Uchaguzi 2020 Ubunge Tarime Mjini: Ngicho ahamishia nguvu zake kwa Gerald Martin

Waitara kiukweli hakubaliki na hana sita Kama Mama Kabaka. Huyu Mama Kabaka Ni mtu mzuri na anayependwa na wana Tarime wote na sifa zake zinajulikana. Waitara Ni mbunge mwenye sifa mbaya tangu Ukonga na huku kwetu. Kiufupi Wajumbe walijichanganya na Heche atampiga asubuhi kabla jogoo hajawika
 
Hata Jimbo la Rorya rushwa ilitumika sana hasa namba 1,2, na 3. Natumaini kuwa TAKUKURU waliliona na watatolea taarifa.
 
UBUNGE TARIME MJINI: NGICHO/WAITARA WAHAMISHIA NGUVU ZAO KWA GERALD MARTIN

Kura za maoni Jimbo la Tarime Mjini zilifanyika tarehe 21 Julai 2020 na Jackson Kangoye akafanikiwa kuongoza kwa idadi ya kura. Inafahamika kwamba Jackson Kangoye na Mwita Waitara walitengeneza muungano ili kusaidiana katika kura za maoni za Tarime Mjini na Tarime Vijijini.

Na wote wawili walitegemea msaada wa Kamati ya Siasa Tarime katika kupindisha tararibu ili waweze kupata upendeleo dhidi ya wagombea wengine. Itakumbukwa Kamati hiyo ya siasa inayoongozwa na Mwenyekiti Daudi Marwa Ngicho, mchimbaji mdogo wa madini ambaye pamoja na mengine ana tuhuma mbalimbali katika hizo biashara zake.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Daudi Ngicho alihakikisha anaweka wabunge ambao watakuwa watiifu kwake na mara nyingi sana amewatishia waliokuwa wakishindana na Mwita Waitara ili kuhakikisha kuwa anapata nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Tarime Vijijini.

Kura za maoni zilifanikisha mpango wao kwa wote kushinda kura za maoni, japo iko wazi kilichotumika kuwapa hizo kura ni rushwa ambayo iko wazi. Baada ya kura hizo wananchi wengi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wameonyesha wazi kutokubali mapendekezo hayo ya wagombea maana hayaendani na matarajio ya wapiga kura wa Jimbo la Tarime Mjini na pia Tarime Vijijini.

Baada ya kujiridhisha kuwa Jackson Kangoye hakubaliki, ameruka na kuangalia jinsi anavyoweza kuitumia kamati ya siasa kumpendekeza mshindi wa tatu, Gerlad Martin, ambaye naye alipata kura 20 baada ya kuwa mtoa rushwa pia na taarifa zake zipo wazi.

Ngicho, Waitara wamekubaliana ni bora katika kikao cha kamati ya siasa kujaribu kushawishi na kumpendekeza Gerald Martin, kwani kwao ni mtu dhaifu ambaye wanaweza kummiliki na akafanya yale wanayotaka wao.

Na ikumbukwe Jumuiya ya Vijana Tarime kwa muda mrefu walijigeuza kuwa kikundi cha kumpigia Kampeni kinyume na kanuni za Uchaguzi. Hivyo ilikuwa rahisi Mwenyekiti wa UVCCM Tarime kumshawishi Waitara na Ngicho kuwa bora waende na Gerald, ambaye naye pia kiufupi sio mtu anayekubalika kwa wananchi maana hana mchango wowote kwenye jamii ukilinganisha na Michael Kembaki aliyekuwa mshindi wa pili na ambaye anakubalika.

Ngicho hamtaki Michael Kembaki kwa sababu haoni kama anaweza kummiliki kwa sababu ni mtu anayejitambua, mwenye biashara zake na asiyetegemea mtu katika maamuzi yake binafsi. Hivyo ameona ni bora ampiganie Gerlad, na kwa kuwa kamati nzima ya siasa iko chini yake na huwa anawalipa wote posho basi bila shaka anajua mapendekezo yake yote yatapita kwa asilimia 100.

Tunaomba viongozi wa kitaifa wa Chama waangalie kwa undani hali ya Tarime kwani maamuzi mabaya yatakayofanyika yatapelekea majimbo yetu kuendelea kuwa chini ya CHADEMA.

Wenu,
Venance Marwa,
Mwana CCM Mkereketwa Tarime.
Kaa huko na majungu yako maana hata hatukuelewi
 
Venance, kuna ukweli kidogo lakini mengi umeongeza chumvi sana.
 
Kumbe hata wanamme wakurya nao wana majungu!!
 
Hahaha majimbo yana wabunge tayari mnahangaika nini tena?!

Ona, hamuwataki kabla hamjawapoteza kura zenu, bora kuwapigia wanao kubalika na wengi, hao wa Chadema kuliko kupiga kura ikapotea.
 
Hapo Tarime Mjini Kuna Mama Fulani Ni Dr. Simkumbuki jina ana Sera na mipango madhubuti, japo sidhani Kama alikua na hela lakini Wajumbe hawakumpa kura
 
Hapo Tarime Mjini Kuna Mama Fulani Ni Dr. Simkumbuki jina ana Sera na mipango madhubuti, japo sidgani Kama alikua na hela lakini Wajumbe hawakumpa kura
wajumbe hawakuwa na muda wa kusikiliza sera, bali kupima pochi ya mgombea.
 
Waitara kiukweli hakubaliki na hana sita Kama Mama Kabaka. Huyu Mama Kabaka Ni mtu mzuri na anayependwa na wana Tarime wote na sifa zake zinajulikana. Waitara Ni mbunge mwenye sifa mbaya tangu Ukonga na huku kwetu. Kiufupi Wajumbe walijichanganya na Heche atampiga asubuhi kabla jogoo hajawika
tuna IMANI Kamati KUU itatupa chaguo sahihi la wana Tarime.
 
Hata Jimbo la Rorya rushwa ilitumika sana hasa namba 1,2, na 3. Natumaini kuwa TAKUKURU waliliona na watatolea taarifa.
Kwani kuna Jimbo rushwa haijatumika ?!. Acheni safari hii suba na nyancha zipambane . Girango na Luo imbo zisubiri miaka ijayo
 
Back
Top Bottom