Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Nyaronyo Kicheere, yule mhariri wa Kulikoni, leo amenyaka fomu ya kugombea ubunge wa Tarime kupitia Chadema. Ajabu, kumbe wanajifucha uanachama wao mpaka dakika ya mwisho ndio wanajionyesha!
 
Kama ubunge ndio namna hiyo basi hakuna maana yoyote

Nina mfahamu vizuri sana kijana huyu, kwani kabla ya kuwa President alikuwa mwenyekiti wa Faculty ya Sayansi pale UDSM ambayo hata mie nilikuwa member wake, akafanya brunda kibao na mauza uza ya ajabu na hata facult yenyewe ilimshinda

Ilipofika wakati wa uchaguzi wa President, kama kawaida yao, kwa sababu alishaonyesha kulinda maslahi ya CCM na wakuu toka akiwa kama mwenyekiti wa facult, Vice cancelor wakampitisha na sijui alipata wapi pesa akawanunua wanachuo kwa pombe na mziki wa usiku (wasomi hawa jamani) akashinda

Lakini mambo yalikuwa ovyo sana wakati wa uomgozi wake, na mbaya zaidi ni kwamba aliwageuka wanachuo na akaanza kutumikia management zaidi badala ya wanachuo na migomo ikaanza

The guy is pretending to be smart, but 100% he is nothing in leadership.
 
ni kweli kabisa jamaa ni opportunist ile mbaya. kabla ya kuingia CCM alikuwa kada wa NCCR mageuzi. kipindi hicho akiwa karibu kabisa na BAHATI TWEVE ambaye alie 'mbeba' mpaka kupata uraisi wa DARUSO. jamaa hakuwa na ubavu wa kuupata uraisi bila support ya TWEVE. vilevile aligombea na mtu ambaye alikuwa very unpopular kwa kukubali kupandaish rent ya makazi na kusapport cost sharing. TWEVE mpaka sasa anacheo flani ndani ya NCCR.
huyu Mwita alisha wahi kukana saini yake juu ya kupinga opinion poll ya REDET kuwa JK anapendwa. alipo pigwa mkwara akaikana saini yake. toka hapo CCM walimwinda na kumfanya kada wao. toka hapo akawa anafanya kazi za kugawa tisheti za JK kwa wanachuo. nasikia alikuwa anakula pesa nzuri kwa kazi ya kupeleka wanachuo kwenye mikutano ya CCM wakati wa kampeni.

pia amekula pesa nyingi tu kwa kujidai kuwa yeye ni mtaalamu wa kutuliza migomo ya chuo.

We jiulize jamaa ni mwalimu wa hesabu na sayansi masomo yenye uhaba mkubwa wa waalimu nchini kwa nini hakuona hakuona umuhimu wa kutumia taaluma hiyo toka alipo maliza chuo 2006?

kwa nini aliona aende kuwa kwanza kibaraka then katibu wa vijana kabla ya kupeleka taaluma yake mashuleni where it is critically needed?

kwa kifupi jamaa sio wakumwamini kabisaaaaaaaa! labda CCM na maajabu yao wanaweza kumpa dhamana kiumbe kama huyo
 
Kwanza hoja zke za kitoto sana.Yaani mwalimu mzima anashindwa kueleza matatizo yaliyoko Tarime? Huyu naona hawezi kumfikia Chacha Wangwe hata robo
 
Other people bwana!

Lakini anauzika huko Tarime? Nimewahi kumwona mara mbili hivi akihojiwa kwenye luninga. Anaonekana ana uchungu na nchi yake.

Uchungu na nchi hauwezi kuthibitika kwa kuongea bali kwa kutenda. Many can talk the talk but only few are capable of walking the walk.
 
Heshima Mbele,

Harakati za uchaguzi wa Jimbo la Tarime umeanza kwa mwebwe nyingi na kwa watu kadhaa wa CHADEMA kuchukua fomu,Leo kulikuwa na kikao cha kupitia majina ya walioomba kugombea jimbo aliloliacha Mhe. wangwe.

Mgombea mmoja maarufu kwa jina la chacha tayari ameshajinadi kuwa ana uwezo mkubwa zaidi ya ule aliokuwa nao wangwe kw akujitapa anaweza kuvivaa.Haya maneno yaliwa kuzungumwa na Zitto kuwa marehemu chcha wabngwe hakuacha pigo katika CHADEMA.

JF imekuwa Mstari wa Mbele sana kutetea maslahi ya nchi na kuweka mbele U-CHADEMA zaidi kuliko kitu kingine,Je kwa mbinu hizi za CHADEMA watafanikiwa kulichukua Jimbo la Tarime?ikizingatiwa na maneno yao ya kumuona wangwe hakuwa na umuhimu katika CHADEMA.

Anguko la pili la upinzani linakuja na hii yote imechangiwa na kupuuzwa kwa yale aliyoyasema marehemu wangwe.Pili yamechangiwa na muungano wa upinzani kuvunjika baada ya CHADEMa kujiona wao ni bora zaidi.

CHADEMA hawataki kuyatekeleza yale mazuri aliyoyaacha na mpaka sasa sijasikia tamko lolote la kuhusu matumizi ya pesa za CHADEMA zaidi ya kukanusha bila kutoa fact.

ukiangalia kwa undani kabisa basi CCM walishashinda jimbo hilo kwa kuwa CHADEMA na NCCR amabo wao wataweka mgombea mmoja wakishilikiana na vyama vya CUF na TLP watagawa kura za upinzani wakati CCM wakivuna kura za ushindi..

Mbio zimeanza je ni CHAMa kipi kitashinda?
 
Mpaka kieleweke,

unaweza kutupa kilichojiri Tarime kwa leo?
 
Maneno yapi hayo? Nadhani Itakuwa vizuri ukiyanukuu ili tujue tunaongelea maneno yapi haswa na yalisemwa na nani. Je ni tamko rasmi kutoka CHADEMA? Tusije tukajadili mada nzuri kama hii kwa maneno yasiyokuwepo

Maana kuna tofauti kubwa, tena sana kati ya kuzibika kwa pengo lililoachwa na aliyetangulia na huyo aliyetangulia kutokuwa na umuhimu.
 
Sauli Giliard

“NINA ndoto ya kuikomboa Wilaya ya Tarime. Naamini anahitajika mtu makini, jasiri na asiyeogopa katika kutetea ukweli ili kuibadilisha Tarime. Nimejipima na kuridhika kuwa mtu kwa wakati huu ni mimi.

“Elimu niliyo nayo kuhusu uchumi, biashara na fedha ni silaha ya kutosha ya kuwapigania Wanatarime ili maisha yao yafanane na wananchi wengine hapa nchini, kwani kiuchumi bado tuko nyuma sana”.

“…Naamini naweza kushiriki kuikomboa jamii yangu kwani ipo nyuma. Ni kama vile imetengwa, Chacha Wangwe alianza, sasa hayupo, anahitajika mtu wa aina yake na pengine zaidi yake kuendeleza yale aliyoyaanzisha. Mimi ndiye mtu huyo. Naweza kuongoza jahazi hili kuwakomboa Wanatarime”.

Hiyo ni kauli nzito ya Esther Matiko, mwanasiasa kijana na mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Dar er Salaam, aliyejitosa kuwania ubunge wa Tarime kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), nafasi iliyoachwa wazi na Wangwe, aliyefariki dunia mwezi uliopita kwa ajali ya gari.

Katika mahojiano na gazeti hili, Matiko, ambaye wakati wote alikuwa akizungumza kwa umakini wa hali ya juu huku akionekana kuchagua zaidi maneno ya kuzungumza, anasema iwapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Tarime, atakuwa tayari kupambana na lolote kukabiliana na kero za wananchi.

Atawatetea wananchi wa Tarime dhidi ya dhuluma ikiwamo kunyang’anywa maliasili zao. Nia yake ni kuhakikisha kuwa Wanatarime wanarejeshewa utu wao unaopotea kwa kukosa uhuru wa kunyang’anywa ardhi waliyoachiwa na babu zao.

Matiko, mwanadada pekee miongoni mwa wagombea wengine kupitia CHADEMA, alieleza kuwa ameamua kuingia katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu anaamini wanawake nao wanaweza kugombea nafasi za uongozi na kuwashinda wanaume.

“Nina moto wa kuleta mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Jimbo la Tarime kupitia CHADEMA. Naamini nitaweza kwa sababu Wangwe ameacha msingi mzuri, nitaanzia hapo.

“Tarime pamoja na kuwa na madini yenye thamani, haijafanikiwa kujikwamua katika lindi la umaskini, hii ni changamoto yangu ya kwanza nikiwafanikiwa kuwa mbunge nitakakopigana kuhahakisha kuwa madini yaliyopo Tarime yatumika ipasavyo na kuwasaidia Wanatarime kujikwamua katika umaskini unaowaandama.

“Ubovu wa miundombinu, hasa barabara ni jambo jingine linaloniumiza kichwa, natamani kuona barabara za Tarime zinapitika kaktika kipindi chote cha mwaka.

“Hili litakuwa jambo jingine ambalo nitalipa kipaumbele iwapo CHADEMA itanipa ridhaa ya kuwa mgombea wake kwa sababu nina hakika nikiteuliwa, wapiga kura wa Tarime hawataniangusha, watanichagua. Ninaamini hivyo.

“Lipo pia suala la elimu, ninaifahamu Tarime ni kwetu, kodi za Wanatarime zimenisomesha na ndiyo maana ninataka kuwalipa kwa kuwatumikia kama mbunge wao. Sikubaliani na hali ilivyo katika ufundishaji katika shule za msingi na sekondari jimboni Tarime.

“Shule inakuwa na walimu wachache…hizo shule za kata na wananchi, wasichana wanakatizwa masomo kutokana na vishawishi vya aina mbalimbali,” anasisitiza.

Hakubaliani na hali ilivyo kwa wananchi wa Tarime alioeleza kuwa wanakosa uhuru wa kutembea wakiwa ndani ya ardhi waliyozaliwa, kisa kutukuza wawekezaji.

Anaeleza zaidi kuwa kodi zisizo na msingi na kilimo kisicho na tija, kwake ni changamoto ambazo amejiandaa kukabiliana nazo hadi ‘kieleweke’.

Anakiri kuwapo kwa mabadiliko ya hali ya maisha kwa wananchi wa Tarime, hasa kupitia CHADEMA kuanzisha mpango wa kuwalipia wanafunzi wote wanaofanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari. Anaamini utawasaidia watoto wengi wa Tarime kuwapata elimu waliyokuwa wakiikosa kwa muda mrefu.

Mjue Esther Matiko

Esther Matiko alizaliwa Novemba 1976 katika Kijiji cha Nyabirongo, wilayani Tarime, akiwa mmoja wa watoto wanne wa familia ya mzee Nicholas Matiko.

Alisoma na kuhitimu elimu ya msingi katika Shule ya Kiongera kati ya mwaka 1985 na 1991. Mwaka 1992 hadi 1995 alisoma elimu ya sekondari Msalato, Dodoma.

Baadaye alisoma elimu ya juu ya sekondari kati ya mwaka 1996 na 1998 katika Shule ya Wasichana Nganza mkoani Mwanza.

Alifaulu vizuri masomo ya sayansi (Fizikia, Kemia na Baiolojia). Mwaka 1999 alichaguliwa kujiunga na Chuo Cha Kilimo cha Sokoine kuchukua shahada kwanza ya Sayansi katika fani ya Maarifa ya Nyumbani na Lishe, alihitimu mwaka 2002.

Mwaka 2003 hadi 2005 alijiunga Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosoma shahada ya Uzamili katika fani ya uongozi wa biashara akiegemea zaidi kwenye masuala ya fedha na kuhitimu mwaka 2005.

Baada ya kuhitimu, alibaki chuoni hapo katika kitengo hicho kama mhadhiri msaidizi, kazi anayoifanya hadi sasa.

Pamoja na umri mdogo alio nao, Matiko amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi - uenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake ya Kuondoa Umaskini (TWAAP).

Alijiunga na CHADEMA mwaka 1992 akiwa mwanafunzi na kwa maneno yake mwenyewe, tangu akiwa shule ya sekondari alikuwa karibu na Wangwe kutokana na wote kuwa wakereketwa katika masuala ya siasa.

“Nakumbuka wakati wazazi wangu wakinifanyia sherehe ya kunipongeza kujiunga na Chuo Kikuu cha Sokoine, Wangwe alikuwapo na aliniusia mambo mengi…harakati zake za kupigania haki kwa Wanatarime ziliniweka karibu naye sana nami niliamini iko siku nitapata nafasi ya kuwa mwanasiasa”.

Katika uchaguzi mkuu uliopita, Matiko aligombea ubunge kwa viti maalumu kupitia CHADEMA bila mafanikio. Hata hivyo, jambo hilo halikumkatisha tamaa kwa kile alichoeleza kuwa aliamini anao muda na nafasi ya kuwa kiongozi kutokana na umri wake.
 
Heshima Mbele,

Harakati za uchaguzi wa Jimbo la Tarime umeanza kwa mwebwe nyingi na kwa watu kadhaa wa CHADEMA kuchukua fomu,Leo kulikuwa na kikao cha kupitia majina ya walioomba kugombea jimbo aliloliacha Mhe. wangwe.

Mgombea mmoja maarufu kwa jina la chacha tayari ameshajinadi kuwa ana uwezo mkubwa zaidi ya ule aliokuwa nao wangwe kw akujitapa anaweza kuvivaa.Haya maneno yaliwa kuzungumwa na Zitto kuwa marehemu chcha wabngwe hakuacha pigo katika CHADEMA.

JF imekuwa Mstari wa Mbele sana kutetea maslahi ya nchi na kuweka mbele U-CHADEMA zaidi kuliko kitu kingine,Je kwa mbinu hizi za CHADEMA watafanikiwa kulichukua Jimbo la Tarime?ikizingatiwa na maneno yao ya kumuona wangwe hakuwa na umuhimu katika CHADEMA.

Anguko la pili la upinzani linakuja na hii yote imechangiwa na kupuuzwa kwa yale aliyoyasema marehemu wangwe.Pili yamechangiwa na muungano wa upinzani kuvunjika baada ya CHADEMa kujiona wao ni bora zaidi.

CHADEMA hawataki kuyatekeleza yale mazuri aliyoyaacha na mpaka sasa sijasikia tamko lolote la kuhusu matumizi ya pesa za CHADEMA zaidi ya kukanusha bila kutoa fact.

ukiangalia kwa undani kabisa basi CCM walishashinda jimbo hilo kwa kuwa CHADEMA na NCCR amabo wao wataweka mgombea mmoja wakishilikiana na vyama vya CUF na TLP watagawa kura za upinzani wakati CCM wakivuna kura za ushindi..
Mbio zimeanza je ni CHAMa kipi kitashinda?

Urafiki huu wa mashaka wa Wapinzani ni turufu muhimu kwa CCM and the winner is CCMMMMM!
 
Chama cha NCCR-Mageuzi juzi kilionja joto la kusaka ubunge wa Jimbo la Tarime, baada ya kukumbana na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hasa vijana na kupigwa mawe katika mkutano uliohutubiwa na Mkurugenzi wake wa Katiba na Sheria, Dk. Sengodo Mvungi.

Kundi hilo lilivamia mkutano huo uliokuwa ukifanyika katika kiwanja cha mpira cha Sabasaba mjini Tarime na kuitaka NCCR-Mageuzi kutowaingilia katika jimbo hilo walilodai kuwa ni miliki yao huku wakidai chama hicho cha upinzani kimetumwa na Chama Cha Mapinduzi kuwagawanya wapinzani.

Tafrani ilianza baada ya wazee wakiwakilishwa na Grigory Nyanchini, kuwaeleza wananchi waliohudhuria mkutanoni hapo kuwa mtu katika upinzani ambaye ana sifa za kurithi mikoba ya marehemu Chacha Wangwe, kutokana na msimamo wake wa kutetea jamii kuwa ni Enock Haruni maarufu kama Macho ambaye ni mgombea pekee aliyepitishwa na NCCR-Mageuzi.

Baada ya kauli hyo, makundi ya vijana yalianza kupiga kelele yakisema jimbo hilo ni la Chadema, huku baadhi yao wakikusanya bendera za CCM zilizokuwa zimesimikwa sehemu mbalimbali za kazi za maduka ya biashara wakati Dk. Mvungi akihutubia.

Hali ilizidi kuwa mbaya walipouliza maswali kadhaa likiwamo la kwamba wakati marehemu Wangwe akiwa NCCR, alifungwa na Chadema walimtuma wakili Tundu Lissu akamtoa na kwamba wanasema walikuwa wakimpenda huku hawakumshughulikia na pia wakahoji juu ya ushirikiano wa vyama vya upinzani kama bado upo huku wakisema inatakiwa Chadema iungwe mkono.

Katika majibu yake, Dk. Mvungi aliyepigwa mawe pamoja na viongozi wengine waliokuwa jukwaani, aliwaambia kuwa chama ambacho hakikumpenda Wangwe ni Chadema kutokana na kumsimamisha Umakamu Mwenyekiti, huku akidai kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwahi kutamka kuwa ni bora kupoteza jimbo kuliko kukaa meza moja na Wangwe.

Alisema NCCR haikumtimua au kumvua uanachama wakati alipokuwa Diwani wa Tarime Mjini huku akiwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mara na kuwaambia kuwa hakuna chama chenye hatimiliki katika jimbo hilo. Aliwataka wawe wanyenyekevu hadi wakuu wa vyama watakapokaa na kuona ni nani anayekubalika ili wamuunge baada ya mchakato wa kura za maoni.

Majibu hayo yalionyesha kutowaridhisha na kumtaka ashuke kutoka jukwaani, huku wakisisitiza kuwa tofauti na Chadema, hakuna chama kitakachoukwaa ubunge huo huku wakimwonyesha picha ya mmoja wa watu 10 waliochukua fomu kugombea kupitia Chadema waliyedai kumtaka na ghafla, walianza kupiga mayowe na kuwatupia mawe na kutawanya mkutano huo.

Akizungumza baada ya kupigwa mawe, Dk. Mvungi alilaani kitendo hicho cha mkutano wao kuvurugwa na Chadema na kuwaeleza kuwa siyo wastaarabu, akisema nguvu haiwezi kutumika kutwaa jimbo hilo. Alisema walichoonyesha Chadema ni uhuni kwa wafuasi wake kuvamia mikutano ya vyama vingine vilivyopo kwa mujibu wa sheria kikiwamo CHAUSTA ambacho siku nne zilizopita, mgombea wake, Hellena Steven alishushwa jukwaani na gari lake kunusurika kuchomwa moto wakati akijinadi hapo.

Alitupia lawama Polisi kwa kutoweka ulinzi katika mikutano ya vyama vya upinzani licha ya kuwa walitoa taarifa ya kuwapo mkutano, kitendo ambacho kinatoa mwanya kwa watu aliodai walevi na wavuta bangi, kuwavuruga na kuhatarisha maisha ya viongozi wa vyama hivyo pamoja na raia wema.

Kwa upande wake, Katibu wa Chadema Wilaya ya Tarime, Anthony Joseph aliwataka wanachama wake kuacha tabia ya kuvamia na kuwapiga watu sambamba na kuvuruga mikutano hata ya wenzao akisema kuwa kwa kitendo hicho ni kuwafanya watu waamini kuwa Chadema ni chama cha kigaidi.

Alisema hawawezi kuishi kwa kutafuta uwakilishi kwa kufanya fujo za kuwazuia wanasiasa kufanya kazi zao kwa vile kila mtu anayo haki ya kuamua kile anachoona kinafaa na siyo kulazimishwa kufuata matakwa ya mwingine katika siasa ya demokrasia. Aliahidi kulishughulikia suala hilo. Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime utafanyika Oktoba 12, mwaka huu, kujaza nafasi ya Wangwe wa Chadema aliyefariki dunia usiku wa Julai 28, mwaka huu, eneo la Pandambili Kongwa mkoani Dodoma. Uteuzi wa wagombea utafanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Septemba 13, mwaka huu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom