Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Hawa NCCR ni uroho na tamaa tu hakuna kingine......ni uwazi kuwa kule Tarime CHADEMA ndio wanakubalika sasa kiongozi unaenda unaongea maneno mbofu mbofu unategemea nini na wananchi wa kule wameamuka sio sawa na wananchi wa sehemu nyingine walio lelewa kwa kudanganywa danganywa wakule wanakumaliza hapo hapo.
 
Ndivyo upinzani unavyotakiwa kuwa, na sio vyama kuungana na kushindana na CCM tu
Bali kila chama kitumie jitihada zake kukishinda chama kingine chochote kilichosajiliwa
Mimi siukatai muungano wa vyama vya upinzani, ila ukweli unabaki kuwa hauwezi kuwa endelevu kwa kuwa kila chama kina sera na malengo yake ya kushika madaraka ya nchi. Ni ukweli usiopingika kuwa kuungana kwa vyama hivi ni kuongeza nguvu ila matokeo yake vile viyenye nguvu ni kuendelea kuwa na nguvu zaidi na vile vidhaifu hatima yake ni kufa kabisa. Mfano TLP haiwezi tena kujitutumua kusimamisha wagombea wengi watakaokubaliwa na jamii kama vile sema CHADEMA au CUF, ndani ya muungano huu matokeo yake mwishoni ni nini? Umoja unaweza kuwa na nguvu kama vyama vitaunganishwa na kuwa chama kimoja, vinginevyo kila ukifika wakati kama huu ni mbio kama hizi ambazo baadae zinakosa mashiko na tija.

'Alliance' zipo tangu zamani, lakini imekuwa daima ni mashirikiano ya mashaka kwani kila mmoja anatumia mbini ya kujifunza kuwa nini kinakufanya wewe unafanikiwa ili akupiku! Lakini mkiungana na kuwa na kitu kimoja suala la mashaka linakuwa halipo tena kwani ni kitu 1, na sio kama muunganiko unaofanana na Jamhuri yetu ya Muungano.

Namini vyama vichache vitaendelea kukuwa na kufikia kileleni kama hivi vilivyopo havitaungana na kuwa na chama kimoja kikubwa cha upinzani, japo itachukua miaka mingi, kitu ambacho sio kulitendea haki taifa letu.
 
Jamani NCCR wamejaa tamaa? No, hawana hata mbunge mmoja bungeni baada ya yule mzee wa Biharamulo kushindwa mahakamani.
Sasa badala ya kukaa na upande wa pili wa opposition waone watapata au la, unaona wanakuja na ujinga huu wa kurushia ndugu zao madongo.
Wataendelea kupigwa mawe na hawatapata kitu maana hiyo inaonyesha wana Tarime walikuwa wana beep.
Na nyinyi sisiemu bado zamu yenu maana hiyo ndio mnatumia mara kwa mara mkidhani mnadhoofisha upinzani.
Ole wako wewe mzee uliyechoka kisiasa Kingunge Ngombale Mwitu uliezoea kusema ovyo ovyo ukienda ukaeleza upuuzi huo huko Tarime hutarudi na macho.
Habari ndio hiyo.
 
Pamoja na hayo kwamba Dr. Mvungi aliponzwa na kauli zake lakini pia tukubali au tukatae wenzetu wa Tarime wana tabia za kupenda ushari sana. Sipendi kueleza mengi kuhusu tabia za wakazi wa wilaya hiyo maana wote huwa tunazisikia kwenye vyombo vya habari kila mara> Hata Slaa nao waangalie sana watakapokwenda huko maana bado wakazi wale wana hasira na yale yaliyokuwa yanaendelea ndani ya CHADEMA kati ya uongozi na marehemu Chacha kwa hiyo wasidhani kwamba labda kupigwa kwa mwenzao ndio tiketi ya wao kupokelewa kwa vifijo.
 
Hii ya Tarime sasa imegeuka kuwa every one against CHADEMA, wote wanaelekeza makombora, shutuma, nk dhidi ya chama kilichokuwa na jimbo hilo. CCM wakifanya hivyo inaeleweka, wanajitahidi kurejesha himaya yao, kwa hiyo watapambana na yeyote wafanikishe azma hiyo. Hao wengine wanataka nini na kwa faida ya nani?
 
Sio lazima vyama vya upinzani viungane na kutengeneza chama kimoja hioyo sidhani kama itawezekana. What they should do or should have done a long time ago ni kuhakikisha wana wabunge wengi hata nusu ndani ya bunge. Na hii inawezekana kama wapinzani hawatalumbana katika majimbo badala yake wamsimamishe mgombea kutoka chama kimoja kulingana na strenght za vyama vyao na kumpigia debe bila kujali ametoka chama kipi. Hapa ninaamini hata watz wataungana na wapinzani.
 
Viti maalumu? Labda abadili jina au aolewe na mtu wa mkoa mmoja kaskazini! kwi kwi kwi!!!

Acha fikra hizo za kuzingilwa na ukabila,angalia uwezo wa mtu kuchangia mawazo.Naamini kabisa, vigezo vilivyotumika na chadema ndio sahihi.Waliangalia zaidi mchango wa mtu na uwezo wa kifikra kuliko kugawa nafasi kwa kuangalia mtu ametokea wapi.Hizi fikra zinastahili kupuuzwa kabisa hazitusaidii kama watanzania. Utamaduni wa kitanzania unazingatia zaidi uzalendo wa mtu kuliko kuangalia mtu anatoka sehemu gani.
 
Eti CHADEMA walikua hawampendi Chacha!

Halafu mimi nataka huyo mzeee aliyejichokea na siasa zake za majitaka akapeleke propaganda Zake uchwara kule,maanke Kingunge amekosa ndhamu ya kitanzania kabisa.

Ngoja tuwaona na hao wanaojiita mabingwa wa kampeni akina Emmanuel nchimbi watasema nini maanke wamezoa kuwa-manipulate watu wasio na uelewa mkubwa wa mambo
 
huu ndio mwanzo wa kupoteza focus kwenye uchaguzi. vita vya panzi
 
Mimi nakuambia Hapa Jamvini kuna watu wakiaandika kitu unaweza kushtuka.Tanzania nako tuna wasomi ambao bado wamezingirwa na mila potofu na hawako tayari kubadilisha mawazo yao sasa sijui tutategemea nini kutoka wale ambao hawajafika hata
form 4?

Bado kuna wasomi ambao Akina kingunge na makamba wameweza na wamefanikiwa kupandikiza hisia kali za ukabila vichwani mwao hadi hawawezi jinasua.Kaazi kweli kweli.Mimi nadhani mabadiliko Tamzania yataletwa na wale watu wanotumia common sense zaidi wakiongozwa na wale wasomi wachache wazalendo na wenye misimamo kama ya Mwanafalsafa Socrates
 
Kwa haya ninayoyasoma sitashangaa jimbo la Tarime likienda CCM. CHADEMA kama mnapiga mawe ambao hamkubalini nao, je CCM nao wakituma vijana wao makusudi na kushambulia viongozi wa CHADEMA, mtalalamika?

Dr. Slaa hatakiwa kuhalalisha kwa njia yoyote ile vijana wa chama chake kutumia nguvu kuwanyamazisha viongozi wa vyama vingine.

Ninavyowajua CCM, tegemea vurugu kwenye mkutano wa CHADEMA na kisha tutaambiwa CHADEMA waliponzwa na maneno yao.

Dunia hii ukitaka kuwa salama ni muhimu kupinga double standards za aina zote. Aidha wakati mzuri wa kupinga jambo baya ni pale linapotumika dhidi ya adaui.
 
Acha fikra hizo za kuzingilwa na ukabila,angalia uwezo wa mtu kuchangia mawazo.Naamini kabisa, vigezo vilivyotumika na chadema ndio sahihi.Waliangalia zaidi mchango wa mtu na uwezo wa kifikra kuliko kugawa nafasi kwa kuangalia mtu ametokea wapi.Hizi fikra zinastahili kupuuzwa kabisa hazitusaidii kama watanzania. Utamaduni wa kitanzania unazingatia zaidi uzalendo wa mtu kuliko kuangalia mtu anatoka sehemu gani.

Nsaji,

Kama unakubaliana na vigezo walivyotumia CHADEMA, vigezo ambao vilipingwa na makamu mwenyekiti wao, vigezo ambavyo kwa kuvipinga vilimfanya Wangwe awe champion wa wana CHADEMA walio wengi mikoani basi wewe ni katika minority wa CHADEMA.

Mkabila sio anayeweza kuona vitendo vya kikabila bali ni yule anayefanya vitendo vya kikabila. Hapo amua mwenyewe.

Huyo lecturer wa mlimani, uwezo wa kufikiri ni mdogo kuliko wale dada wengine?

Yeyote mwenye kufikiri analiona tatizo juu ya hili. Hapo CHADEMA mmejifunga goli la kisigino.
Usitegemee CHADEMA wafanye tena uteuzi kama huo mwaka 2010 kwasababu hata kama wanakataa, lakini wanajua wamechemsha.
 
Mtanzania,

Mkuu heshima yako,Hivi Dr.Slaa amehalalishia wapi au ni kipi kilichokufanya useme Slaa amehalalisha hivyo vitendo.Kumbuka maesema ingawa haungi Mkono hizo vurugu,lakini alichokisema ni fact kwamba Maneno ya Dr. Mvungi ndiyo yaliyomponza.

Je,unadhani angenadi sera na kuacha kuichafua CHADEMA yangemkuta hayo? Sometimes inasikitisha kuona mwanasiuasa wa kariba ya Mvungi akifanya siasa Chafu badala ya kuwa kinara wa siasa safi yenye nia ya kuleta mabadiliko ktk taifa letu changa kisiasa.Anashindwa kutofautiana na Makamba types.

Pia wananchi wa Tarime walitegemea kuona upinzani unaungana,badala yake wanaona kila chama kinaibuka na mgombea na kingine kwenda mbali zaidi na kuwatukana CHADEMA ambao ni kipenzi cha wapenda demokrasia (Wanatarime).Kimsingi Mvungi ali-misbehave ingawa pia siungi mkono watu kutumia nguvu.

Sometimes ajifunze kutokana na makosa na aache kulalamika maanake inakua kama vile hataki ku-learn from the mistakes
 
Mtanzania,

Mkuu heshima yako,Hivi Dr.Slaa amehalalishia wapi au ni kipi kilichokufanya useme Slaa amehalalisha hivyo vitendo.Kumbuka maesema ingawa haungi Mkono hizo vurugu,lakini alichokisema ni fact kwamba Maneno ya Dr. Mvungi ndiyo yaliyomponza.

Je,unadhani angenadi sera na kuacha kuichafua CHADEMA yangemkuta hayo? Sometimes inasikitisha kuona mwanasiuasa wa kariba ya Mvungi akifanya siasa Chafu badala ya kuwa kinara wa siasa safi yenye nia ya kuleta mabadiliko ktk taifa letu changa kisiasa.Anashindwa kutofautiana na Makamba types.

Pia wananchi wa Tarime walitegemea kuona upinzani unaungana,badala yake wanaona kila chama kinaibuka na mgombea na kingine kwenda mbali zaidi na kuwatukana CHADEMA ambao ni kipenzi cha wapenda demokrasia (Wanatarime).Kimsingi Mvungi ali-misbehave ingawa pia siungi mkono watu kutumia nguvu.

Sometimes ajifunze kutokana na makosa na aache kulalamika maanake inakua kama vile hataki ku-learn from the mistakes

Ben,

Maneno kama hayo tumeyasikia sana. Mtu anaua mke, watu wanasema huyo mwanamke aliponzwa na umalaya wake. Ninachosema hata kama Dr. Mvungi alifanya makosa basi kuna njia nyingi za kisheria za kumchukulia hatua. Kama alikuwa anamsingizia Mbowe, basi kuna polisi, kama hamuwaamini polisi kuna mahakama.

Hakuna sababu ya kuhalalisha makosa. Unaweza usikubaliane na mimi lakini binafsi ndivyo ninaamini na kutenda.

Kwa siasa za mabavu za TZ, maneno kama hayo yanaweza kuwageukia muda sio mrefu. Kuna maneno mengi sana ya kashfa ambao wanasiasa wanatumia, sasa CCM nao wakitumia hao vijana wao, kweli mtaweza kupambana nao?

Wapenda demokrasi wanatumia mawe dhidi ya watu ambao hawakubaliani nao? Labda nirudi kwa mwalimu wa siasa akanifundishe tena maana ya demokrasia.
 
By the way, kwanini huyu Dr. pamoja na kufundisha muda mrefu - hadi kuwa Dean wa Faculty ya Law - hajaweza hadi sasa kuwa Professor?

Kaona bora avamie siasa. Siasa zina wenyewe!
 
NCCR na TLP ni waganga njaa hao. Kwa kutokuwa na wabunge, vyanzo vyao vya mapato ni vya kubabaisha. Si ajabu wakanunuliwa na LISISIEMU. Who knows?
 
NCCR na TLP ni waganga njaa hao. Kwa kutokuwa na wabunge, vyanzo vyao vya mapato ni vya kubabaisha. Si ajabu wakanunuliwa na LISISIEMU. Who knows?
na kwa chuki ya kukosa wabunge ndo maana wanaipiga vita CHADEMA!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom