Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mnyika,
  1. Hivi JF ni chombo cha habari au ndio CHADEMA inapotolea matangazo yake? Mbona chama kikubwa namna hii kinafanywa kuwa kama kikundi tu cha mitaani au chama cha wanafunzi?
  2. Imejulikanaje kuwa waliokamatwa wamekamatwa kwa sababu za kisiasa na sio vurugu au ubovu katika utendaji wa jeshi letu la polisi? Hebu tupe ushahidi ili tusione kuwa ni malalamishi tu ya kisiasa.
Nakubaliana na Mwjj kuwa kama kuna ushahidi, picha, video n.k. zitolewe, katika kuwafahamisha wana JF na sio kama ujumbe kwa IGP.

Halafu, unless tufahamishwe kuwa kuna uhusiano wa kimaslahi kati ya JF na CHADEMA, otherwise JF isitumiwe kutolea matamko ya vyama vya kisiasa kwa serikali. Tukifanya hivyo tusije tukalalamika JF ikija kuvamiwa tena.

Kubwajinga nadhani unafanya makusudi sasa .Ina maana hoja za Chadema kuja hapa leo hii pekee ndiyo unazua hoja za aina hii ?

Hebu tujikite kwenye hoja ya sasa ya Polisi na CCM kunyanyasa watu Tarime badala ya kutupotezea muda tafadhali .
 
Jamani huku tuelekeako kuna tisha jama! Yaani pesa mwana haramu, mtu anageuka kuwa kama roboti bila hata kutumia akili ya kuzaliwa? we unaambiwa kamata mtu tu bila sababu yoyte unatekeleza tu!!!

Hivi majeshi yetu kwanini wasitumie akili na kuwa huru kukataa kukiuka miiko yao ya kazi? nijuavyo wameapa kulinda raia na mali zao si kulinda maslahi ya kikundi cha watu wachache, kwanini wanapo ambiwa kitu ambacho si shahihi nao wasikatae?

Majeshi yetu matuangusha kwa kukubali kuwa vibaraka badala ya kusimama na kutetea haki kwa kadri ya viapo vyenu! Damu itakayo mwagiga itakuwa juu yenu milele.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba, kwenye mambo muhimu kwa wana Tarime kama ukosefu wa maji ya uhakika, makampuni ya madini kumwaga sumu kali na mbaya sana kwenye vyanzo vya maji Tarime, Tarime kutopata share yao ya mapato ya madini, hakuna kiongozi wa serikali au ccm anayetokea hata kuhutubia na kuwasaidia wana Tarime.

Wangwe na Sasi walipigania kufa na kupona haki za wanatarime wakaishia kuwekwa jela kwa shinikizo la makampuni ya madini mpaka pale Tundu Lissu alipokuja Tarime na kushikia bango kesi yao na serikali ikaamua kuwaachia.

Wanatarime wengine waliojaribu kutetea haki za Tarime walikufa kwa "ajali" - mwanaharakati Maisa - na wengine waliishia kupigwa risasi za moto na walinzi wa makampuni ya madini. Haya yote hayakumleta Makamba, Msekwa, Wasira na wengine wote hadi leo wakati wa uchaguzi.

Hii ni aibu kwa serikali na kwa Rais Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa ccm kwa Tanzania nzima. Ndio maana mie naamini kuwa kinachoendelea sasa hivi Tarime sio suala la kupata kiti cha ubunge na udiwani bali ni swala kubwa tu ambalo serikali kupitia vyama vya siasa wameamua kuanzisha Tarime ili kutia adabu wana Tarime ambao wamekuwa wanadai haki zao kama raia kwa miaka mingi sana.

Hii ni aibu kabisa.
 
Picha zinasema maneno mengi na zinatumia lugha nyingi. Ni sawa na mtu anasema "fulani ananunua kadi za kupigia kura" na hadi leo huyo fulani hajawahi kujitokeza au kuwekwa mtego wa kukamatwa wanunuzi n.k Sasa sitaki kuamini kuwa hakuna mtu anayeweza kutega mtego wa namna hiyo.

Sisemi vitendo hivyo vya Polisi havipo (nawajua polisi wetu) ninachosema ili kuweza kuleta outrage and outcry; show the world the pictures!!

Hapa mimi ndipo huwa napishana na ndugu zangu wanasiasa, katika maisha yangu hakuna kitu kibaya kama kudhani na wanasiasa wetu wa siku hizi wanathubutu sana hasa panapokuwa na jimbo la kushindania. Mimi naamini hizi fujo na mengineyo yangekuwa yanaletwa kwa picha kama alivyosema mwenzangu Mzee mwanakijiji nafikiri hapo ingekaa sawa sana na ndio maisha bora yanavyotaka. "Seeing is Believing" WEKENI PICHA MEZANI TUSHUHUDIE NA SIO KUBWABWAJA TUUU.
 
Ukisoma gazeti la Mtanzania la leo, ukurasa wa kwanza "Kampeni zazidi kunoga Tarime" utaona Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa anasema,

"Wakati nakuja (tarime), rais (Kikwete) alinituma kuangalia kama kweli kuna fujo au la, lakini tangu niwasili wilayani hapa yamekuwapo matukio ya fujo. Nilipokuwa naingia Tarime, msafara wangu ulizomewa na kurushiwa mawe. Leo (jana) usiku nitamjulisha hali halisi ilivyo, na ifahamike yeye ni Amiri Jeshi Mkuu, kwa hiyo atampa maagizo Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo msije mkajuta."

Leo asubuhi saa 5.20, Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, akiwa katika jengo la CRDB Bank Tarime, aliendewa na maofisa wa polisi wakiwa na vijana wa FFU na muda mfupi wakaondoka na kuanza kamata kamata.

Wakati huo dereva wa polisi aitwaye Constantino jana alipakia viloba vya mchele, kuku na kuni nyumbani kwa mgombea wa CCM.

Wakati hayo yakiendelea, Mwenyekiti wa DP, anayejiita Mchungaji, Christopher Mtikila, yuko eneo la Sirari akisambaza vipeperushi vinavyosema kwamba Mbowe kamuua Wangwe, anafanya hivyo akiwa analindwa na polisi.

Watu wana ushahidi hadi wa picha za matukio hayo.

Nini maana ya yote haya yanayotokea:

-Kama Taifa tunakoelekea ni kubaya na tutarajie maafa ama machafuko huko.
-Tujiandae kutokea pengine mabaya zaidi ya yaliyotokea Pemba mwaka 2001, wakati huo Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi, kama ilivyo sasa Kikwete yuko nje ya nchi.
_Kuna kila sababu kwa wapenda amani kote nchini kukemea mara moja vitendo vichafu vinavyofanywa na CCM.

Wakati huo dereva wa polisi aitwaye Constantino jana alipakia viloba vya mchele, kuku na kuni nyumbani kwa mgombea wa CCM.

Hiyo ya dereva wa polisi ilikuwa Sept 22 saa 5.30 kweupee, gari la FFU Makao Makuu TP 1408 dereva S/SGT Constantino C5967, na walipakia mchele, ndizi na vyakula vingine nyumbani kwa Mgombea wa CCM
 
Ushahidi mzito sana huu, uwekwe kwenye rekodi unaweza kutumika baadae
 
Kubwajinga nadhani unafanya makusudi sasa .Ina maana hoja za Chadema kuja hapa leo hii pekee ndiyo unazua hoja za aina hii ?

Hebu tujikite kwenye hoja ya sasa ya Polisi na CCM kunyanyasa watu Tarime badala ya kutupotezea muda tafadhali .

Lunyungu,
Kama sijakosea huu ujumbe ulikuwa ameandikiwa IGP toka kwa kiongozi wa juu wa CHADEMA. Ndio maana nikataka kufahamishwa kuwa JF ni chombo cha habari au ni kitengo cha CHADEMA?

Kama chama kinaendeshwa kwa jinsi hii, basi inaonyesha wazi jinsi kulivyo na upungufu wa busara kiutendaji ndani yake.

Mimi nimeshindwa kuelewa nia ya Mnyika kubandika ujumbe huo kuwa ilikuwa ni kututaarifu yanayotokea Tarime au ndio ujumbe aliomwandikia IGP.
 
Hakuna makosa yoyote kubandika huu ujumbe hapa. IGP hataweza kukataa kama mambo yatawekwa kweupe namna hii. Hii haina tofauti na wale ambao wanaandika ujumbe kwa Kikwete, Mbowe, Mtikila na viongozi wengine kupitia hii forum.

Hii forum inasomwa na watu wengi na vizuri ikajulikana kuwa IGP amejulishwa kinachoendelea Tarime.
 
Nyumba 60 zateketezwa moto Tarime

na Chris Mang'era, Tarime

KAYA 17 zenye nyumba 43 na maghala 17 ya kuhifadhia vyakula, zimechomwa moto katika Kijiji cha Turugeti wanakoishi wananchi wa koo za Wahunyaga na Wamera, wilayani Tarime, Mara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jana, Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Stanley Kolimba, alisema nyumba hizo na maghala hayo ni mali ya koo ya Wamera na kwamba zilichomwa moto na wananchi wa koo ya Wahunyaga, wote wakazi wa Kijiji cha Turugeti.

Kolimba, alisema kwamba tukio hilo lilitokea juzi alfajiri na kwamba Wahunyaga, walifikia hatua ya kufanya uhalifu huo baada ya mifugo ya Wamera, kuvamia na kuharibu baadhi ya mihogo ya Wahunyaga.

Alisema polisi walifanikiwa kuwahi eneo la tukio na kuwazuia wananchi wa koo ya Wamera waliokuwa wamejiandaa kujibu mapigo kwa kuwashambulia Wahunyaga waliowachomea miji yao.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya, hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo na kuongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na wanakijiji husika, wanaendelea na tathmini ya kujua thamani halisi ya mali zilizoteketea katika tukio hilo.

Aidha, alisema Polisi, wanaendelea kuweka ulinzi kijijini hapo pamoja na kuendesha msako dhidi ya waliohusika katika tukio hilo ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Alisema wanakijiji waliochomewa nyumba na maghala, wamepata hifadhi ya muda katika miji ya jamaa zao na kuongeza kuwa serikali inaandaa mipango ya kuwasaidia.

Tukio hilo limekuja mwezi mmoja baada ya koo hizo kuzusha mapigano makali na kusababisha Wahunyaga wanne na Mmera mmoja na wengine kadhaa kujeruhiwa huku nyumba na maghala ya vyakula vikichomwa moto.

Chanzo cha mapigano hayo kinadaiwa ni uhasama wa wizi wa mifugo uliojengeka baina ya koo za Wahunyaga na Wamera, zote za kabila la Wakurya.
 
Nyumba 60 zateketezwa moto Tarime

na Chris Mang’era, Tarime

Hii Tarime ndio eti inaongoza kwa mabadiliko? Unaharibu mali za ndugu zako huku ukikumbatia wageni toka mbali?

Watu wa Tarime acheni ujinga huo. Maendeleo na amani yanaanzia nyumbani kwako, ukishindwa kumtendea haki mwana Tarime mwenzako, kweli utamtendea haki mtu wa mbali?

Pataneni kwanza kabla hata ya kutuhubiria mabadiliko wengine. Mnachofanya ni ujinga kuuana na kuibiana kila siku. Tafadhali tatueni matatizo yenu kwa faida ya wilaya yenu.
 
Mtanzania,

Jiulize kuwa haya "mapigano" yameanza lini Tarime? Kama yalianza zamani, je polisi au vyombo vya usalama vilikuwa wapi kuyazuia? Na kama yameanza leo, je kwa nini yaanze leo? je inawezekana hii ni sababu ya kuhalalisha kuleta mamia ya polisi Tarime leo hii (siku chache kabla ya chaguzi) ili kuzuia "haya mapigano".

Naona una bidii sana kuleta habari za machafuko hapa mtandaoni. Kama nia yako ilikuwa kuchafua wanatarime na kuanza kuwapondea ili kuhalalisha kauli ya amiri jeshi mkuu wa Tanzania kuwa Tarime kuna fujo, basi unafanikiwa sana tu mkuu.
 
Popote pale Tanzania ambapo CCM huwa inabanwa kwenye uchaguzi hutokea fujo, tena fujo kubwa, na fujo zote hizi hufanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM. CCM wataingiza hii nchi kwenye maafa. Kama hawapo tayari kwa ushindani wa kistaraabu wangefuta mfumo wa vyama vingi kulikoni kuendelea kuwadanganya watu.
 
Magabe,

Ni wajinga tu wanaounga mkono machafuko na thanks God I am not one of them.

Mimi nimewaambieni ukweli kama kwa kufanya hivyo naunga mkono machafuko basi vizuri.
Siasa za shoot the messenger hizo, ukitegemea ujumbe utakufa.

Hakuna cha visingizio juu ya hayo mapigano. Serikali ina makosa yake, kama walivyo polisi lakini pia Wana Tarime wana makosa makubwa. Huwezi kupigana na ndugu yako huku unajifanya utaunganisha nchi. Charity starts at home.

Hakuna cha kisingizio cha mapigano yameanza lini, kama wilaya mna wajibu wa kutatua hilo tatizo sugu. Unganieni na kuondoa hiyo kero ya kuuana na kuibiana kisa eti koo tofauti.
 
Nakuunga mkono kufuta vyama vingi.

Lakini lazima tukubali na tujifunze kuukubali ukweli kua tarime kuna wizi haswa wa ng'ombe na solution yake hua ni mapigano na kuuana h.huo ndio ukweli.

Na hawa wezi wamejipanga kutumia uchaguzi huu kwa kuibia watu yani wewe unatoka ktk mkutano wa kampeni unakuta nyumbani kweupe peeee .

Ni sawa tu na wahuni wachache wanapotumia maandamano fulani kuibia watu .

Ama ngoja niulize swali MBONA ktk maandamano ya AMANI hua wamejaa polisi?? Na je tumeshawahi kuhoji kwanini polisi wanajazana kwenye maandamano?
Na je kimantiki maandamano na mikutano ya kampeni kwa TZ inautofauti upi ktk hali ya kiusalama?

Mimi nadhani kamanda mzuri hujaza watu wake mahala anapohisi kwa namna moja ama nyingine uwezekano wa vurugu kutokea ni mkubwa.

Mfano hapa JUVENALIA za wanafunzi yani ile sherehe ya wanafunzi polisi hujazana sana na hakuna anayewahoji kwanini wamejazana pale.

Polisi kujazana TARIME ni mda mwafaka,Na anayeleta vurugu ama za kuletwa lazima aadhibiwe VIGOROUSLY
 
Hii Tarime ndio eti inaongoza kwa mabadiliko? Unaharibu mali za ndugu zako huku ukikumbatia wageni toka mbali?

Watu wa Tarime acheni ujinga huo. Maendeleo na amani yanaanzia nyumbani kwako, ukishindwa kumtendea haki mwana Tarime mwenzako, kweli utamtendea haki mtu wa mbali?

Pataneni kwanza kabla hata ya kutuhubiria mabadiliko wengine. Mnachofanya ni ujinga kuuana na kuibiana kila siku. Tafadhali tatueni matatizo yenu kwa faida ya wilaya yenu.

Mtanzania,
Badala ya kulaumu victims lawama zako ungezielekeza kwa dola. Polisi na FFU waliomwagwa Tarime wako wapi kuhakikisha uhasama wa aina hii haufanyiki? Wenyewe wamejibanza Tarime mjini tu kuwabana wana Chadema wasifanye mikutano yao. Hebu jiulize mbona enzi za Mwalimu hatukusikia uhasama huu wa kikabila? Leo chini ya CCM kuna lawlessness ambayo dola imeshindwa(makusudi) kuidhibiti.
 
Popote pale Tanzania ambapo CCM huwa inabanwa kwenye uchaguzi hutokea fujo, tena fujo kubwa, na fujo zote hizi hufanywa na polisi kwa maelekezo ya CCM. CCM wataingiza hii nchi kwenye maafa. Kama hawapo tayari kwa ushindani wa kistaraabu wangefuta mfumo wa vyama vingi kulikoni kuendelea kuwadanganya watu.

Mkuu Kitila,

Una maana vita na kuibiana ng'ombe kwa hizo koo ni kwasababu ya CCM kubanwa?

Tuwe wakweli jamani, hatuwezi kutatua tatizo kama kila siku ni kukimbilia visingizio na kuacha tatizo.

Watu wanachinjana shauri ya ujinga na badala ya kukaa chini na kujaribu kutatua tatizo kazi kulaumu wengine tu.
 
Mimi naijua Tarime. It has nothing to do with CCM kubanwa, ila there is a leadership void that is being exploited by the 2 koos. Ndio maana nimeuliza mbona enzi za Mwalimu hukusikia uhasama wa aina hii? Mwalimu knew how to deal with it and he did. Waulize Wanatarime.
 
Magabe,

Ni wajinga tu wanaounga mkono machafuko na thanks God I am not one of them.

Hata mimi siungi mkono machafuko ya aina yoyote - yawe yanayosababishwa na polisi au wananchi wa Tarime. Lakini pia sishangilii habari ambazo hazina kichwa wala miguu kuwa Tarime "kuna fujo".

Mimi nimewaambieni ukweli kama kwa kufanya hivyo naunga mkono machafuko basi vizuri.

Kuna matumizi mengi sana ya neno ukweli, wewe kuleta habari za magazeti (ambayo wakati wa mazishi ya Wangwe yalitoa ramli kuwa Tarime kutawaka moto kwa machafuko kabla ya kupata aibu ya mwaka) haimaanishi kuwa wewe una ukweli.

Hali halisi ya mambo haisapoti kinachoandikwa na magazeti hapa ili kuweka sababu ya kujaza mamia ya polisi Tarime ili "kutuliza fujo".

Siasa za shoot the messenger hizo, ukitegemea ujumbe utakufa.

Hakuna cha visingizio juu ya hayo mapigano. Serikali ina makosa yake, kama walivyo polisi lakini pia Wana Tarime wana makosa makubwa. Huwezi kupigana na ndugu yako huku unajifanya utaunganisha nchi. Charity starts at home.

Mimi sina haya ya kukushoot wewe (messenger muhimu sana kwa habari za machafuko ya Tarime) ili kumaliza story. Ninasisitiza kile nilichosisitiza wakati wa mazishi ya Wangwe kuwa wananchi wa Tarime sio majuha kama ambavyo TBC1 na magazeti ya Rostam Azizi yalivyotaka (likiwemo mtanzania????) watu waaamini.

Mwisho wa siku, magazeti yalionekana yanachochea habari za uongo na mimi nilikuwa vindicated kwa kuonyesha picha halisi ya Tarime hapa JF - Hakuna fujo wa vita iliyotokea Tarime.

Hakuna cha kisingizio cha mapigano yameanza lini, kama wilaya mna wajibu wa kutatua hilo tatizo sugu. Unganieni na kuondoa hiyo kero ya kuuana na kuibiana kisa eti koo tofauti.

Wewe nimekuuliza useme kama una hakika kuwa Tarime kuna vita au la. Na swali la nyongeza ni kuwa vita ilianza lini (just in case utasema kuwa Tarime kuna vita na machafuko zinazohitaji mamia ya polisi kuzimaliza).

Hapa ni hoja tu huku maswali na majibu yakitolewa accordingly. Umbea na habari za uchochezi zitakemewa mkuu (katika hili nakuhakikishia right now).
 
Mkuu Kitila,

Una maana vita na kuibiana ng'ombe kwa hizo koo ni kwasababu ya CCM kubanwa?

Tuwe wakweli jamani, hatuwezi kutatua tatizo kama kila siku ni kukimbilia visingizio na kuacha tatizo.

Watu wanachinjana shauri ya ujinga na badala ya kukaa chini na kujaribu kutatua tatizo kazi kulaumu wengine tu.

Huna hakika na habari hii ya kuchinjana ndugu yangu Mtanzania. Umeanza lini kuwa mdaku na mzushi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom