Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Mkuu,

Kama huamini sera za jino kwa jino mbona unazishabikia? Acha usanii bro,tumeshakushtukia.

Katika maelezo yako hapo juu,hoja iko wapi mkuu? kwi kwi kwi!

Ben,

Inaelekea tatizo lako ni Mtanzania, uko tayari kupotosha kila kitu. Wapi mimi nimeshabikia sera za jino kwa jino? Highlight hata sehemu moja ambapo nimeshabikia vurugu. Kuanzia leo sitachangia tena hoja yako yoyote maana hakuna tija. Mijadala ikigeuka kuwa Ben au Mtanzania inakuwa haina tija tena. Nimekubali kutokukubaliana na wewe na sio mwisho wa dunia. Afadhali kutumia muda wangu kwa mambo yanayoongeza tija kuliko ubishi usio na maana yoyote. I am not prepared to go that low!
 
Sio Ben, ongeza na Asha. Wewe ulikuwa mtetezi wa mafisadi. Ila nakupongeza umebadilika taratibu unaanza kuwa neutral na kuwaacha wakina Masatu na Mkamap wakiendelea na kazi yao.

Hebu soma mwenyewe michango yako ya nyuma utajiona.
 
Assha unasema kwamba Mtanzania amefanyaje ?
 
Sio Ben, ongeza na Asha. Wewe ulikuwa mtetezi wa mafisadi. Ila nakupongeza umebadilika taratibu unaanza kuwa neutral na kuwaacha wakina Masatu na Mkamap wakiendelea na kazi yao.

Hebu soma mwenyewe michango yako ya nyuma utajiona.

Asha,

Utaisaidia JF na majadiliano kama utatoa mifano. Kwa mfano ungesaidia mjadala huu kama ungetumia hata dakika zako chache kutafuta maandishi yangu yanayotetea mafisadi na ukatoa kama mfano.

Haya mambo ya kuja na tuhuma kubwa bila hata kufanya jitihada ndogo ya kuambatanisha na ushahidi inaishusha mno JF.

Naamini dada Asha ni msomi, na msomi yoyote anajua umuhimu wa data kabla ya kutoa conclusion. Kwa faida ya JF nakuruhusu tafuta maandishi yangu yanayotetea mafisadi.

Kitu ninachotofautiana na baadhi ya watu hapa ni ile dhana ya kwamba ukimpinga Mbowe/Slaa basi wewe ni mtetezi wa mafisadi. Mambo kama hayo yamemshinda Bush na ujinga wake wa you are either with us or the terrorists. Dunia sio black and white kama tulivyokuwa tunaambiwa zamani.

Niko tayari kujadiliana na mtu yeyote anayejadili hoja lakini mambo ya kugeuka personal na mtu ambaye hata simjui ni ujinga mtupu na pia ni kupoteza muda. Kwenye change tunaamini ni kupoteza muda kujaribu kumbadili mtu ambaye unajua hawezi kubadilika. Badala yake ni muhimu kutumia hiyo nguvu kwa watu wa katikati ambao kuna uwezekano wa kubadilika.
 
Mfano ni kuwa wewe umekuwa ukimtetea fisadi mtikila swahiba wa fisadi Rostam Aziz. Unapindisha maneno kwa njia ambayo wengine hawawezi kugundua. Hufanyi wazi wazi kama Masatu na Mkamap

Asha
 
Mfano ni kuwa wewe umekuwa ukimtetea fisadi mtikila swahiba wa fisadi Rostam Aziz. Unapindisha maneno kwa njia ambayo wengine hawawezi kugundua. Hufanyi wazi wazi kama Masatu na Mkamap

Asha

Kumbe Mtikila naye fisadi? Mimi siwezi kumweka Mtikila kwenye kundi la mafisadi japo pia siwezi kuweka kwenye kundi la waadilifu, ni mganga njaa hapo katikati.

Lakini pia kupinga watu kumpiga Mtikila haina uhusiano na kutetea ufisadi. Hata ingelikuwa MKapa au Ballali kapigwa bado ningeandika vile vile kama nilivyoandika kwa Mtikila. Naheshimu utawala wa sheria na sio watu kujichukulia madaraka mikononi mwao.

Mnapotosha kabisa maana ya neno fisadi, sishangai siku hizi hata katibu wa kijiji akifanya kosa anaambiwa ni fisadi. Itafika mahali hilo neno litachuja kiasi kwamba halitaumiza mtu tena, maana kila mtu ataitwa fisadi kwa njia moja ama nyingine.

