Ubunge EALA ni Vita kali CCM. Mpaka sasa ni makada 64 tayari wamevuta fomu

Ubunge EALA ni Vita kali CCM. Mpaka sasa ni makada 64 tayari wamevuta fomu

Makada 64 CCM wapigana vikumbo ubunge Afrika Mashariki​

Ubunge PIC

Wiki moja baada ya kufunguliwa kwa pazia la ubunge wa Afrika Mashariki (EALA), wanachama 64 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamejitokea hadi leo Alhamisi, Agosti 4, 2022 kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo.​


Idadi hiyo inaashiria mchuano mkali katika kinyang’anyiro hicho, kinachohitaji watu tisa wakiwemo wawakilishi kutoka vyama vya upinzani.

Miongoni mwa makada wa chama hicho waliojitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo ni Godfrey Shirima, Dk Paul Anthony, Henry Bulengera,Paschal Mayalla na James Kasurura.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganaizesheni, Maudline Castico amewataja wengine ni Nasikiwa Berya, Amina Mgeni, Ambwene Kajura, Nasser Nzamba, Prakseda Marmo, Maria Kangoye na Shogo Mlozi.

“Yupo Alfa Munyi, Manase Michael, Ayubu Lemilya na Nicksoni Kahimba waliochukulia Dar es Salaam, huku Haji Vuai Ussi, akichukua kwa upande wa Zanzibar,” amesema.

Kwa mujibu wa Castico, milango ya kuchukua fomu za kuwania nafasi hizo itakuwa wazi hadi Agost 10, 2022.



#Kaka yetu Mayalla Paskali kila lenye heri
Kila lenye heri chama langu la CCM,
 
Pole sana comrade Paskali Mayala kwa kuanguka kwenye uteuzi uliofannywa na CC ya CCM.
Kuna nyakati maamuzi yanafanyika ambayo they don't work in favour of people with ability, but it doesn't indicate those unchosen are less important.

Kwa muono wangu, Paskali yuko so much connect and know to many people in the corridors of power. Bila shaka angetumia nafasi hii kugombea wale jamaa wangali hai, huenda Paskali angekuwa na substantial contribution either mjengo wa Idodomya au Makao makuu ya EA.

Kaka mkubwa Paskali ameona fursa ya kuingia nyakati za Farao asiemjua mzee Andrew Mayalla.

Hongera kwa kuonesha nia, na pole kwa matokeo ambayo hayakuwa upande wako.

Weekend njema.
 
Back
Top Bottom