Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Na waharifu hao hawana uhusiano wowote na CCM, eh?

Jasusi, uchokozi huo...wenye chama chao watakushukia kama mwewe kwa kifaranga....hawapendi kusikia hivyo..teh teh teh teh

Ushi
 
Mimi nashuhudia haya kwa kuwa niko Tarime na hata huko kwenye kata zinazo semwa ni uongo mtu ila Serikali imeamua kufanya uharamia juu ya wana Tarime .Chuki zilionyeshwa tangia zamani na Lowasa na sasa kila CCM nzima inaonyesha jinsi gani walivyo wastaarabu.

tafadhali kama uko jirani fika hapa opposite na Bank ya CRDB kuna vijana na wakina mama wanajitafutia maisha yao hapa wasikie kilio chao.Wanadiriki kusema Tarime ni Iraq maisha ya mtu hayathaminiwi bali kura tu .

Mwenyewe, brother yangu anafanya kazi kwenye kampuni ya Barrick. Nilimpigia simu couple of weeks ago baada ya kusoma habari kwenye magazeti ya Mengi kuwa "risasi zavuma tarime," lakini akanambia kuwa huo ni uzushi na kwamba tarime ni shwari kabisa. So sijui hizi habari za kipuzi zinatoka wapi?
 
Mimi nashuhudia haya kwa kuwa niko Tarime na hata huko kwenye kata zinazo semwa ni uongo mtu ila Serikali imeamua kufanya uharamia juu ya wana Tarime .
Kamalizie zile nyepesi zako na Tabwe
 
Mimi nashuhudia haya kwa kuwa niko Tarime na hata huko kwenye kata zinazo semwa ni uongo mtu ila Serikali imeamua kufanya uharamia juu ya wana Tarime .Chuki zilionyeshwa tangia zamani na Lowasa na sasa kila CCM nzima inaonyesha jinsi gani walivyo wastaarabu.

tafadhali kama uko jirani fika hapa opposite na Bank ya CRDB kuna vijana na wakina mama wanajitafutia maisha yao hapa wasikie kilio chao.Wanadiriki kusema Tarime ni Iraq maisha ya mtu hayathaminiwi bali kura tu .

Acha fix haupo Tarime wala nini... kamba tu...
 
Ombi: Hii ni independent thread hivyo ningeomba moderator (Invisible) aiache ijitegemee. In other words, P'se don't move it. I kindly request so.

Now, the thing that bother me the most, I suppose, is that the journalistic excellence in Tanzania is almost zero or close to nothing. It's not only unprofessional, it's ridiculously insane, too. And I hate it. I can't stand it.

The thing is: yes, kuna historia ya vita vya kikabila na koo wilayani Tarime since the era of Alexander the Great, but it really angers me kuona jinsi waandishi uchwara na wajingawajinga wa CCM [Msekwa, especially]wanavyotaka/jaribu ku-exploit hii issue kwa manufaa yao wenyewe. Manufaa ya kushinda uchaguzi mdogo wa uchaguzi huko Tarime.

Vita vya kabila na koo vimekuwa vikiendelea huko Tarime kwa muda mrefu sana! Je, ni kwanini hao wanaojidai ku-adress hili issue hivi sasa walikuwa kimya muda wote huo? Why now? Why are they playing politics na maisha ya wananchi wa Tarime? Why?

Coz kumekuwa na habari za kipumbavu sana lately kwenye vyombo mbalimbali vya habari ambazo lengo kuu ni kuipaka Tarime matope Kwasababu tu Tarime imeikataa CCM.

Mfano, akizungumza na Alasiri, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bw. Pius Msekwa, alikariiwa jana akisema, "Kampeni zinaendelea vizuri, lakini huku kuna mapigano ya kikabila, hivyo ulinzi mkali unahitajika, maana unaweza ukawa katika kata hii, ukasikia katika kata nyingine yamezuka mapigano."

Lakini ukweli ni kwamba: Hivi sasa hakuna mapigano ya kikabila huko Tarime. In fact, CCM ndiyo inayotumia vitisho na nguvu kunyamazisha wale wasiokubaliana na sera zake huko Tarime. And I'm not confused about this. P'se follow me closely:

Gazeti la Alasiri, 2008-09-29 15:59:09: Watu wanne walikamatwa jana katika kijiji cha Nyamongo, kutokana na kuwazomea viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, waliokuwa wakifanya mkutano wa kampeni kijijini hapo.

Think of it, Queen mwenyewe anazomewa!

Let me tell you something here: This whole thing of "Tarime Ngoma nzito," "Tarime hakukaliki," " Risasi zavuma Tarime," you always read/hear in the media is just a lie. Lie, Lie, lie.

Thanks.

Gustanza,

Kama vile walivyoaibika wakati wa msiba wa Wangwe, watazidi tu kuaibika wale wote wanaoleta uchafuzi na habari za majungu kwa misingi ya kisiasa na ufisadi.

Wana Tarime wako makini na hawachukulii mambo juu juu kama mafisadi wote wanavyodhani. Makamba anaambia watu kuwa ccm ndiyo inapesa za kuleta maendeleo jimboni at the same time Msekwa na wengine wakisema kuwa JK amewatuma kuangalia kama kuna machafuko Tarime ili JK achukue hatua za kijeshi - kama ccm wanafikia mambo this low, basi kuna kazi kweli tuendako.
 
Poti,

Mbona una hasira sana leo? Watu wa Tarime wamekukosea/kunyima nini mpaka uwe na big time interest na kugombana na wachangiaji hapa?

Ongea hoja zako zieleweke maana hii inachanganya kujua unasimama wapi kwenye issues hapa.

Hapana poti.

Mimi mara nyingi hua tunabishana tu hata kama unaona hazimeki sense huna haja ya kuanza kutukana watu.
Poti wewe tumetofautiana sana bila mgogororo wowote ILA kuna watu hapa hoja zao mpaka waanze kuita watu majina na kutukana .Angalia nani kaanza na mara nyingi ndio tabia zao.

Kama huyu LUnyungu anadaganya mke wa mtu kua yeye ni koshula ,Harafu anakuja kuzomea viongozi wengine nimemuheshimu siku nyingi lakini naona yeye hawezi kujiheshimu Na Asirudi moshi.

Watu wa tarime wanikosee mimi nini poti .Ninachopingana hapa Watu wengine wapondwe mawe na kumwagiwa pilipili waseme midomo ndio imewaponza ,wakipigwa wao waseme kampeni chafu .HUU uhuni Poti.

Mtu akikukosea mpeleke ktk vyombo husika na ukamua kumpiga watu wanaofuata sheria lazima wakulaumu wewe LAkini wakiamua kushangilia na wao siku yakiwakuta wengine wana haki ya kushangilia pia.
 
makap nadhani jikite kwenye hoja na uachane na huu uzushi .Useme tu mapenzi yako kwa CCM iwe clear lakini do not mix up things .Konsula ni jambo kubwa hata mjumbe wa nyumba kuni anajulikana itakuwa mtu kujiiita konshula ina maana kweli huna hoja ama umeamua kufanya maajabu ?
 
Lunyungu.
wewe kaa chini na wala usiseme kitu. kuendelea kubisha utasababisha aibu bure
 
Lunyungu.
wewe kaa chini na wala usiseme kitu. kuendelea kubisha utasababisha aibu bure

Nashauri jikite kwenye hoja badala ya kuanza mambo ya ya ajabu ndiyo ushauri wangu .
 
Gustanza,

Kama vile walivyoaibika wakati wa msiba wa Wangwe, watazidi tu kuaibika wale wote wanaoleta uchafuzi na habari za majungu kwa misingi ya kisiasa na ufisadi.

Wana Tarime wako makini na hawachukulii mambo juu juu kama mafisadi wote wanavyodhani. Makamba anaambia watu kuwa ccm ndiyo inapesa za kuleta maendeleo jimboni at the same time Msekwa na wengine wakisema kuwa JK amewatuma kuangalia kama kuna machafuko Tarime ili JK achukue hatua za kijeshi - kama ccm wanafikia mambo this low, basi kuna kazi kweli tuendako.

Unachosema ni kweli mkuu. The truth is, CCM wanajua kuwa watapoteza jimbo la Tarime tena. So wanachofanya hapa ni kutaka ku-create narratives ili wakishindwa, waseme kulikuwa na fujo/vita/machafuko Tarime, kisha wakate rufaa ili matokeo yatenguliwe. Same game Warioba aliyomchezea Wasira mwaka 1995 [wakati Wasira bado akiwa NCCR].
 
Nashauri jikite kwenye hoja badala ya kuanza mambo ya ya ajabu ndiyo ushauri wangu .

Usirudie tena kuita watu majina ya ajabu ajabu,Na ujenge hoja na ukiona hoja za wenzako ni makapu basi uzichalenji kwa hoja zako makini,kua makini
 
Usirudie tena kuita watu majina ya ajabu ajabu,Na ujenge hoja na ukiona hoja za wenzako ni makapu basi uzichalenji kwa hoja zako makini,kua makini

Acha kujibaraguza na kujishebedua. Rudi kwenye hoja. Mjadala unahusu Mtikila kupigwa Tarime? Kamuulize, anaendelea na maneno yake? Polisi si walisema akirudia watamkamata na yeye akasema atarudia?

Asha
 
Sasa hii hapa mnaripoti habari za Tarime au mnacreate credibility ya habari kwa kuwa mko Tarime na mna ndugu Tarime??? bado sijawaelewa hapa!
 
Sasa hii hapa mnaripoti habari za Tarime au mnacreate credibility ya habari kwa kuwa mko Tarime na mna ndugu Tarime??? bado sijawaelewa hapa!

very good question........it deserve a good answer. maana tunashidwa kuelewa issue ni mapungufu ya media au ni swala la siasa chafu za vyama huko tarime?? au issue ni rushwa kwa wandishi! what is the point....?tusaidiane ili twende sawa
 
Respect kwenu wakuu,

Mkamap,huo unazi wako siku moja utakutokea puani.Kama hutaki kuingia ktk mjadala kaa mbali na kompyuta au sijui simu yako hiyo.

Btw;
Wakuu mimi narudia tena ktk mazingira ambayo unaona polisi wanatumika agaist haki zetu sisi wananchi ni bora kuchukua hatua sisi wenyewe.Kama jeshi la polisi tunalilipa kwa kutumia kodi zetu sisi wananchi ili watulinde na badala yake wanakubali kutumika kama jumuiya ya chama cha Magabachori ni bora tuaamke kudhibiti hizi dhuluma.Sipendi siasa za vurugu lakini ikibidi au kama mzalendo na mpenda haki nikishindwa kufanya mabadiliko ninayotaka in a peacefully way then lazima niyafanye katika mazingira yoyote.

Leo hii tunalilia kuburuzwa na Kenya kiuchumi lakini sisi bado tunafumbia macho huu upuuzi,leo hii Waziri wa nishati na madini yupo Tarime kwenye kampeni kushirikia na wezi wa raslimnali zetu ili kumchagua mfisadi mwingine wa kuruhisisha unyonyaji wao ktk hilo jimbo.Ngeleja ameacha majukumu yake ya kututatulia mataizo ya umeme ambao ni kiungo kikubwa katika ukuaji wa uchumi wetu ili tusiburuzwe tena na kenya,badala yakeanaenda kufanya kazi za chama,hapa inabidi akirudi Dar Es salaam awajibishwe moja na ninatoa wito kwa wananchi wa Tarime waanze kumuwajibisha kwani sasa huko huyo ndiyo kiini cha matatizo yenu.

Siasa za hujuma hazina tija,Nguvu ya umma ifanye kazi dhidi ya serikali au dola iliyoshindwa .

Salute kwa wanatarime,Revolution Forever!
 
Habari za leo zinasema kuwa mgao wa umeme umefikia kikomo baada ya mafundi wa umeme kutoka marekani kuwasili na kutengenza mtambo mmoja wa kuzalisha megawatti 40 ukijumuisha na 72 za awali mnakuwa pouwa.

Ngereja na wenzie lazima wa mlete uku...si unajua baada ya tarime mpaka nyamwaga umeme unaishia hapo?So wanahitaji mut kama ngereja aje maeneo ya kama nyamogo...nyekunguru na vijiji vingine...kueleza wataletaje umeme maeneo hayo...kwa sasa nguzo ziko daraja la mto mara...kuja maeneo twajwa juu....

Kingine Chadema wanasema kuwa wanasomesha watoto bure lakini hizo pesa hazitumiki kumalizia shule wanazosoma watoto wao...kwa kigezo kuwa hiyo ni kazi ya serikari...sasa wanasoma kwenye madarasa yenye madirisha wazi na kibaridi cha tarime plus mvua ya upepo.Hivi si kila sehemu watu wanachangia ujenzi wa shule?kwanini chacha alikuwa anawakataza wasichange?

Hizi ndio siasa?
 
Lunyugu
nilikua naona wewe sijui unalaumu viongozi kwa sababu zipi?na wewe tunafahamu zako natunakufahamu vizuri sana

Unafahamu wewe ulitaka kuvunja ndoa ya watu na bahati yako siku hizi hutokei moshi
ulitaka kuvunja ndoa ya watu kwa kufanya mavituz na mke wa watu pale Arusha.
Bado unabisha !!!kwa kushambulia watu wengine vinara lakini ninyi ndio walewale na ndio maana nasema CHADEMA ni kama CCM wala sio chama mbadala wala nini MAFISADI tu wote.

mkuu hii sasa mpya lakini si ungemfaata private na kisha uka sms....
Au anzisha thread ingine ya kumchambua Lunyungu.
 
mkuu hii sasa mpya lakini si ungemfaata private na kisha uka sms....
Au anzisha thread ingine ya kumchambua Lunyungu.

mkuu,

Hapa jamvini tuna watu wa kila aina,sijui private messages hazina umuhimu! Sometimes unaweza fikiria kushauri uongozi wa JF uongeze masharti ya kuwa NI LAZIMA MTU ANAYEINGIA HAPA AWE NA AKILI TIMAMU,

Mkuu bila hivyo ni kazi kweli kweli tutakuja kujikuta tuna Mtikila,makamba na wafuasi wao hapa.kwi kwi kwi!
 
•
Familia ya Wangwe yamjia juu Slaa

Na Waandishi Wetu

FAMILIA ya aliyekuwa mbunge wa Tarime, marehemu Chacha Wangwe, imesema inamtambua Bibi Mariam, kuwa miongoni mwa wajane watatu wa marehemu ndugu yao.

Na imemtaka Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilbroad Slaa, kutorudia kutamka kuwa mwanamke huyo hakuwa mke halali wa marehemu.

Akizungumza na gazeti hili Dar es Salaam jana, msemaji wa familia hiyo Profesa Samwel Wangwe, alimtaka Dkt. Slaa kuacha kuingiza siasa katika familia yao na kama alitaka kujua alipaswa kuuliza.

"Yule (Mariam) ni mke wa mdogo wetu, yeye (Dkt Slaa) hapaswi kuhoji mambo ya familia," alisema na kusisitiza kuwa familia inamtambua. Alisema wake wote watatu wa marehemu Wangwe waliolewa kwa ndoa ya kimila na kulipiwa mahari, hivyo alimalizana na wazazi wao.

Alisema anaamini Dkt. Slaa amekosea kwa kutoa kauli hiyo na anaamini kuwa hatarudia kutoa maneno ya aina hiyo.

Kauli hiyo ya Profesa Wangwe iliungwa mkono na mdogo wake, Bw. Gideon Wangwe, ambaye alimtaka Dkt. Slaa kuacha mara moja kuingilia masuala ya familia kwa kuwa Bibi Mariam alikuwa mke halali wa marehemu ndugu yao.

"Dkt. Slaa ameanza kuwa mwongo, kwa sababu huyo anayemsema ndiye anaishi na watoto wote tisa na ni ndiye anayewasomesha," alisema na kusisitiza kuwa wanamtambua kwa muda mrefu kuwa ni mke wa marehemu Wangwe.

"Kama anasema si mkewe basi awataje wale anaowafahamu ... ana ushahidi gani kuwa yeye si mke wa marehemu?," alihoji Profesa Wangwe na kuongeza kuwa kutokana na kauli yake hiyo, kwa sasa familia inafikiria kumpeleka mahakamani, kwa kuwa ameanza kudhalilisha familia na kutumia kifo cha ndugu yao kujitafutia umaarufu kisiasa.

Kwa upande wake, Bibi Mariam alisema madai yaliyotolewa na Dkt. Slaa dhidi yake kuwa si mke halali wa marehemu, inaonesha kuwa ni mwendelezo wa chuki dhidi ya familia yao hata baada ya kifo cha Bw. Wangwe.

Aliitafsiri kauli hiyo kuwa "ni ya kihuni na ya kike, kwani haikutakiwa kutolewa na mtu kama Dkt. Slaa, ambaye aliwahi kuwa padri.

"Kama anasema mimi sikuwa mke wake, aeleze yeye alihudhuria harusi ya nani kati ya wake watatu kati ya Ghati, Dotto na mimi (Mariam), wakati ndugu walioshiriki kunilipia mahari wananitambua," alisema Bibi Mariam.

Alisema Dkt. Slaa anapaswa kutambua kuwa hoja iliyopo mbele yao si nani mke wa marehemu, bali ni utata uliogubika mazingira ya kifo cha mumewe.

Huku akionekana wazi kukerwa na kauli hiyo, Bibi Mariam alisema hata wao wakiamua kumchambua Dkt. Slaa, si msafi, lakini hawawezi kufanya hivyo kwa sababu watakuwa wakifanya mambo aliyoyaita ya kike.

Alisema kama anasema yeye si mke halali wa marehemu ilikuwaje kifo kilipotokea alipewa nafasi ya kutambua mwili na kusimamia kazi ya uchunguzi iliyokuwa ikifanywa na madaktari.

"Dodoma aliniona nikiutambua mwili wa marehemu, iweje sasa ananikana?," alihoji na kuongeza kuwa hata kwenye mikutano ya CHADEMA alikuwa akipewa nafasi ya kujitambulisha kama mke wa marehemu Wangwe na Dkt. Slaa alikuwa akiona, iweje ahoji sasa?," alihoji.

Alimtahadharisha kuwa hizo siri ambazo Dkt. Slaa anadai atazitoa dhidi yake, awe na uhakika nazo vinginevyo akiendelea kumchafua, atamburuta mahakamani.

"Atakachokisema awe na uhakika, vinginevyo 'nitakufa' naye mahakamani," alisema na kusisitiza kuwa hawezi kunyamaza kutokana na vitisho vya Dkt. Slaa, badala yake ajiulize yale anayosema ana uhakika nayo vipi ndani ya jamii.

"Mimi ninachokisema kina maslahi kwa familia, aliyekufa ni mume wangu nataka uchunguzi ufanyike ili kuondoa majungu," alisema na kuongeza kuwa tangu kifo cha mumewe kitokee, hajawahi kusema kitu chochote hadi alipozungumza na waandishi wa habari Ijumaa wiki iliyopita.

Kuhusu kauli ya Spika wa Bunge, Bw. Samuel Sitta ya kupuuza ombi lake la kutaka aunde Tume ya kuchunguza kifo cha marehemu Wangwe, alisema hakutarajia majibu yaliyotolewa na Spika.

"Kama anaona nilikosea, alipaswa kunishauri, anajua uchungu nilionao na yeye alikuwa na uchungu mwingi na alilia sana siku ya msiba, sasa leo anataka kutuambia uchungu aliokuwa nao umekwenda wapi?," alihoji Bibi Mariam.

Alisema kauli ya Bw. Sitta kuwa Bunge lisitwishwe mzigo wa kuchunguza kifo hicho, inalenga kuonesha kuwa leo hii kifo cha mumewe kimeishageuka mzigo kwa Bunge.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita, Bibi Mariam aliomba kufanyika upya kwa uchunguzi wa kifo cha mumewe. Pia alidai viongozi wa CHADEMA wamemtelekeza.

Wakati huo huo, viongozi wa CHADEMA wilaya ya Kinondoni, wamemtaka Dkt. Slaa kumwomba radhi mjane huyo, kutokana na kauli aliyoitoa kuwa hamtambui kama mke wa marehemu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa Vijana wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Maulid Mkwanja, alisema umoja huo umesikitishwa na kauli ya Dkt. Slaa kwa sababu Bi. Mariam anatambulika kama mke wake tangu zamani.

"Tangu zamani anafahamika kuwa ni mke wa marehemu Wangwe na kila alipokwenda iwe kwenye mikutano ya kichama alitambulishwa kuwa ni mke wake, iweje leo hii wamkane?," alihoji Bw. Mkwanja na kuongeza:

"Sisi kama chama wilaya, tunamtaka Dkt. Slaa amwombe radhi huyo mjane na kama hatafanya hivyo, watakutana ili kujua hatua za kuchukua."

Alisema kama Dkt. Slaa alikuwa na chuki binafsi na marehemu Wangwe asiziingize kwa mkewe au familia yake.

Kiongozi huyo alimtaka Dkt. Slaa awe anatafakari kauli zake kabla ya kuzitoa hadharani kwa sababu amemdhalilisha Bibi Mariam na watoto wake kwa ujumla.

Akizungumzia kauli ya Spika Bw Sitta, aliyoitoa baada ya mjane huyo kumwomba aunde Tume, alisema haikuwa busara kumwambia kuwa amekurupuka, bali alitakiwa kumsaidia.

"Alitakiwa amsaidie kwa kuunda Tume kwa kuzingatia kuwa kifo chake kiligubikwa na mazingira ya utata," alisema.

Dkt. Slaa alikaririwa akisema hawamtambui mjane wa Wangwe, Bibi Mariam aliyeomba kufanyika kwa uchunguzi upya, kwani wake za marehemu wanaowatambua wako Tarime.

Dkt. Slaa kupitia taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) juzi alimtaka mjane huyo kuweka wazi ni kwa vipi CHADEMA haikushiriki mazishi ya Wangwe.

Marehemu Wangwe alikufa katika ajali ya gari iliyotokea Julai 28 mwaka huu, wilayani Kongwa eneo la Pandambili mkoani Dodoma akiwa njiani kuelekea Dar es Salaam.

Mazingira ya kifo chake yalizua utata ambapo hadi sasa baadhi ya watu hawaamini kama alikufa kifo cha ajali ya kawaida.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom