Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
...Tarime hatuoni vurugu wala kufukuzana badala yake kuona polisi wamevalia kijeshi muda wote na kuranda mitaani ? kuna vurugu ipi hapa kwa muda huu na imeanza lini ?

Njia ya mwongo ni fupi..
 
Salaam tokea Tarime .Mambo si shwari na CCM sasa wameamua kufanya yale yaliyo tegemewa .Nimeshuhudia Tossi leo na kikao kikubwa hapa Tarime na Kova anategemea kutinga muda wowote ili kuhakikisha CCM wanapata jimbo hili .................

Jeshi la Polisi linafanya kufuru sasa maana leo pekee wameletwa 300 na wiki hii wanategemea wengine 600 zaidi kwa jina la vurugu za kikabila lakini ukweli ni kwamba jimbo la Tarime lirudi CCM ndiyo nia yao.

Yale yale ya Zanzibar. Sijui safari hii wataua wangapi kuhakikisha CCM inashinda.
 
CCM kipima joto chao kimeonyesha ukweli kwamba Mwenyekiti ya Halmashauri ya Tarime ndugu Charle ndiye anakubalika zaidi kuliko Kaongoye na Makamba na Gachuma .Kangoye ni mkono wa Gachuma na Makamba ni kipaza sauti tu .Niko Tarime sasa na hakuna matatizo yeyote ila uwingi wa askari umezua maswali na kila mara watu wako katika makundi makundi wanashangaa kama kweli ni Wanchari ama ndiyo mambo ya Kiteto nk .Hivi Kova kweli leo anakuwa ni jibu la Tarime ? Kama ni kweli kwa nini sasa asipelekwe kuwa RPC hapa Mara badala ya kanda maalumu ?

CCM yetu macho na rushwa imeshamiri Tarime na wanaomba wazi wazi na maaskari wa barabarani na wale wa Patrol nk .
 
Lunyungu unachemka! hivi kuna tatizo gani vyombo vya ulinzi na usalama kuwepo hapo ilhali hali ya Tarime ni tete? If anything hiyo ni blessing na uhakika wa usalama acha spin zako

Tatizo siyo hao mapolisi wa CCM kuwepo.Tatizo ni je wao nao watapiga kula au watasaidia kuiba na kuiwezesha CCM kushinda.Hapo ndo hofu inaanzia.
 
Mbio za mwenge zilikuja na wagombea uchaguzi kwa ticket ya ccm mpaka nyamongo ambako ni balaa kwa upizani....polisi lazima tarime jamani....uku kuna siasa za jazba mgombea mmoja anaweza kuwajaza jazba hawa watu na wakafanya maajaabu uku roho za wasio husika zikawa matatani...

Wakati wa kifo cha kipenzi mbunge wao...njia ya tarime nyamwaga nyamongo ambayo inapita kijijini kwa Chacha ilifungwa kwa ajiri ya usalama...lakini bado kuna tatizo lilitokeza.Kama umeanza sikia kuwa hata CCM wamsimamishe na upinzani wasimamishe GOGO,gogo litashida...

Tatizo kuu uku ni jazba ya wananchi na ukikuta mwasiasi anajua kutumia mdomo wake vyema basi lazima vurugu ndio maana wameleta vijana wa kazi(ghasia kuu.kutuliza ghasia)Mapigano ya kikabila yapo tena kwa minor reasons...recently Nyamongo na kijiji cha jirani walianza pigana kwa ajiri ya ng'ombe kuibiwa nyamongo.See

Hii inayo endelea ni ya mbuzi waliibiwa..kwenye kijiji kingine na mwenzao akaenda fatilia akauwawa..kwa taarifa ukiua mmoja wao ni dhahama...na sio wanchori na wanchari.

Uchaguzi hauwezi fanyika katika hali hii...sasa njia mbadala ni kuleta polisi hata kama hawapiga watu kuonekana tu kunaweza tuliza munkari wa wananchi...

Mwanasiasa akitaka kushinda uku ni lazima kwanza awe against CCM,Barrick hasa north mara..mining.Aonyeshe kuwa ardhi inayo chibwa na wawekezaji ni uny'anganyi usio kuwa wa halali...kwa ujumla aongee negative kuhusu the whole system iliyopo..tena kwa jazba utaona anavyo shida.Kila kitu ni nguvu uku.

Lunyungu kama uko maeneo haya..unaweza jua hali halisi kama hutaongelea katika mtizamo wa kisiasa zaidi...na unaweza unganisha na siasa uone mambo inavyo weza kuwa tarime.

Niko kwenye middle of issue.
 
Lunyungu unachemka! hivi kuna tatizo gani vyombo vya ulinzi na usalama kuwepo hapo ilhali hali ya Tarime ni tete? If anything hiyo ni blessing na uhakika wa usalama acha spin zako

Mapigano yamekuwepo muda mrefu, hao askari 300, Kova na Tossi wapo siku zote mbona hatukuwaona wakija tarime?

Kama wamekuja kuhakikisha hali ya usalama inakuwepo tarime basi na wafanye hivyo muda wote tena waende maeneo ya vijijini kwenye mapigano wakashike doria huko kukomesha wizi wa mifugo,watafute suluhu ya kudumu na si kuzurura mjini.

Inajulikana warenchoka na wanchari wako maeneo yepi na ni wapi wanapoendesha mapambano-huko kubiterere na kwingineko,hivyo basi hao askari waende huko wakashike doria na kutafuta suluhu ya kudumu baina ya pande zinazopigana.

Tossi huyu si yeye ni mtaalamu wa kukamata wanaochemsha gongo maporini mara hii tena kaanza kuingia mijini?

Anyways, all in all tunajua serikali itatumia kisingizio cha mapigano kujaza askari tarime lakini ukweli ni kuwa wamekuja kuiongezea ccm nguvu.

Lakini wacha tuendelee kuwaangalia wanachofanya, kama kweli wameamua kuja kutafuta suluhu ya ugomvi wa hizi koo hasimu,tutawapongeza,kinyume na hapo tutawazomea!
 
Lunyungu unachemka! hivi kuna tatizo gani vyombo vya ulinzi na usalama kuwepo hapo ilhali hali ya Tarime ni tete? If anything hiyo ni blessing na uhakika wa usalama acha spin zako

Hebu we masatu na hiyo ccm yako acheni unafiki, tangu lini mmeanza kuijali tarime? Mara ngapi tunapiga kelele hapa kwamba ndugu zetu wanamalizana huko wanauana kama wanyama? mbona hawajawahi hao kina kova na i dont know who kwenda na vikosi vyao vya watu mia sita kutuliza na kukomesha hiyo vita ya wanchari na warenchoka once and for all? Huo ni upuuzi na unafiki mkubwa. Wanajipendekeza kwa sasa kwamba wanawajali ili wawapihie kura au wameenda kutumia nguvu na kutisha wananchi ili waibe na kushinda uchaguzi? I really hope wanatarime wasuse kabisa kupiga kura kuliko kuchezewa akili.
 
Mvungi alijitakia mwenyewe. Huu ugomvi wa Wanyanchare sijui na akina nani wale umekuwepo muda mrefu tu mbona FFU hawakupelekwa. Sasa wakati uchaguzi mdogo unapokaribia ndipo mnapeleka jeshi la CCM?

Ndo hayo yatushangazayo Wananchi kuhusu Polisi kusimamia matakwa ya Watawala kwa nguvu zote wakituacha Wananchi tunaumizwa na kuumizana.

Salaam tokea Tarime .Mambo si shwari na CCM sasa wameamua kufanya yale yaliyo tegemewa .Nimeshuhudia Tossi leo na kikao kikubwa hapa Tarime na Kova anategemea kutinga muda wowote ili kuhakikisha CCM wanapata jimbo hili .Hii ni baada ya wana Tarime kumkataa Kangoye Ryoba ambaye anabebwa na Makamba na Gachuma ambao wamesema ni mtu wao na lazima apite .Wana Tarime wanasema wana imani na Charle Mwela baada ya CCM kumkataa kipenzi wao Nyambali Nyangwire .Ukweli upo maana Dodoma kumekuwa kimya kwa siku 2 hadi jioni hii walipo amua kumoa Kangoye wa TRA kisa yeye na gachuma ni damu damu na Makamba yeye ni omba omba anajua chake cha juu kiko wazi .

Jeshi la Polisi linafanya kufuru sasa maana leo pekee wameletwa 300 na wiki hii wanategemea wengine 600 zaidi kwa jina la vurugu za kikabila lakini ukweli ni kwamba jimbo la Tarime lirudi CCM ndiyo nia yao .JK na Mwema yetu macho na tuna waangalia kwa makini sana .Chadema bado wana uwezo mkubwa wa kulitwaa jimbo hili kwa mujibu wa uchunguzi wangu na imekuwa tishio hadi Tossi na Kova kuaminiwa kuja kulirudisha jimbo .

Ndo yaleyale yanatufanya tuishange Serikali hii kila kukicha, Maalbino wanauwawa kinyama Serikali inapiga propaganda tu na Polisi wapo na hawachukui hatua yoyote ya maana lakini inapofikia suala la kutetea Maslahi ya Watawala wako tayari hata kuuwa kuhakikisha matakwa ya Watawala yanafikiwa!

Wiki hii huko Mara North Gold Mine, Majambazi yamevaimia Mgodi na mabomu na Bunduki za Kivita, yameua Mfanyakazi wa Mgodi na kujeruhi Polisi waliotumwa kutoka Mkoani na yakaishia (sina hakika kama yalipora au la) na hatujasikia Kamanda Tossi kapelekwa na FFU kuyasaka na wala hayajitiwa nguvuni. Lakini suala la uchaguzi Watawala wanataka kulifanya tete na sitashangaa kusikia baadhi ya watu wakajeruhiwa, kuuwawa na kutiwa ndani ati kwa kusababisha fujo.

NAsikia uchaguzi wa 2005 Wana Tarime walijitoa muhanga kwelikweli maana ilibidi FFU kutoka mkoani waondoke na Msimamizi wa Uchaguzi na matokeo yalitangaziwa Musoma! Nina wasiwasi kuwa ripoti za vyombo vya habari wakati wa mazishi ya Wangwe ziliandaliwa ili kuweka mazingira ya kumwaga Polisi ili kuhakikisha Uchaguzi unavurugwa na Watawala wanahakiksha mgombea wao anashinda.
 
Naomba kuuliza POLICE kazi yao ni kulinda WANANCHI au kuwalinda MAFISADI?
1. Vurugu MARA ni za muda mrefu sana hata kabla ya kifo cha Mpendwa wetu WANGWE
(RIP) hatukusikia wala kuona wakipelekwa 300 kwenda kulinda AMANI. sasa leo hii hao
askari 300 wametoka wapi??

2. Maadili ya JESHI LA MAFISADI SORRY POLICE ni nini?
a. Kwenda kupiga kura hewa.
b. Kuwalinda MAFISADI na sio WANANCHI.

3. KOVA ni Kamanda wa KANDA MAALUMU ipi Tanzania nzima ama DSM?
4. Ina maana KOVA na TOSSI ni vibaraka wa MAFISADI?
 
Hivi ni lini Tanzania itakuwa na UCHAGUZI HURU NA WA HAKI?
 
Hukusikia yaliyomkuta Dr Mvungi?
Masatu,
Taarifa zako sijui source yake nini? Hali tete leo? Mbona Wangwe, ndani ya Bunge amepiga kelele siku nyingi na Polisi wengi kiasi hicho hawajapelekwa hata siku mmoja? Tunafuatilia kwa karibu nini kinaendelea. Maadili ya uchaguzi yasipofuatwa process ya demokrasia inakuwa derailed. Nadhani uwepo wa excessive presence of the state organs athari yake inajulikana. Hasa pale visingizio mbalimbali vinapoanza kutumika kama ilivyotaka kufanyika juzi kuanza kukamata vijana wenye pikipiki, Tarime mjini. Hata hapo kuna mapigano? Pikipiki ni silaha za mapambano? Au kuna lililojificha?
 
Dr.Slaa, heshima yako mkuu.
Unajua kwa watu wasioijua tarime ni rahisi sana kupotoshwa na hivi vyombo vya habari vya mafisadi +TBC.
Kwa mfano wakati kulipotokea mapigano ya wahunyaga vs wamera na watu kuuwawa polisi hawakuwa na haraka yoyote ya kupeleka askari.Siku chache baadaye kukatokea chokochoko za kuzuka mapigano ya mahasimu wa jadi warenchoka vs wanchari lakini kama kawaida yao polisi walikuwa kimya.
Mimi niliposikia juzi eti mkuu wa wilaya ameshindwa kushiriki kwenye mbio za mwenge ili kwenda kutuliza mapigano ya wanchari vs warenchoka huku jeshi la polisi likizuia mkutano wa chadema, nikajua sasa mikakati ya ccm imekamilika kinachofuata ni utekelezaji tu, na huo ndio ulikuwa mwanzo wao.
Kwa watu walio makini wanakumbuka ni kwa kiwango gani na mara nyingi kiasi gani marehemu wangwe amekuwa akiisihi na kuiomba serikali ikomeshe mapigano ya koo tarime bila mafanikio yoyote.
Na kama ni hali ya usalama kuwa tete, sio tarime mjini walipojaza askari, waende huko mwema,kubiterere na bumera ndipo watu wanauana.
 
Npata hasira sana na huu upuuzi unaofanywa na chana tawala sijui nini.Unajua hata polisi wenye akili wanapata hasira sana mana nilibahatika kukaa na marafiki zangu ni maaskari arusha hawa,wanasikitika sana kwa kitendo cha kupelekwa kiteto kwennda kuwatisha raia.Ila nataka kuwahakikishia kwa tarime wamechemka wale hawatishiwi nau hata siku moja bwana.watafute mbinu nyingine sio hii ya kipumbavu.nilisoma tarime miaka miwili na muda wote huo sikuwahi hata kuwaona hao ffu iweje leo wapelekwe huko?
 
Kila mtu hapa anaongea katika mtizamo wa kisiasa...lakini hatuongea hali halisi ya wilaya ya tarime watu walivyo..na uchaguzi unao kuja kutakuwa na impact gani kama watakuwa na jazba kama kawaida yao...hivi mapigano yanaendela uchaguzi utafanyikaje?

Yes hawakupeleka askari toka awali lakini kwa sasa ni lazima Dk.Slaa anajua nini maana ya jazba ya hawa watu wa uku.....wakati wa kupiga kura ni wakati unapo hitajika utulivu..na amani ili watu wapige kula..

Kwenye eneo ambapo kijiji wanaweza pigana kwa ajiri ya ng'ombe mmoja...si swala la utani hili.Majita..mtu kwao..Mwita maranya..na wengine...

Angalia hili tatizo katika pande mbili sio kwa sababu kova na tossi wako hapa...mbona wakwenda nyamongo kwenye operation maalumu ya kupunguza vibaka(intruders) wakaa kwa wiki nane...wakahama wote kwenda tarime,musoma,mwanza na kwingineko..baada ya operation kwisha wote wamerudi...ugomvi ni asili yao polisi wanakuja leo..wanawapiga..baada ya wiki nzima warudia tena ugomvi....

Hawana jingine la kufanya...kama hawalimi...na wana ardhi nzuri...ingekuwa kwa wasukuma wala haya mapigano ya koo usinge yasikia..

Check mji wa nyamongo maendele ni duni kwa ajiri ya watu wake wenyewe kuwa na kichw ngumu,ulitakiwa uwe kama kahama,geita,nzega kote kwenye madini...lakini hata umeme wa grid ya taifa hamna mpaka sasa...hii ni kwasababu hata kuwa compasated ili nguzo za umeme zije hawataki...utafikiri umeme ni wa mgodi peke.

Good day
 
Buswelu inaonanekana unayajua mazingira ya Tarime vizuri kuliko Kaka Lunyungu anaejidai yupo "Tarime"....
 
Mbowe,Lunyungu,DK.slaa,Mvungi,zitto,mrema....na mkuu wa wilaya anajua hali halisi ziaidi ya siasa morali waliuyo nayo watu wa uku..uku kuna msema wanaume hawapigwi wote jamani...

Mtu asiye na kovu si mwanaume...lazima uwe na alama flani ya kukatwa ajari...kuonyesha umepitia hard time....mtu kwenda jela ni sifa...sasa wakati wa uchaguzi kuwaacha bila kuwa na hata picha ya askari...unataka kutengeneza nini...?

Mie naunga mkono askari kuwepo hapa kwa kulinda usalama hasa wakati huu wa uchaguzi....mabasi yote yatokayo nje ya tarime stand kuu ni tarime,si kila mtu anataka kupiga kula bwana...sasa kama zogo litazuka stand polisi hawapo..na unataka kwenda mwanza,sirari,kenya...si utakuwa victim...?

Kwanza uku hakuna anaye ongelea polisi hata kidogo ni sie kwenye mtandao....watu wanaongelea CCM kushidwa tu...hatakwa kuweka gogo...lipigiwe kula..kwa mwenye kupambanua..unawe jua ni nini hawa watu wako tiyari kufanya.

Ingekuwa usukumani wangesema doho tabu...tokwicha...wanaachana na uchaguzi.

Good day
 
Kila mtu hapa anaongea katika mtizamo wa kisiasa...lakini hatuongea hali halisi ya wilaya ya tarime watu walivyo..na uchaguzi unao kuja kutakuwa na impact gani kama watakuwa na jazba kama kawaida yao...hivi mapigano yanaendela uchaguzi utafanyikaje?

Yes hawakupeleka askari toka awali lakini kwa sasa ni lazima Dk.Slaa anajua nini maana ya jazba ya hawa watu wa uku.....wakati wa kupiga kura ni wakati unapo hitajika utulivu..na amani ili watu wapige kula..

Kwenye eneo ambapo kijiji wanaweza pigana kwa ajiri ya ng'ombe mmoja...si swala la utani hili.Majita..mtu kwao..Mwita maranya..na wengine...

Angalia hili tatizo katika pande mbili sio kwa sababu kova na tossi wako hapa...mbona wakwenda nyamongo kwenye operation maalumu ya kupunguza vibaka(intruders) wakaa kwa wiki nane...wakahama wote kwenda tarime,musoma,mwanza na kwingineko..baada ya operation kwisha wote wamerudi...ugomvi ni asili yao polisi wanakuja leo..wanawapiga..baada ya wiki nzima warudia tena ugomvi....

Hawana jingine la kufanya...kama hawalimi...na wana ardhi nzuri...ingekuwa kwa wasukuma wala haya mapigano ya koo usinge yasikia..

Check mji wa nyamongo maendele ni duni kwa ajiri ya watu wake wenyewe kuwa na kichw ngumu,ulitakiwa uwe kama kahama,geita,nzega kote kwenye madini...lakini hata umeme wa grid ya taifa hamna mpaka sasa...hii ni kwasababu hata kuwa compasated ili nguzo za umeme zije hawataki...utafikiri umeme ni wa mgodi peke.

Good day

Wakati mwingine mambo ya kipuuzi kama haya inabidi yakemewe kabisa hapa JF na kwingine kokote. Hii generalization na dharau dhidi ya watu wa Tarime imezidi sana hapa JF na kwenye vyombo vya habari.

Wewe Buswelu acha upuuzi na ujinga wa kusema kuwa watu wa Tarime asili yao ni ugomvi. Mimi nimezaliwa na kukulia Tarime na sijawahi kuona hayo ya ugomvi wa asili na uvivu kama unaotaka kuuweka hapa.

Ukome kabisa kutumia lugha chafu dhidi ya watu wa Tarime. Kusema kuwa wao wangekuwa wasukuma kusingekuwa na mapigano ni upuuzi mkubwa sana na unaofaa kukemewa kwa nguvu zote.

Yanayoendelea Tarime yanajulikana kwa wanatarime na namna migogoro ya kipuuuzi inavyoletwa na kukukuzwa na vyombo vya usalama na vya habari ili kuwatoa watu kwenye the main issue ya Tarime - deposit kubwa kabisa ya dhahabu ambayo bado haijaanza kuchimbwa.

Hao polisi wanachofanya kinajulikana na watu wa Tarime wanawaangalia tu kwa mshangao. Mimi ningewashauri wa usalama kuwa makini na wastaarabu sana dhidi ya watu wa Tarime au watanzania wowote kokote kule Tanzania. Haya mambo ya kipuuzi na generalization za kizembe kama hizi hazitapelekea kusolve matatizo ya watu wa Tarime au watanzania ambao wanaendelea kuwa masikini kila kukicha.

Nimetumia lugha kali kwa makusudi ili kukemea upuuzi na maneno yako yenye vijembe dhidi ya watu wa Tarime kwako Busweli. Natumaini utaacha upuuuzi huu na kuanza kuheshimu watu wa Tarime ambao wengi wao ni wastaarabu na watu wasiopenda fujo.

Asante
 
Masatu,
Taarifa zako sijui source yake nini? Hali tete leo? Mbona Wangwe, ndani ya Bunge amepiga kelele siku nyingi na Polisi wengi kiasi hicho hawajapelekwa hata siku mmoja? Tunafuatilia kwa karibu nini kinaendelea. Maadili ya uchaguzi yasipofuatwa process ya demokrasia inakuwa derailed. Nadhani uwepo wa excessive presence of the state organs athari yake inajulikana. Hasa pale visingizio mbalimbali vinapoanza kutumika kama ilivyotaka kufanyika juzi kuanza kukamata vijana wenye pikipiki, Tarime mjini. Hata hapo kuna mapigano? Pikipiki ni silaha za mapambano? Au kuna lililojificha?

Msianze kutenganeza mazingira ili mkishindwa mpate kupiga kelele .Mnaanza kutuandaa mtakaposhindwa mje na hoja za polisi.

Kama mnaona vipi wawakirishi ktk vituo vya kupigia kura wawekeni makomandoo wa chadema na wao baada ya matokeo watakua na copy za matokeo hivyo wakitoa matekeo siyo ,ninyi mtuletee facts hizo Na si fact za FFU na POLISI.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom