga na mauchawi tupu! humo humo!! Tena waziwazi

kule nyuma anawekaga nini?? km mnajua??....ndo maana laana haziwaishi. Mnaroga sana sirikali nyie watu.hasa mlioko kando kando ya brbara...Sirikali ikijenga barabara itabomoa kisukuru yoote ile!! Mko barbrni mnoooo!!

Ndo maana mnaroga ma greda! Yansishiwa nguvu!
Tusamehe tuuu,endapo uyasemayo yana ukweli,dunia ina watu wa aina zote na ni kila mahali,na hii isitumike kuumiza '"innocent people"
kwa ugomvi na maslahi binafsi.
Ila kama unaitumia hii kama kinga ya madaraka utakwama
maana safari ya kufichua kinachoendelea ndo imeanzo hivyo.
 
Lipa tozo za miamala barabara ijengwe la sivyo komaa
Kazi ya kulipa tozo inaendelea mkuu,ila kuna maeneo yalitengenezwa hata kabla hiyo tozo haijaanzishwa
hapo tuiteje? ndo maana nikaamua kuvunja ukimya ili tusijepitwa hata wakati huu wa tozo.
 
Kazi ya kulipa tozo inaendelea mkuu,ila kuna maeneo yalitengenezwa hata kabla hiyo tozo haijaanzishwa
hapo tuiteje? ndo maana nikaamua kuvunja ukimya ili tusijepitwa hata wakati huu wa tozo.
Yalitengenezwa kwa lami au vumbi? Kama ni changarawe hiyo ni kawaida bila shaka watarudia maana hakuna barabara za kudumu za udongo.

Ila kama lami hapo tumbueni meneja wa Tarura.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na meneja wa Tarura kwenye Eneo lako kwa email au nenda ofisini kwao wanaweza wakawa na ufumbuzi kwa sababu Kazi kwa sasa ziko kwenye manunuzi
 
Asante sana kiongozi kwa ushauri,hii barabara imetengenezwa kwa kifusi,ila ukiangalia magari yanayopita na umuhimu wake wa kuunganisha kata zaidi ya moja kama nilivyoeleza hapo juu unaona ina umuhimu wa kujengwa kwa kwango cha lami.
 
Back
Top Bottom