Mimi siukatai muungano wa vyama vya upinzani, ila ukweli unabaki kuwa hauwezi kuwa endelevu kwa kuwa kila chama kina sera na malengo yake ya kushika madaraka ya nchi. Ni ukweli usiopingika kuwa kuungana kwa vyama hivi ni kuongeza nguvu ila matokeo yake vile viyenye nguvu ni kuendelea kuwa na nguvu zaidi na vile vidhaifu hatima yake ni kufa kabisa. Mfano TLP haiwezi tena kujitutumua kusimamisha wagombea wengi watakaokubaliwa na jamii kama vile sema CHADEMA au CUF, ndani ya muungano huu matokeo yake mwishoni ni nini? Umoja unaweza kuwa na nguvu kama vyama vitaunganishwa na kuwa chama kimoja, vinginevyo kila ukifika wakati kama huu ni mbio kama hizi ambazo baadae zinakosa mashiko na tija.Ndivyo upinzani unavyotakiwa kuwa, na sio vyama kuungana na kushindana na CCM tu
Bali kila chama kitumie jitihada zake kukishinda chama kingine chochote kilichosajiliwa
kauli za mvungi ndio zilimponza... Dr. Mvungi asilaani wananchi bali alaani ulimi wake
Viti maalumu? Labda abadili jina au aolewe na mtu wa mkoa mmoja kaskazini! kwi kwi kwi!!!
Acha fikra hizo za kuzingilwa na ukabila,angalia uwezo wa mtu kuchangia mawazo.Naamini kabisa, vigezo vilivyotumika na chadema ndio sahihi.Waliangalia zaidi mchango wa mtu na uwezo wa kifikra kuliko kugawa nafasi kwa kuangalia mtu ametokea wapi.Hizi fikra zinastahili kupuuzwa kabisa hazitusaidii kama watanzania. Utamaduni wa kitanzania unazingatia zaidi uzalendo wa mtu kuliko kuangalia mtu anatoka sehemu gani.
Mtanzania,
Mkuu heshima yako,Hivi Dr.Slaa amehalalishia wapi au ni kipi kilichokufanya useme Slaa amehalalisha hivyo vitendo.Kumbuka maesema ingawa haungi Mkono hizo vurugu,lakini alichokisema ni fact kwamba Maneno ya Dr. Mvungi ndiyo yaliyomponza.
Je,unadhani angenadi sera na kuacha kuichafua CHADEMA yangemkuta hayo? Sometimes inasikitisha kuona mwanasiuasa wa kariba ya Mvungi akifanya siasa Chafu badala ya kuwa kinara wa siasa safi yenye nia ya kuleta mabadiliko ktk taifa letu changa kisiasa.Anashindwa kutofautiana na Makamba types.
Pia wananchi wa Tarime walitegemea kuona upinzani unaungana,badala yake wanaona kila chama kinaibuka na mgombea na kingine kwenda mbali zaidi na kuwatukana CHADEMA ambao ni kipenzi cha wapenda demokrasia (Wanatarime).Kimsingi Mvungi ali-misbehave ingawa pia siungi mkono watu kutumia nguvu.
Sometimes ajifunze kutokana na makosa na aache kulalamika maanake inakua kama vile hataki ku-learn from the mistakes
na kwa chuki ya kukosa wabunge ndo maana wanaipiga vita CHADEMA!!!NCCR na TLP ni waganga njaa hao. Kwa kutokuwa na wabunge, vyanzo vyao vya mapato ni vya kubabaisha. Si ajabu wakanunuliwa na LISISIEMU. Who knows?