Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Imebainika kuwa Askari zaidi ya 400 walio mwagwa Tarime wamegeuka omba omba na kupita kwenye maduka na kwenye kumbi za starehe wakiomba misaada ya kijamii zikiwepo fedha na vinywaji.....Inasemekana posho iliyo tolewa na Tume ya Uchaguzi ni kwa ajili ya siku ya kupiga kura na si kabla ya hapo...Msimamizi wa Tume ya uchaguzi kathibitisha..
 

..lack of coordination.
 
Hapa kuna kazi kweli, umefika wakati wa uchaguzi ambao wengi wanajua utakuwa wa amani lakini inaonekana kuwa kuna wengine wanawaona watu wa Tarime kama majuha hivi au mazimwi yenye kupenda fujo.

Swali kubwa ni moja.... hawa askari wamekuwa wapi miaka yote ambapo wanatarime na watanzania wamekuwa wanasumbuliwa na majambazi right and left?
 
CCM inajua kutatokea vurugu kwa sababu wataiba kura no wonder wamemwaga askari wengi maana wanajua wao ni wezi waliokubuhu kwa kura!
Na hawa watu watarime nadhani wameshajijengea sifa ya vurugu na inaonyesha vururgu zao ni za kiutuuzima ndio maana polisi wa kutosha tuu!
CCM mtashindwa kwa jina la Bwana Yesu!
 
Tatizo hapa hawa askari saizi wana njaa kali sana posho haitoshi wanayo pewa...je wana JF hamwoni kama njaa zao zinaweza zikasababisha watu kukosa amani???
Usiombee ukutane na askari mwenye njaaa atakung'ang'ania balaa hata kama ni haki yako.
 



Hahahahahah!
Utaratibu gani ulitumika? Ni dhahiri walipelekwa huko mtu anayefanana na mzee Makamba, maana yeye ni bingwa wa kutoa kauli na maamuzi ya kisomi.



.
 
Sitaki kuamini kuwa Jeshi la Polisi halina fungu la Operesheni maalumu. Yaani katika mipango yao wamekaa chini na kusema tunaenda Tarime, tutafanya a, b, c, na d. Wakafunga safari na magwanda yao. Na wakaanza kazi halafu ndio wakakumbuka bajeti? Wenzetu wanasema ni kuweka mkokoteni mbele na farasi nyuma!
 

Mwanakijiji,

Hii habari ingelikuwa kweli, ungeiona kwenye magazeti yote.

Sio rahisi polisi waliopelekwa na CCM kwenda kuwasaidia ushindi eti wakose pesa ya matumizi. Hilo sahau mkuu. Wako tayari mle nyasi ili wawalishe hao polisi.

Hizi habari ndio zile zile za kuwajaribu kuwadanganya Watanzania kwa faida za kisiasa.

Mtu anaongea na rafiki yake mmoja, tayari inageuka na kuwa official.
 


..kuna vitu vya ajabu nchi hii. mi wala sishangai wala kushtuka.

..haitakuwa mara ya kwanza.
 
Tarime risasi zavuma

2008-09-15 15:24:37
Na Usu-Emma Sindila, Jijini

SOURCE: Alasiri
 
Mwenyekiti wa Tuyme ya Uchaguzi, jaji makame, ametua Musoma leo hii. Alipofika moja kwa moja akaenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na wakaitwa maofisa wa Polisi wa mkoa.
Kilifanyika kikao na baadaye aliitwa Meneja wa CRDB. Kuitwa kwa meneja huyu inaweza kuwa kunaashiria kwamba kweli hakukuwa na fedha zilizopangwa kwa ajili ya posho ya hawa askari na sasa ndio zinatafutwa
 
Wakaange sumu wanywe!Yaani wao wanaenda kuhakikisha usalama ama to make sure CCM wanachinda at all costs?
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, jaji makame, ametua Musoma leo hii. Alipofika moja kwa moja akaenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na wakaitwa maofisa wa Polisi wa mkoa.
Kilifanyika kikao na baadaye aliitwa Meneja wa CRDB. Kuitwa kwa meneja huyu inaweza kuwa kunaashiria kwamba kweli hakukuwa na fedha zilizopangwa kwa ajili ya posho ya hawa askari na sasa ndio zinatafutwa
 
Taarifa za moto moto zimepatikana kutoka ndani ya vikao vya siri vya CCM zikieleza kuwa kikosi maalum kitapelekwa Tarime ambacho kitashirikiana na wazawa wa huko kuwafanyia fujo viongozi wa CHADEMA hasa wanaotoka mkoa wa KIlimanjaro.

Hili limeamuliwa baada ya kuona kuwa itakuwa fedheha kubwa kwa chama endapo CHADEMA hawatafanyiwa vurugu yoyote. Imezingatiwa pia kuwa kule Tarime kuna ugumu mkubwa sana wa kununua shahada za wapiga kura.

Maamuzi haya yamekuja kukiwa kuna kila umuhimu wa kuendelea kukitumia chama cha DP kupunguza kasi ya CHADEMA huko Tarime. DP wamepewa kazi ya kuinyima CHADEMA kuconcentrate katika uchaguzi kwa kufuatilia kesi na kujibu kashafa dhidi yao. Kazi hii inaweza kuwapatia DP 50m/=.

Hadi sasa hatujapata majina ya wanaoongoza kikosi hicho cha vurugu wala atakayewapokea huko Tarime.

Tafadhalini vuteni subira tutawapa habari zaidi kuhusu yale yanayotokea, yakiwepo majukumu ya siri waliyopewa kamanda Tossi. Msimamizi wa uchaguzi na viongozi wa serikali.
Kwa taarifa yenu CCM wameamua kuwa liwalo na liwe ni lazima washinde jimbo la Tarime
 
Kamende,
Usishangae hapa JF ukiulizwa kama una ushahidi wa hii habari uliyotuletea. Kuna wasioamini kabisa kwamba Mtikila anatumiwa na CCM kuhujumu Chadema.
 
mnajistukia wenyewe kuwa ni udaku...
Ndugu yangu Masatu niko Mwanza sasa hivi na kuna ushahidi wa kutosha kuwa wapo vijana wanaandaliwa kuelekea huko Tarime kuyafanya hayo. TUNAELEKEA KUBAYA
 
Kuthibitisha hainipi shida kama kuwashawishi wasiopenda uathirifu wa ukweli katika siasa.

Kama kuna mtu haamini kuwa Mtikila anatumiwa basi asubiri wamwone atakavyotoka kwenye hii hoja ya kutaka Uchunguzi wa kifo cha Wangwe ufanywe na Br. Snoot.

Kama kuna asiyeamini kuwa CCM watafanya fujo huko Tarime na ya kuwa wamejiridhisha kuwa shahada hazinunuliki basi asubiri.

Hata hivyo nitawaletea mpango mzima wa shughuli za NCCR Mageuzi huko Tarime.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…