Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.

MMJJ,
Mazingira ya hizi chaguzi ni tofauti kabisaa kulinganisha. Sidhani kama Kiteto kuna aliyechomwa kisu kwa kupigania uwanja wa kutulia Helikopta. Ukosefu wa amani Tarime ni wazi kuwa ndio uliowafanya zaidi ya 50% ya wapiga kura kuogopa kutoka nje siku ya uchaguzi. Analysis yoyote inatakiwa ianzie hapa.
 
Kama ni kweli CHADEMA mmeshinda, basi 'hongereni zenu'.

CCM tulishasema kuwa tutakubali matokeo.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi

Kidumu Chama Tawala



Asante sana mkuu kwa kuonesha ukomavu kisiasa.Kukubali matokeo ndio uungwana.Nakusihi fanya kazi ya kuelimisha wenzio nao waelewe.At least tunaanza kuona Demokrasia.Bravo CHADEMA.
 

Every Dog Has Its Day!
 
Currently Active Users: 1,403 (222 members and 1181 guests)
Most users ever online was 1,565, 12th February 2008 at 07:03 PM.


Hivi kulikuwa na tukio gani siku hiyo? The record will be broken today before it reaches 7 PM this evening!



.
 
Nafikiria kuhusu ule muungano wa upinzani.......
Ni kwamba CHADEMA wameishinda Sisiem iliyokua pamoja na baadhi ya wapinzani!
Tafadhali kaeni muongelee uzoefu mlipata Tarime, labda mtapata muungano bora kuliko wa sasa (au ulikuwepo?).
 

Sidhani kama CCM waliweza kununua shahada 20,000 bila ya CHADEMA n.k. kutokupata habari. Hivyo vitisho vya watu kwenda kuchukua silaha zao na kuingia mitaani, ni lazima ziliwafanya wasio wakereketwa wa CHADEMA na CCM kukaa nyumbani.

Despite winning, CHADEMA have to be worried of 10% decrease in support. Kama upungufu huo ungetokea kwenye jimbo lingine lolote waliloshinda ubunge 2005, basi wangepoteza hivyo viti.
 

Kwa jinsi CCM ilivyo na mtandao mkubwa mpaka kwenye nyumba kumi kumi kama ni suala la kununua shahada kwa ni jambo rahisi sana, kwa sababu mjumbe wa nyumba kumi almost atakuwa anawajuwa watu wa maeneo yake vizuri sana, yupi mwenye shida, yupi ana njaa sana au watu gani tuwatumie kwa urahisi kufanikisha zoezi etc ...

Pamoja na yote hayo lakini inabidi vyama vianze(hasa CHADEMA) kufanya kazi kisayansi sasa kwa kufanya tathmini baada ya uchaguzi kama huu wa Tarime wajue kabisa bila shaka ni sababu gani imesababisha turnout kuwa ndogo. Wanaweza kutumia hata questionnaires kujua hilo, na ni kwa ajili ya manufaa yao ya baadaye.
 

Nakubaliana na wewe kabisa kuwa mtandao wa CCM ni mkubwa na kabambe hata kwenye jimbo kama la Tarime lililokuwa chini ya umiliki wa CHADEMA.

Lakini, let's be fair, kununua shahada 20,000 bila kugundulika sio jambo rahisi. Ila la wazi na lililoandikwa na wanaCHADEMA wengi waliokuwa Tarime humu JF, ni vitisho vya utumiaji wa silaha kwa baadhi ya wakereketwa. Sina shaka kabisa kuwa wale wote ambao sio wakereketwa wa hivi vyama hawakuona umuhimu wa kushiriki uchaguzi kwa vitisho vya usalama vilivyokuwepo.
 

Ifikapo saa 6 usiku leo idadi ya waingiaji JF inaweza kuvunja rekodi. A good work WaTZ tuendelee kuingia na kuchungulia.
 
CHADEMA wamepambana kiume Tarime na wanastahili sifa.
 
HONGERA CHADEMA, NATAMANI 2010 IWE KESHO VILE, MAANA NINA KIMUKEMUKE! ccm GO TO HELL!!!!
 

Hata mimi sidhani kama sababu inaweza kuwa moja, ndio maana nasema ni vizuri watu wakatumia njia za kisayansi kujifunza nini kimekuwa chanzo....Kukosekana kwa watu zaidi ya 20,000 najua sababu zitakuwa nyingi tu....wagonjwa, ununuzi wa shahada, vitisho, kukosekana majina vituoni, kuhamishwa vituo bila taarifa, wengine kupigia kura upinzani, low motivation na kadhalika...
 
...pwaa...pwwaa... eeh kidedea........pwaa...pwwaa... eeh kidedea........pwaa...pwwaa... eeh kidedea.....
 

mhh mhh

haya mwaya....
 
Bi. Mdogo kama hili lisingekutoa kwenye fungate unajua ningekuja mwenyewe nikutoe huko kwa nguvu.. it is good to see you here again at such a moment like this. Weekend kwetu kwa nyama choma na cha kugigida kidogo.
 
Bi. Mdogo kama hili lisingekutoa kwenye fungate unajua ningekuja mwenyewe nikutoe huko kwa nguvu.. it is good to see you here again at such a moment like this. Weekend kwetu kwa nyama choma na cha kugigida kidogo.

Hili ni la uchaguzi wa Tarime ni kubwa zaidi kuliko chochote kile mwaya. Kama hili lisingenitoa huko basi hakuna tena lingine lolote ambalo lingeweza. Leo ni siku ya furaha sana kwangu. I am so happy that nafikiria kuruka angani na kupaa mpaka golden gate bridge na kufanya makelele makubwa sana ili wote wa San Francisco mpaka Manhattan NY wanisikie.

Asante sana Mkjj, ninapanga kuja huko weekend, nitatengeza sambusa za nyanya na vitunguu saumu - no meat please!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…