Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

sidiria na muhogo tena on top of utoto? haya ndiyo nimekwambia kuwa baada ya kusoma postings zako zote (nimesoma zote) nimegundua wewe ni wa aina gani kutokana na maandishi yako mkuu. Yaani hukawii kufikia kwenye sidiria na mihogo na ndio maana ninatoa muda kujua undani wa swali lako - naona maandishi yako yameanza kutoa jibu tartibu.

Kwa kuanzia tu mkuu, Anza na kitu inaitwa cyanide ambayo inatumiwa sana na wachimba madini Tarime (na probably kwenye migodi yote ya dhahabu Tanzania).
 

Sikujua kama umeni-system postings zangu. Hongera sana kama umeweza kusoma postings zangu zaidi ya 1000. Natumaini utakuwa umevutiwa sana na niliyoandika.

CN, inatumika kwenye mining hasa kwenye kusafisha Gold. Hili lipo wazi, tatizo ni kuonyesha data za kuthibitisha kuwa inamwagwa kwenye mito bila kufanyiwa usafishaji (treatment) yoyote. Nafikiri hizi ndio data zinazotakiwa kuonyesha malalamiko yako.
 
Posted Date:: 23.09.2008 @00:17 EAT NEC official warns Wassira By Frederick Katulanda, Tarime

A returning officer for the Tarime parliamentary by-election intends to write a warning letter to Mr Stephen Wassira for using a Government vehicle during CCM election campaigns.

The officer, Ms Trasias Kagenzi, said the National Electoral Commission (NEC) had already cautioned against the use of Government vehicles in the campaigns.

But Mr Wassira, who is the minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives and Bunda member of parliament, violated the rules, she said.

Ms Kagenzi said apart from writing to Mr Wassira, the NEC would also write to the secretary general of the ruling party, CCM, to warn him against the use of Government vehicles in campaigns.

This follows a protest raised by the candidate of an opposition, NCCR-Mageuzi, Mr Enock Haruni.

He had reported that Mr Wassira had used a vehicle with Government plate numbers last Friday while campaigning in Tarime for his party.

The minister was receiving the CCM secretary general, Mr Yusufu Makamba and vice chairman, Mr Pius Msekwa, who launched campaigns for their candidate, Mr Ryoba Kangoye.

Mr Haruni claimed that the next day Mr Wassira also used the same vehicle, which belonged to the Tanzania Cotton Board.

However, its number plate was changed to show that it belonged to a parastatal, which is also illegal, he claimed.

Apart from Mr Wassira all other party dignitaries used vehicles with private number plates.
However, when contacted, Mr Wassira said he arrived with the car from Mwanza to attend the funeral of a former regional police commander and was not using it for campaign purposes.

He said he was very conversant with election regulations and could not have used the car for campaigns. He noted that in all campaigns he had been using a vehicle belonging to the MP for Rorya, Prof Philemon Sarungi. He said he would defend his stance if opposition parties raised queries on the matter.
 


Inaonekana huyu kijana wa NCCR ana hoja nzuri,WASSIRA aadhibiwe tu asitake kudaganya watu hapa.
 
Sikujua kama umeni-system postings zangu. Hongera sana kama umeweza kusoma postings zangu zaidi ya 1000. Natumaini utakuwa umevutiwa sana na niliyoandika.

Oyaa,

Baada ya ile debate kati yangu nawe kwenye suala la Mtikila na maneno yote uliyotoa, ilibidi nichukue muda wa kutosha kukusoma ili nijue na-debate na mtu wa aina gani. So far nina very good picture of you kutokana na nilichosoma.

CN, inatumika kwenye mining hasa kwenye kusafisha Gold. Hili lipo wazi, tatizo ni kuonyesha data za kuthibitisha kuwa inamwagwa kwenye mito bila kufanyiwa usafishaji (treatment) yoyote. Nafikiri hizi ndio data zinazotakiwa kuonyesha malalamiko yako.

Yaani ndicho kinachofanyika - na ndicho baadhi ya watu waliojaribu kuuliza hili kule Nyamongo "walipatikana na hatia ya kuwa mgodini bila kibali". Ambacho bado sijakupata vizuri ni - unataka picha za matukio au unataka kujua kiasi kilichomwagwa? au unataka kujua siku ngapi kwa wiki inamwagwa, au data unazotaka hapa ni zipi hasa?

Asante
 

Tossi warns troublemakers in Tarime​
MUGINI JACOB in Tarime
Daily News; Tuesday,September 23, 2008 @20:06



AT least two motor vehicles have been damaged and one person seriously wounded in violence connected with the on-going by-election campaigns in Tarime constituency, Deputy Commissioner of Police Venance Tossi said here yesterday.

According to Mr Tossi, one of the cars belongs to Rorya Legislator, Prof Philemon Sarungi and the other is the property of the Tarime District CCM Chairman, Mr Simon Mseti.

He said three people have been arrested and taken to court in connection with the incident that took place during a CCM campaign rally on Monday.

He named them as Mwita Nchagwa (28), Nyangoye Chacha (33) and Chacha Muniko (29), all residents of Tarime township.

Mr Tossi also named a CCM member who had been seriously injured on the head with a stone thrown by unidentified person as Ruben Marwa (45) of Nyamisangura in Tarime town.

He said Nyamisangura was rushed to the Tarime District Hospital alongside another CCM cadre, Emmanuel Zungu, who was splashed on the face with water believed to contain hot pepper.

CCM Vice-Chairman (Mainland), Mr Mr Piusi Msekwa and the party's Secretary General, Lt Yusuff Makamba, condemned the violence which was brought to an end by anti-riot police .

"We have arrested the prime suspect in the incident," he said and mentioned him as Jumanne Maranja Masese(46).

He also refuted media reports that police have been using excessive power to disperse supporters of the major competing political parties (CHADEMA and CCM).

"We will be forced to do so if violent incidents persist," he said.

He also warned CHADEMA supporters against involving children under 10 years of age in their illegal demonstrations.
 

Poti
Unafanya makosa
kujadili topic kwa kumpiga mtu picha wewe jadili kilichoandikwa wala usijaribu kumtafsri huyu mtu ni wa namna gani.

Na kila unapomkuta mliye pingana kihoja ktk thread fulani wewe jaribu ku assume tu huyu ni mpya kwanza leo hapa ndio naona hoja yake kwa mara ya kwanza .


Ni hatari na nusu to work with past experience

Ni maoni yangu tu.
 

Nimekuelewa poti,

Ila kumbuka kuwa mtu ambaye hajui anakotoka au aliko, inakuwa kazi kweli kujua anakokwenda. Katika hili nimejaribu kujiweka kwenye nafasi ya kujua ninakotoka na niliko kuhusiana na mwenzangu hapa. Ukiona mtu (hata ikiwa mimi) anashupalia sana jambo hapa, inakuwa vyema kusoma maandishi yake mengine ili kujua mwelekeo wa fikra zake.

Hiyo inasaidia kujua kama uendelee kujadili na mtu au uachane na maneno yake. Vinginevyo, nimechukua ushauri wako vizuri.
 
Mhh!, CCM kweli kusimamisha mtu huwa hawaangalii. Huyu bwana anayegombea udiwani sijui ndani ya vikao itakuwa vipi. Ninamvyomjua ugomvi wake Bastola mkononi, mabishano madogo tu huwa anakuwa mkali vibaya mno. Lakini hilo CCM hawaangalii, mradi ana mali na ni mfanya biashara mkubwa pale Tarime. Kuanzia vituo vya mafuta Tarime mpaka Shirati. Bila kusahau mabasi. CCM na wafabiashara, inanikumbusha kauli ya Mkulu mmoja aliposema ukitaka biashara zako zinyooke kuwa CCM.

Kazi tunayo!
 
[Source Tanzania Daima]


Vijana 30 wa CHADEMA waswekwa ndani


na Mwandishi Wetu, Tarime


ZAIDI ya vijana 30 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wamekamatwa na polisi wilayani Tarime kwa kile kilichodaiwa kuwa ni operesheni kamata wazembe na wazururaji.

Operesheni hiyo ilianza jana asubuhi ambapo askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), walimwagwa katika mitaa yote ya mji mdogo wa Tarime, hususan katika vijiwe maarufu vya wafuasi wa CHADEMA.

Vijana hao ambao hadi sasa bado wapo ndani, walifikishwa katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Tarime ambapo Mkuu wa Kituo hicho (OCD), aliwataka viongozi wa chama hicho waliokuwa wakiwafutilia vijana hao, kuacha kumwingilia katika kazi zake.

Akizungumza katika mikutano mitatu ya kampeni katika vijiji vya Mrito, Karende na Kewanja, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema kitendo cha Serikali kumwaga polisi wengi katika jimbo hilo, kinawatisha wananchi.

Dk. Slaa ambaye alikuwa akimnadi mgombea wa CHADEMA, Charles Nyanguru, alilalamikia kauli za Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa na Katibu Mkuu, Yusuph Makamba, kwamba wametumwa na Rais Kikwete, kuangalia hali ya vurugu ili wamjulishe rais.

"Kauli hiyo ni ya vitisho na kamwe hapaswi kutolewa na viongozi hao. Tunasema serikali ndiyo inayojenga mazingira ya hofu katika uchaguzi huu, wakati wananchi hawana mpango wa kuanzisha vurugu," alisema.

Dk. Slaa alisema katika mkutano huo kuwa ana ushahidi wa kikao cha Makamba cha Septemba 19 kwamba Jimbo la Tarime liwe mikononi mwa CCM kwani wana pesa na polisi, hivyo hawana sababu ya kushindwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, ndiyo maana polisi mjini hapo, wamekuwa wakitekeleza maagizo ya CCM ya kuwakamata vijana wanaoonyesha alama ya vidole viwili, inayotumiwa na CHADEMA.

Dk. Slaa alisema serikali inataka kulifanya Jimbo la Tarime kama visiwa vya Zanzibar katika uchaguzi kwani matokeo wanayoyafanya, yanaonyesha ni jinsi gani wanataka kuleta vurugu.

Katika mkutano huo, Dk. Slaa, alimlaumu Rais Kikwete kuwa amekuwa bingwa wa kusuluhisha matatizo ya nchi jirani kama vile Kenya na Zimbabwe wakati Zanzibar ikibaki katika uhasama na sasa hali hiyo inataka kupandikizwa Tarime.

Aliwataka wananchi hao kuacha kumpigia kura mgombea wa CCM kwani hataweza kuwaletea maendeleo na badala yake wamchague mgombea wa CHADEMA ili kumalizia kazi iliyoachwa na marehemu Chacha Wangwe.

Naye mgombea CHADEMA, Nyanguru, aliwaahidi kuwatetea vijana, hasa katika operesheni za aina hiyo ambazo alisema ni za kinyanyasaji.

Uchaguzi katika jimbo hilo utafanyika Oktoba 12.
 
mchemko mwingine wa viongozi wa CCM. kwa mtindo huu tutafika?

Makamu mwenyekiti CCM aomba nguvu ya dola kudhibiti upinzani


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Pius Msekwa, amesema atawasiliana na Rais Jakaya Kikwete ili amwagize Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Mstaafu Isaac Machibya, aruhusu nguvu zaidi ya dola itumike kuwadhibiti wanachama wa Chama cha Demokrasia (Chadema), aliyodai kuwa wanafanya fujo.

Akizungumza jana wakati wa kumnadi mgombe udiwani wa CCM Tarime mjini, Peter Zacharia, Msekwa, alisema atamweleza Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM amwamuru Kanali Machibya awaamuru polisi kutumia nguvu ya ziada katika kubilina na hali hiyo wakati huu wa kampeni za kuwania kiti cha ubunge wa Tarime.

"Wanatufanyia fujo, jana mfuasi wetu, Rubeni Marwa, alijeruhiwa kwa mawe na amekatika kidole na mwingine, Omari Nzungu, leo hii amemwagiwa pilipili machoni. Sasa hizi ni vurugu hatuwezi kuendela kuvumilia, nitamwambia Rais leo hii, hivyo yatakayo tokea shauri yenu," alisema Msekwa wakati akihutubia mkutano huo wa kampeni.

Hata hivyo wachunguzi wa masuala ya siasa ambao wamezungumza na gazeti hili baada ya kauli hiyo ya Msekwa, walionya kuwa kama Rais atapokea taarifa hiyo na kuamuru Jeshi la Polisi kutumia nguvu, hali ya usalama Tarime inaweza kuchafuka zaidi.

Walisema eneo hilo linaweza kugeuka uwanja wa vita kutokana na msimamo wa wananchi wa wilaya Tarime ambao wamekuwa wakiishi kwa mapigano ya koo kwa kwa muda mrefu.

Dalili za kuwapo kwa vurugu, zilianza kuonekana tangu kuanza kwa kampeni hizo na hasa baada ya kuwasili kwa viongozi wa ngazi za juu wa CCM ambao walipkewa kwa kuzomewa wakati wanaingia mjini Tarime.

Hata hivyo vurugu ziliibuka zaidi mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya wafuasi wa Chadema kukerwa na vitendo vya viongozi wa CCM kuwakikejeli chma chao kwa kukiita kuwa ni cha watu wawili.

Hata hivyo, juzi jioni wakati wa mkutano wa kampeni wa CCM ambapo kada mmoja wa chama hicho, alimwagiwa pilipili na kijana ambaye anayedaiwa kuwa mfuasi wa chadema, kulisababishwa na viongozi wa CCM kuanza kuishambulia chadema kwa maneno hivyo kuamsha hasira za wananchi hao ambao walianza kuzomea.

Vurugu zilizuka baada ya askari polisi kumshika kijana huyo na kutak kumpeleka kituoni ndipo wafuasi Chadema waliwasonga wakiwataka wamwachie mwenzo huku wakirusha mawe mpaka alipoachiwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CCM, Luteni Yusuph Makamba, aliwataka wananchi hao kutomchagua mgombea wa Chadema, kwa madai kuwa chama hicho hakina bajeti ya kuendeshea nchi, hivyo hawatapata maendeleo haraka.

Tangu kuanza kwa kampeni huizo kumekuwapo msuguano mkali kati ya wafuasi wa CCM na Chadema.


source: Mwananchi
 
Hivi Mbowe, mwenyekiti wa CHADEMA ameenda Tarime kwenye kampeni?
 
Mbona mwandishi hakumuuliza huyo bosi wa polisi kwa nini anawakamata chadema tu?
 
TARIME ipewe KENYA

Kwa fujo na rabsha zinazoendelea huko TArime mimi ninashauri kwamba Waziri Mkuu wa Kenya. Mheshimiwa sana Raila Omolo Odinga atapokuwa hapa Tanzania apewe zawadi ya aina yake: nayo sio nyingine ila wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Baada ya Tarime kuwa sehemu ya Nyanza tutaondokana na fujo za Waancholi na Wanchokaa milele na milele. Amin!

Mwanakijiji, Nyoronyoro Kichechere na kina Mobhare na wazawa wenzangu mwasemaje juu ya hili! Yaani tulivyo na akili baada ya miaka michache tu sisi ndio tutakao warithi Wakikuyu na Wajaluo kama watawala wapya wa Kenya. Baada ya hapo tunarudi tena kuungana na Tanganyika!
 
Hata JK (CCM), Lipumba (CUF), Mbati (NCCR) nk hawajaenda! Au hao si muhimu?
 
Mheshimwa mbunge kama tutasuruhisha jamii zinazogombana kwa kuzigawa (disown) mwisho wa s iku tutabaki na nchi kweli?

Swali dogo tu kwako kwa mfano wakulima na wafugaji wa morogoro wakianza kupigana tutawagawa kwa nchi gani? Maana hawa wa tarime umewagawa kwa nchi wanayopakana nayo, hawa wa morogoro tutumie kigezo gani?
 
Hata JK (CCM), Lipumba (CUF), Mbati (NCCR) nk hawajaenda! Au hao si muhimu?

Nijuavyo mimi sio kawaida kwa rais kwenda ku kampeni kwenye chaguzi ndogo. Ninategemea kiongozi wa upinzani aende labda kuwe na sababu kubwa sana.

Pia Mbowe nilisoma hapa kwamba anapendwa sana Tarime, sasa kwa mtu anayependwa si ndiye anafaa kwenda kuongoza kampeni?

Hakuwepo wakati wa mazishi ya Wangwe, asipoenda kwenye kampeni, huhitaji kuwa genius kujua maana yake.

Kuna sehemu nilisoma kama Mbatia emeenda au anaenda. Sina taarifa kuhusu Lipumba, je CUF pia wameweka mgombea wao?
 
ha-ha-ha-hah!
Makamba sijui tumfananishe na nani.



.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…