Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Mkuu kawadanganye watoto wadogo! Hivi kweli wananchi wengi kwenye kituo cha kupigia kura wawe wanamtaka mgombea wa CDM wangeacha kufanyafujo kama kungekuwa na uonevu wa kiasi hicho??

Hizo fujo unazosema ndio zilipelekea Akwilina kupoteza maisha, viongozi wa cdm kuwa na kesi mpaka leo. Narudia tena, huu uhayawani uko wazi sana, na wananchi waliuona kila mahali. Ndio maana uliona idadi ndogo sana ya watu kujitokeza kujiandikisha uchaguzi wa SM. Hakuna mtu ana muda wa kushiriki ushenzi. Sasa subiri uchaguzi wa 2020 uone idadi ya wapiga kura itakavyokuwa ndogo. Huu uzi nitauvuta kwa ushahidi.
 
Amber Rutty naye nilimsikia anagusia uwezekano Wa kugombea sijui eneo gani,bunge litashine sana
 
Kumbe hilo mnalijua fika kuwa watu wote hatuwezi kuipenda ccm, sasa inakuwaje mnatuona kama siyo watanzania sisi tusiyo ipenda ccm?
Wewe utabaki kuwa ndugu na mtanzania
Tatizo mnavuka mipaka na kukosa uzalendo
 
Watapungua kwa kuwa watz wengi wanaimani na Rais Magu na wanajua hakuna wakumshinda toka upinzani na wabunge itategemea jimbo na jimbo ila tuseme ukweli wapinzani mwaka huu watapata tabu sana. Wakina Mbowe na genge lake wamalizie ruzuku za mwisho mwisho!
 
Wewe utabaki kuwa ndugu na mtanzania
Tatizo mnavuka mipaka na kukosa uzalendo

Kuvuka mipaka ni kutokuipenda ccm, na kutokumsujudia magu ni kukosa uzalendo? Hivi ni Nani kawapa kipimo cha kupimia uzalendo?
 
Kuvuka mipaka ni kutokuipenda ccm, na kutokumsujudia magu ni kukosa uzalendo? Hivi ni Nani kawapa kipimo cha kupimia uzalendo?
Kuvuka mipaka ni pale unaposhangilia ndege kukamatwa,au kushadidia nchi iwekewe vikwazo vya kiuchumi
 
Atashinda kihalali kabisa.
 

Siku Barcelona ikicheza na simba ni wazi Barcelona itaifunga simba, je washabiki wa simba wataacha kwenda uwanjani kisa Barcelona atashinda? Ni hivi, Magufuli hawezi siasa za ushindani na hatakaa aziweze, hata hiki kinachoendelea ndani ya chaguzi zetu hivi sasa ni kwasababu yeye hataki ushindani, kwani kwake kushindwa ni aibu ndio maana ananajisi mchakato wa uchaguzi. Fuatilia kipindi chake cha ubunge ni mara ngapi aliwahi kushinda kwa njia ya kura zaidi ya figisu? Wananchi nao ni waelewa, hawashiriki sio kwakuwa wanamkubali, bali wanatuma ujumbe kuwa walishatoka kwenye dunia ya kupatiwa viongozi kwa shuruti.

Hizi tabia za kiongozi eti anakubalika na kushinda kwa asilimia kubwa, ziko kwenye nchi nyingi zinazoendeshwa kidictator, na katika nchi hizo mazingira ya uchaguzi huwa ya figisu za wazi ili kuuhadaa umma na dunia kuwa kiongozi husika na chama chake wanakubalika. Lakini kwa bahati mbaya, wananchi na dunia huwa wanajua Hadaa zote hiyo. Mfano wa chaguzi za hadaa ambazo hata wananchi na dunia walizipuuza ni Zimbabwe enzi za Mugabe, Sudan chini ya Elbashir, Egypt chini ya Hosni Mubarak, Rwanda chini ya Kagame nk. Tabia hiyo ya chaguzi za kishenzi nayo imehamia hapa nchini chini ya Magufuli, na ndio maana sasa hivi wananchi na dunia wanapuuza chaguzi zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…