Kama huo ndio ushahidi wako wa mimi kutetea mafisadi basi uko weak kweli kweli, hata kwenye mahakama ya kijiji huwezi kushinda kwi kwi kwi!!!
 
Mfano ni kuwa wewe umekuwa ukimtetea fisadi mtikila swahiba wa fisadi Rostam Aziz. Unapindisha maneno kwa njia ambayo wengine hawawezi kugundua. Hufanyi wazi wazi kama Masatu na Mkamap

Asha

Mbowe anawakopesha lini milion kadhaa mkakodi helkopita kenya ili mje mfanye mshambulizi ya Anga huko Tarime.Harafu mkipata hilo jimbo fedha zote za posho mda wote mlipe deni la Helkopita mpaka 2010 ndio deni liishe.Harafu 2010 mmkope tena mpae na helkopita na deni liishe 2015 harafu 2015 mmkope tena.kwi kwi kwi kwi kwi kwi.

Mkitoka hapo mjiridhishe kwa kusema serikali inaua vyama vya upinzani.Teh teh teh teh teh.

Wapelekeeni Tarime helkopita lifanye maangamizi .
 
Duh kazi kubwa kweli huku Duniani .
Jamani ee tuache malumbano turejee kwenye hoja yenyewe tafadhali .
 
Kumbe Mtikila naye fisadi? Mimi siwezi kumweka Mtikila kwenye kundi la mafisadi japo pia siwezi kuweka kwenye kundi la waadilifu, ni mganga njaa hapo katikati.

Lakini pia kupinga watu kumpiga Mtikila haina uhusiano na kutetea ufisadi. Hata ingelikuwa MKapa au Ballali kapigwa bado ningeandika vile vile kama nilivyoandika kwa Mtikila. Naheshimu utawala wa sheria na sio watu kujichukulia madaraka mikononi mwao.

Mnapotosha kabisa maana ya neno fisadi, sishangai siku hizi hata katibu wa kijiji akifanya kosa anaambiwa ni fisadi. Itafika mahali hilo neno litachuja kiasi kwamba halitaumiza mtu tena, maana kila mtu ataitwa fisadi kwa njia moja ama nyingine.

Kama huo ndio ushahidi wako wa mimi kutetea mafisadi basi uko weak kweli kweli, hata kwenye mahakama ya kijiji huwezi kushinda kwi kwi kwi!!!

Sio kupigwa tu. Ulimtetea kwenye lile sakata ya yeye kuhongwa fedha na Rostam Aziz. Ulisema Mtikila ndio kiongozi bora zaidi wa upinzani.

Kwani hujui kuwa Mtikila ni FISADI?

Asha
 
Sio kupigwa tu. Ulimtetea kwenye lile sakata ya yeye kuhongwa fedha na Rostam Aziz. Ulisema Mtikila ndio kiongozi bora zaidi wa upinzani.

Kwani hujui kuwa Mtikila ni FISADI?

Asha

Kwi kwi kwi!! Dada Asha nakushauri tena soma hiyo posts yangu na ukiweza ilete hapa ili kila mtu aone nilichoandika.

Nilichosema mimi ni kwamba hata Nyerere alienda kukopa IMF pamoja na kwamba aliwachukia IMF na WB. Pia nikasema mwenye njaa ni ngumu sana kuamua akakope wapi.

Ila nilimsifa Mtikila pia kwa kitendo chake cha kwenda kukopa kwa RA na bado akaendelea kumsagia. Ni watanzania wachache sana wana uwezo huo. Ukiwa na pesa TZ unaweza kununua watu wengi sana.

Mimi mwanasiasa ninayemheshimu kuliko wote ni Mrema. Namheshimu kwasababu amewahi kufanya mambo ya maana kwa vitendo tofauti na sisi wengi wetu hapa ambao tunayoyandika na kutenda ni tofauti kabisa.

Hakuna hata sehemu moja nilipowahi kuandika Mtikila ni kiongozi bora kuliko wapinzani wengine.

Uzuri siku hizi tuna google, hivyo nakuruhusu ku search na kujua niliandika kitu gani kuhusu Mtikila. Una uhuru wa kutokukubaliana na mimi lakini huna uhuru wa kupotosha nilichoandika.

