Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Mnyika,Nakubaliana na Mwjj kuwa kama kuna ushahidi, picha, video n.k. zitolewe, katika kuwafahamisha wana JF na sio kama ujumbe kwa IGP.
- Hivi JF ni chombo cha habari au ndio CHADEMA inapotolea matangazo yake? Mbona chama kikubwa namna hii kinafanywa kuwa kama kikundi tu cha mitaani au chama cha wanafunzi?
- Imejulikanaje kuwa waliokamatwa wamekamatwa kwa sababu za kisiasa na sio vurugu au ubovu katika utendaji wa jeshi letu la polisi? Hebu tupe ushahidi ili tusione kuwa ni malalamishi tu ya kisiasa.
Halafu, unless tufahamishwe kuwa kuna uhusiano wa kimaslahi kati ya JF na CHADEMA, otherwise JF isitumiwe kutolea matamko ya vyama vya kisiasa kwa serikali. Tukifanya hivyo tusije tukalalamika JF ikija kuvamiwa tena.
Kubwajinga nadhani unafanya makusudi sasa .Ina maana hoja za Chadema kuja hapa leo hii pekee ndiyo unazua hoja za aina hii ?
Hebu tujikite kwenye hoja ya sasa ya Polisi na CCM kunyanyasa watu Tarime badala ya kutupotezea muda tafadhali .