Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Uchaguzi 2020 Ubunge Kigoma Mjini, Zitto Kabwe vs Diamond Platnumz

Pasi na shaka atashinda, lakini mshika mawili moja humponyoka, ngoja tuone.
 
Hakuna ubaya lakini kwenye mambo ya siasa inabidi tuwe serious kidogo.
 
Kwa diamond kugombea ubunge ni level ndogo sana tena ya kujidhalilisha sawa na sumaye toka waziri mkuu na kuwa mkuu wa kanda ya chadema mashariki,heri nikalime mahindi.
 
Yeah ni kweli. Ona mwanazuoni kama profesa, japo ana mchango mkubwa, atazidiwa umaarufu na msanii. Kanumba ni mfano.
Kwa akili za Watanzania, Diamond hata akigombea Urais anashinda. Ila Diamond hajijui tu kuwa yeye ni mkubwa kuliko wanasiasa.Tena akigombea Kigoma atashinda asubuhi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond anaweza kutumia umaarufu wake wa muziki kuupata ubunge. Lakini akishakuwa mbunge, hatakuwa na umaarufu wowote bungeni kwa sababu katika siasa hana cha pekee.

Kwenye muziki, Diamond ana uniqueness, lakini hana kitu hiyo sifa katika ubunge, na wala ubunge haitamfanya awe maarufu zaidi katika muziki.
 
Yeah ni kweli. Ona mwanazuoni kama profesa, japo ana mchango mkubwa, atazidiwa umaarufu na msanii. Kanumba ni mfano.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani hii ni jamii nzima duniani .Angalia Kim Kardashian umaarufu wao sioni impact yao kwenye jamii. Kuna wanasayansi wamegundua HIV wala siyo maarufu. Yaani jamii sijui tumeumbwa vipi. Yaani mimi naona tunakuwa attached zaidi kwa vitu vinavyotupa burudani.
 
Sioni tatizo kumtoa mkongoman na kumuweka mkongoman mwingine
 
Yaani hii ni jamii nzima duniani .Angalia Kim Kardashian umaarufu wao sioni impact yao kwenye jamii. Kuna wanasayansi wamegundua HIV wala siyo maarufu. Yaani jamii sijui tumeumbwa vipi. Yaani mimi naona tunakuwa attached zaidi kwa vitu vinavyotupa burudani.
watu muhimu sana duniani hawajali kujulikana Ila wanatengeneza pesa ndefu pia. Maisha ya ufamous yanaharibu akili. Watu muhimu kwa uhai wa binadamu ni vyema wasiwe famous. Waache wanasiasa na wanamziki wachukue hizo nafasi.
 
Mkuu naheshimu maoni yako, akina Abood, Mkono nk ni wabunge, je huyo Diamonds ana hela kuliko wao? Kuna wakati Mo alikuwa mbunge, je utajiri wake wa wakati huo ulikuwa mdogo kuliko huu wa Diamondi hivi sasa? Kumbuka diamonds bado haijawa na hela za ukweli ambazo kwake ubunge ni kitu kidogo, kwani ubunge pia utamuongezea ujiko kwenye huo usanii wake. Kimsingi huyu mleta uzi ameleta hii hadithi ili kufurahisha genge, lakini sio habari ya kweli.
Abood na Mo walikuwa wanataka ubunge kwa ajili ya faida ya biashara zao.Ukiwa mbunge unaweza kutumia cheo chako usilipe Kodi pia kusafeguard biashara zako sasa DIAMOND PLATNUMZ atafute ubunge kwa kipi? Kama umaarufu anao mkubwa Sana Kama pesa anayo pesa nyingi mpaka wakati mwingine anatumia kutoa misaada kwa watu tumeona kigoma kutengeneza visima viwili, kachsngia madawati 600 tandale,katoa bima za afya kwa wamama 40, katoa bajaji 45 kwa walemavu n.k hakuna sababu za msingi zitakazomfanya DIAMOND PLATNUMZ agombee ubunge naona kabisa mtoa mada ametulisha matango pori.
 
Nimedokezwa na wadau hapa Kigoma ya kwamba wazee wanamtaka Diamond agombee.nafasi ya ubunge hapo kigoma mjini badala ya Zitto Kabwe.

Wanadai Zitto kawatelekeza, kahamishia harakati zake twitter na ndani ya jiji la Dar badala ya kuhudumia wanakigoma.

Magwiji hao wa siasa kigoma wanamtaka Diamond awe mgombea wao kupitia chama cha mapinduzi ,wana imani atawawakilisha Barbara,

Kama ni kweli huu ndio mwisho wa ndugu yetu Zitto aliehamishia majukumu yake Twitter.

Kila la kheri Diamond katika.utumishi wako wa ubunge, hakuna wa kukuzuia

Sent using Jamii Forums mobile app
uzi wa kijinga sana ktk mwaka huu mpya
 
Back
Top Bottom