Niko very consistent na ninachoandika, na siogopi kuweka mawazo yangu wazi. Najua siku hizi JF kuna jeshi la CHADEMA ambalo halitaki kusikia mawazo mabaya kwa viongozi wao. Ukiandika tofauti na mawazo yao, utaitwa fisadi, huna upeo nk. Binafsi sijali kabisa kushambuliwa ili mradi mtu anishambulie kwa kitu ambacho nimeandika na sio kuanza kuzua.

Ukija kwa hoja kama unavyofanya wewe kwenye hili tutaendelea kujadiliana lakini ukigeuza personal hapo nitaacha maana nisingependa kujiingiza kwenye maugomvi. Hii dunia tayari ina maugomvi mengi na nisingelipenda kuanzisha maugomvi mengine.
 
02.10.2008 0432 EAT
•
CHADEMA wajisalimisha Polisi

Na Richard Mwaikenda, Tarime
Majira

UONGOZI wa CHADEMA umejisalimisha kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, baada ya kusikia kwamba madiwani wao na baadhi ya viongozi wao wanatakiwa kukamatwa kwa tuhuma za kupanga vurugu katika mikutano ya kampeni za udiwani na ubunge wilayani hapa.

Hayo yalitokea jana baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Bw. Stanley Kolimba, kuwambia wanahabari kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Bw. Zitto Kabwe, anatakiwa achunguzwe kutokana na kuhamasisha wafuasi wake kuchoma fulana za CCM katika mkutano wa kampeni wa CHADEMA hivi karibuni kwenye uwanja wa shule ya Nyamisangura.

Pia katika mkutano huo, Bw. Kabwe alisema CCM imepanga na Jeshi la Polisi kukamata madiwani wa CHADEMA kwa madai kwamba ndio wanaopanga kufanya vurugu kwenye mikutano ya kampeni.

Uongozi wa CHADEMA ulijisalimisha huku ukimtaka Mkuu wa Wilaya naye akamatwe ili aeleze jinsi wauaji kutoka Kenya, yaani Mungiki walivyoingia wilayani hapa na nani amewaleta.

Akizungumza baada ya kutoka kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Kampeni za Uchaguzi wa chama hicho, Bw. Msafiri Mtemelwa, alisema mambo mengine waliyoyajadili kwenye mkutano huo, ni kupinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya kukamatwa kwa Bw. Kabwe kwa tuhuma za kutoa amri wafuasi wake kuchoma fulana zenye nembo ya CCM.

Alisema katika mkutano huo, uongozi wa CHADEMA ulitaka pia uelezwe na Jeshi la Polisi kosa walilofanya madiwani wa chama hicho litakalosababisha wakamatwe.

"Tumelitaka Jeshi la Polisi limkamate Mkuu wa Wilaya, aeleze Mungiki wameingiaje Tarime, hivi sasa wako wapi na wameletwa na nani," alisema Bw. Mtemelwa.

"Tumehoji hivyo ili tupate ukweli juu ya jambo hilo ili baadaye isije ikawa njama wakasema kuwa chama chetu ndicho kimewaleta Mungiki," alisema.

Bw. Mtemelwa alisema Jeshi la Polisi limekiri kuwa lina mpango wa kuwakamata madiwani wa chama hicho lakini si kwa lengo la kuwafungulia mashitaka, bali kuwahoji kutokana na taarifa walizopata.

"Vilevile tumewaeleza kuwa Mkuu wa Wilaya, hana mamlaka ya kumkamata Naibu Katibu Mkuu wao, kwani yeye si Polisi hivyo asiingilie kazi ya Jeshi hilo," alisema.

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA, waliohudhuria mkutano pamoja na Bw. Mtemelwa, ni mgombea ubunge, Bw. Charles Mwera na mgombea udiwani, Bw. John Heche.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, Bw. Costantino Massawe, alipotakiwa aeleze mambo waliyoyajadili katika mkutano huo na waliyokubaliana, alikataa kueleza chochote kwa madai kwamba yeye si msemaji, na kutaka taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, isubiriwe.
 
Ben,

Inaelekea tatizo lako ni Mtanzania, uko tayari kupotosha kila kitu. Wapi mimi nimeshabikia sera za jino kwa jino? Highlight hata sehemu moja ambapo nimeshabikia vurugu. Kuanzia leo sitachangia tena hoja yako yoyote maana hakuna tija. Mijadala ikigeuka kuwa Ben au Mtanzania inakuwa haina tija tena. Nimekubali kutokukubaliana na wewe na sio mwisho wa dunia. Afadhali kutumia muda wangu kwa mambo yanayoongeza tija kuliko ubishi usio na maana yoyote. I am not prepared to go that low!

Mkuu,

Sina haja na mchango wako katika hoja zangu. Kwani unadhani usipochangia hoja zangu dunia ita-crush? Ni bora watu wachache wachangie hoja zangu kuliko kuwa na watu wengi kama wewe mkuu,kuna watu ambao wako neutral wanajulikana na niko radhi ku-debate nao kwa kutumia muda mwingi kuliko wewe na unafiki wako wa kujifanya neutral.Kadanganye wengine mkuu.

Kuna watu kama akina Field Marshal Es,Mkandara na akina kichuguu na wengineo wengi unajua wako neutral lakini wewe,mhh! Hata nimekosa hamu kabisa ya ku-debate nawe maanke ni mtu usiyependa ukweli na u-conservative wa kutisha,na dharau nyingi kwa wenzio.Unafikia hatu ya kuwatukana watanzania na viongozi wao kwa kutumia tusi 'Wajinga'.Siko tayari kulumbana na mtu mwenye mawazo ya aina hii.

Unasema tatizo ni Mtanzania,kwani wewe ni celeb kwa nani hasa? Unasema kushusha JF hadhi,huoni wewe ndiye kinara wa kuishusha JF hadhi kwa kutumia tusi kama 'Wananchi na viongozi wa Tanzania ni wajinga'?

Mkuu,unataka JF ionekana sehemu ya kutukana watu?

Sina haja na mchango wako katika hoja zangu lakini nikikukuta unapotosha au unauchafua upinzani kwa sababu ya unazi wako,basi ni mimi na wewe na usilie lie kutafuta sympathy ya wanaJF.Hilo sitasikiliza kama unataka kuwa na michango yenye Tija,toa unazi wako kwanza halafu tusimamie facts.

Unapenda sana kuichafua CHADEMA kwa unazi wako,sitakuacha
 
Mbowe anawakopesha lini milion kadhaa mkakodi helkopita kenya ili mje mfanye mshambulizi ya Anga huko Tarime.Harafu mkipata hilo jimbo fedha zote za posho mda wote mlipe deni la Helkopita mpaka 2010 ndio deni liishe.Harafu 2010 mmkope tena mpae na helkopita na deni liishe 2015 harafu 2015 mmkope tena.kwi kwi kwi kwi kwi kwi.

Mkitoka hapo mjiridhishe kwa kusema serikali inaua vyama vya upinzani.Teh teh teh teh teh.

Wapelekeeni Tarime helkopita lifanye maangamizi .

Si afadhali CHADEMA wanokopa kuliko Hilo jinamizi CCM linalowaibia walalahoi ili kufanya kampeni.At least CHADEMA wanakopa ili kuongeza sauti za watetezi wa Watanzania bungeni ili kupambana na Majambazi ktk bunge.

Kuu,umesoma kutokana na kodi za watanzania na wanategemea a lot from you na sio hizi low unazomwaga hapa.Wewe bado nio mwanafunzi,go back to school bro maana naona unatumia muda wako vibaya kumwaga low hapa badala ya kuutumia vizuri ili kuja kusaidia kuleta mabadiliko au huoni kama kuna haja ya mabadiliko Tanzania? Sijui una tatizo gani kuwashabikia mafisadi na kikwazo kikuu katika kupiga hatua kimaendeleo.Are you out of your mind or what?
 
Tambwe atishia CHADEMA

na Kulwa Karedia

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa siri ya kuwapo mpango wa kukamatwa viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa mbunge wa Chadema, marehemu Chacha Wangwe.

Siri hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Propaganda, Tambwe Hiza, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Itirya.

Tambwe alisema viongozi hao wa juu, watakamatwa baada ya miezi mitatu, kwa madai ya kuhusika na kifo cha Wangwe.

Tambwe alitumia mkutano huo kuzungumzia kifo cha Wangwe na kukihusisha moja kwa moja na viongozi wa Chadema.

Kutokana na hali hiyo, Tambwe amewataka wananchi wa Tarime kuacha kumpigia kura mgombea wa Chadema, Charles Mwera, kwa madai kuwa chama hicho hakina dola na viongozi wake watasambaratika.

Katika hatua nyingine, CHADEMAimemwaga zaidi ya baiskeli 20 zenye thamani ya sh milioni 2.6 katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime, ikiwa ni sehemu ya kurahisisha usafiri kwa mawakala wake, ili waweze kuwafikia wanachama kirahisi katika kampeni zinazoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi baiskeli hizo, makao makuu ya chama hicho mjini hapa jana, Mkurugenzi wa Kampeni na Uchaguzi, Msafiri Mtemelwa, alisema hiyo ni moja ya hatua ya kukabiliana na mbinu chafu zinazofanywa na wapinzani ambao wamekuwa wakipita na kutangaza kwamba chama hicho hakina uwezo.

"Tumeamua kuwawezesha viongozi wetu wa kata ambao tunaamini kwamba wao ndio wako karibu zaidi na wapiga kura wetu... hivyo tumeona vyema kuwapatia baiskeli hizo ili ziwawezeshe kuzunguka maeneo mbalimbali wakati huu wa kampeni," alisema Mtemelwa.

Alisema hiyo ni moja ya hatua ya kuwajengea uwezo ambao utawawezesha kuwafikia kirahisi watu walioko maeneo ya vijijini, ambako usafiri wa magari umekuwa mgumu, kutokana na hali halisi ya kijografia iliyopo wilayani hapa.

"Huu ni mwanzo, tumejipanga vya kutosha kukabiliana na mbinu chafu zilizoandaliwa na baadhi ya wapinzani wetu ambao wanaonekana sasa wanaweweseka kwa kuandaa mbinu za kutaka kutuvurugia mwenendo wetu wa kampeni...naamini lengo letu litatimia tu," alisema Mtemelwa.

Alisema mbali ya baiskeli hizo kutolewa sasa, pia zitatumika katika uchaguzi wa serikali za vitongoji mwaka ujao, hatua ambayo alisema itakuwa imewajengea uwezo wa kusambaza ujumbe maeneo mbalimbali kwa wanachama wao.

Naye Katibu wa chama hicho, Wilaya ya Tarime, Joseph Anthony, aliwapongeza viongozi wa chama hicho kutoka makao makuu kwa hatua ya kutoa baiskeli hizo ambazo alisema zitatumika kama zilivyokusudiwa kwa nia ya kurejesha jimbo ambalo lilikuwa likishikiliwa na marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

Alisema baiskeli hizo zitatumika zaidi maeneo ya vijijini ambako ndiko kuliko na wapiga kura wengi, ambao wamekuwa hawafikiwi kwa usafiri wa magari na badala yake husababisha chama kukosa kura kutoka kwa wanachama wake.

Kuhusu kampeni zinazoendelea hivi sasa, Mtemelwa alisema zinaendelea vizuri licha ya vikwazo mbalimbali ambavyo wamekutana navyo, hasa kutoka kwa Jeshi la Polisi ambalo limekuwa likishindwa kuwachukulia hatua baadhi ya watu ambao huripotiwa kwao.

Alisema mara baada ya kufanya mazungumzo ya kina na viongozi wa jeshi hilo jana, wanaamini kwamba hali itabadilika na kuona haki inatendeka kwa kila chama ili kufikia malengo yaliyokusudiwa hadi siku ya uchaguzi Oktoba 12, mwaka huu.

Katika hatua nyingine, Chama cha TADEA, na UPDP, kimelaani vurugu zinazoendelea katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Tarime na kwamba endapo hali ikiendelea hivyo, kuna hatari ya uchaguzi huo kutofanyika au kuwa uwanja wa mapambano.

Wakizungumza katika mkutano wa pamoja kwa nyakati tofauti uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Tadea, Lifa Chipaka, alisema kuwa vurugu hizo zinachochewa na wanasiasa wenyewe wawapo kwenye mikutano ya kampeni.

Alisema kuwa kila chama kimekuwa na kauli za uchochezi, lakini alilaani kitendo cha Mwenyekiti wa Chama cha Democratic (DP), Mchungaji Mtikila kupigwa, huku baadhi ya viongozi wa CHADEMA, wakiipongeza hatua hiyo.

"Mimi nimeshangazwa sana na kauli ya Zitto Kabwe, kusema kipigo cha Mtikila ni sawa, kwani amezidi kuropoka, hii si sahihi, hatutarajii vyama vya upinzani vishabikie mmoja wao kupigwa," alisema Chipaka.

Naye Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa, alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Tarime kuwa kama Zanzibar ilivyochafuka mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000, ambapo zaidi ya watu 30 waliuawa na wengine kukimbilia Kenya kutokana na machafuko ya kisiasa.

"Sisi hatutaki taifa lipoteze amani, lakini ndiyo maana tunakemea hali hiyo. Yanayotokea Tarime yasipodhibitiwa, yatatokea tena sehemu nyingine. Sasa hii ni hatari," alisema Dovutwa.

Tanzania Daima
 
Kila unaposoma mambo ya Tarime unagundua jinsi nchi yetu na watu wake walivyo wajinga wa kutupwa.

Hivi kweli ingelikuwa kama huku West, Tambwe angepata wapi hata nguvu ya kusimama jukwaani na kusema hayo anayoyasema sasa? Waandishi wangemtolea hotuba zake za huko nyuma alipokuwa upinzani na hapo ndio ungelikuwa mwisho wake.

Hivi mtu unaweza kuzua jambo kubwa kama hili la kusema viongozi wa CHADEMA watakamatwa, bila ushahidi wowote na vyombo vya habari vikaandika?

Kumbe mambo yanayotokea hapa JF ni refection sahihi ya Tanzania na wananchi wake walipofikia.

Kwa Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana katika fikra za watu. Looh! jitihada zote za Nyerere inaelekea tumerudi hatua kumi nyuma, inasikitisha sana!

Kama hizi ndizo siasa, kweli tuna safari ndefu sana.
 
Si afadhali CHADEMA wanokopa kuliko Hilo jinamizi CCM linalowaibia walalahoi ili kufanya kampeni.At least CHADEMA wanakopa ili kuongeza sauti za watetezi wa Watanzania bungeni ili kupambana na Majambazi ktk bunge.

Kuu,umesoma kutokana na kodi za watanzania na wanategemea a lot from you na sio hizi low unazomwaga hapa.Wewe bado nio mwanafunzi,go back to school bro maana naona unatumia muda wako vibaya kumwaga low hapa badala ya kuutumia vizuri ili kuja kusaidia kuleta mabadiliko au huoni kama kuna haja ya mabadiliko Tanzania? Sijui una tatizo gani kuwashabikia mafisadi na kikwazo kikuu katika kupiga hatua kimaendeleo.Are you out of your mind or what?

Na wewe umesomeshwa na kodi za wananchi wa wapi? Mbona unashabikia MIFISADI ya CHADEMA??

Hii MIFISADI ilimtimua Marehemu CHACHA baada ya kuhoji fedha wanazo ZIFISADI MIFISADI ya CHADEMA kwasabu ni full Timu ktk UFISADI na Minyag'au Ikamgeuzia kibao maremu CHACHA nakumuita yeye ni fisadi .

Eti alipofariki hii MIFISADI ya CHADEMA bila aibu kwa kuawa imekomaa ktk UFISADI eti nayo pale ktk MSIBA inasoma wasaa kua MAREHEMU ktk maisha yake alikua mtetezi wa haki na demokrasia YANI kichefuchefu tupu.

Nani wewe alikuambia UHURU na DEMOKRASIA Utaletwa na MIFISADI kutoka CHADEMA hii ya leo??

Ndiyo uhuru unawezwa kuletwa na CHADEMA lakini si kwa kutumia hii MIFISADI iliyopo sasa na mnayoishabikia.
 
Date::10/3/2008
Tarime: Mbwa avikwa fulana ya CCM,mwenye mbwa akamatwa, mbwa auawa
Frederick Katulanda na Mussa Juma, Tarime
Mwananchi

KAMPENI za uchaguzi wa ubunge na udiwani wilayani Tarime zimezidi kuchukua sura tofauti baada ya watu wasiojulikana kumvalisha mbwa fulana yenye picha ya mgombea wa ubunge wa CCM, Christopher Kangoye na kurandaranda naye katika mitaa ya mji wa Tarime.

Kampeni hizo, licha ya kutawaliwa na kashfa na maneno makali kama zilivyo kampeni nyingine za kisiasa, zimekuwa na matukio mengine mengi yakiwemo ya kutunguana kwa mawe, majaribio yasiyofanikiwa ya biashara ya shahada za kupigia kura, kuchoma fulana za vyama na kupigwa mawe kwa gari la kampeni.

Lakini jana matukio hayo yalipanua wigo wake kutoka kwa binadamu aliyejaliwa akili za kujua mema na mabaya hadi kwa hayawani wa kufugwa.

Mbwa aliyekuwa amevishwa fulana ya rangi za kijani na njano yenye picha ya mgombea wa CCM, alionekana kuanzia majira ya saa 1:00 jioni akikatiza mitaa mbalimbali akiwa ndani ya nguo hizo zinazovaliwa na wafuasi wa CCM kumnadi mgombea wao kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika Oktoba 12.

Haikueleweka mbwa huyo alivishwa fulana hiyo na watu gani, lakini polisi imemkamata mmiliki wa mbwa huyo, Robhi Ikwabe ili asaidie upelelezi wa kumnasa mtu aliyehusika na tukio hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Mara, Liberatus Barlow alisema hadi sasa jeshi lake linawashikilia watu watatu ambao wanasadikiwa kuwa walionekana wakiwa wamemshikilia mbwa huyo na kupita naye mitaani kabla ya kumwachia aendelee na safari zake.

Ingawa haijabainika waliohusika walikuwa na nia gani, inasemekana kuwa watu walioshuhudia tukio la mbwa huyo, ambaye baadaye alikimbilia kwa mmiliki wake aliye eneo la kituo cha mabasi jirani na kituo kidogo cha polisi, huenda ni wafuasi wa Chadema kutokana na kudaiwa kuwa walikuwa wakionyesha ishara ya vidole ambayo ni alama ya chama hicho.

Katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba alieleza kusikitisha na hali hiyo na kusema akiwa kama kiongozi mwenye uvumilivu suala hilo anawaachia maamuzi, ambao alisema ni wananchi watakaopiga kura kuchagua viongozi wao.

Alisema kuwa vurugu zinazoendela zinadhihirisha uhuni na kusema CCM ni chama cha wastaarabu, hivyo wanawaachia wananchi.

''Hizi ndizo siasa za wenzetu, sisi tunawaachia wananchi, maana hata sisi tunaweza kufanya hivyo kama tukiamua, lakini tutaonekana wote wendawazimu ndiyo maana nasema nawaachia wananchi wao ndiyo watakaoamua,'' alieleza Makamba.

Alisema ingawa nao wanazo bendera nyingi ambazo zimesalimishwa na wafuasi wengi wa Chadema, hawatathubutu kufanya hivyo.

Naye mgombea ubunge wa Chadema katika jimbo la Tarime, Charles Mwera aliwafukuza polisi katika msafara wake wa kampeni na kuwataka waende kukomesha mapigano ya koo badala ya kutumia fedha za umma kumfuata kwenye mikutano yake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji Masanga juzi, Mwera alisema katika msafara wake hahitaji kundi la askari na magari kama ilivyo sasa kwani kama kuna umuhimu wa kuwa na askari angependa askari wasiozidi wawili.

''Mimi sina shida na askari najua mnatumia mamilioni ya fedha kutufuata, lakini kuna kazi za muhimu za kufanya kuzuia mapigano ya koo na kulinda amani maeneo mbalimbali nchini na sio sasa askari wote kujazana Tarime na badala yake kuwa kero,'' alisema Mwera.

Alisema yeye kama mwenyekiti wa halmashauri ni mkazi wa Tarime na hivyo haoni umuhimu wa kulindwa kwani yupo nyumbani kwake na mikutano yao haina matatizo kutokana na wananchi kufurahia sera za Chadema badala ya kashfa na uchochezi wa vyama vingine.

Akizungumzia migogoro ya kikabila katika wilaya hiyo, alisema kama akichaguliwa atahakikisha inamalizwa kwa mazungumzo na kujiepusha na kufanya kazi kwa misingi ya ukabila.

''Matatizo yenu ya mapigano tutayashughulikia kwa mazungumzo, matatizo ya wizi wa mifugo nayo yatashughulikiwa kwa umakini ili kuhakikisha wilaya hii inakuwa shwari wakati wote,'' alisema Mwera.

Naye, katibu mwenezi wa Chadema, Erasto Tumbo aliwataka wakazi wa Tarime kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kumpigia kura mgombea wa chama hicho bila hofu na kwamba hakuna ambaye anaiba kura zao kama wanavyodhania.

''Ukimaliza kupiga kura kaa mita 100 mbele ya kituo hadi matangazo ya matokeo yatakapobandikwa na wakimaliza sote twende halmashauri kusubiri kutangaziwa mshindi wetu kwani hakuna kulala siku hiyo hadi kieleweke,'' alisema Tumbo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom