Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,193
- Thread starter
- #1,001
Mkuu Ben asante nilikuwa sijaiona .Samahani maana inaonekana nimekurupuka jamani mnisamehe .
Bomba tuu mkuu wangu!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Ben asante nilikuwa sijaiona .Samahani maana inaonekana nimekurupuka jamani mnisamehe .
Mkuu,
Kama huamini sera za jino kwa jino mbona unazishabikia? Acha usanii bro,tumeshakushtukia.
Katika maelezo yako hapo juu,hoja iko wapi mkuu? kwi kwi kwi!
Ben,
Inaelekea tatizo lako ni Mtanzania, uko tayari kupotosha kila kitu. Wapi mimi nimeshabikia sera za jino kwa jino? Highlight hata sehemu moja ambapo nimeshabikia vurugu. Kuanzia leo sitachangia tena hoja yako yoyote maana hakuna tija. Mijadala ikigeuka kuwa Ben au Mtanzania inakuwa haina tija tena. Nimekubali kutokukubaliana na wewe na sio mwisho wa dunia. Afadhali kutumia muda wangu kwa mambo yanayoongeza tija kuliko ubishi usio na maana yoyote. I am not prepared to go that low!
Sio Ben, ongeza na Asha. Wewe ulikuwa mtetezi wa mafisadi. Ila nakupongeza umebadilika taratibu unaanza kuwa neutral na kuwaacha wakina Masatu na Mkamap wakiendelea na kazi yao.
Hebu soma mwenyewe michango yako ya nyuma utajiona.

Asha,
Utaisaidia JF na majadiliano kama utatoa mifano. Kwa mfano ungesaidia mjadala huu kama ungetumia hata dakika zako chache kutafuta maandishi yangu yanayotetea mafisadi na ukatoa kama mfano.
Haya mambo ya kuja na tuhuma kubwa bila hata kufanya jitihada ndogo ya kuambatanisha na ushahidi inaishusha mno JF.
Naamini dada Asha ni msomi, na msomi yoyote anajua umuhimu wa data kabla ya kutoa conclusion. Kwa faida ya JF nakuruhusu tafuta maandishi yangu yanayotetea mafisadi.
Kitu ninachotofautiana na baadhi ya watu hapa ni ile dhana ya kwamba ukimpinga Mbowe/Slaa basi wewe ni mtetezi wa mafisadi. Mambo kama hayo yamemshinda Bush na ujinga wake wa you are either with us or the terrorists. Dunia sio black and white kama tulivyokuwa tunaambiwa zamani.
Niko tayari kujadiliana na mtu yeyote anayejadili hoja lakini mambo ya kugeuka personal na mtu ambaye hata simjui ni ujinga mtupu na pia ni kupoteza muda. Kwenye change tunaamini ni kupoteza muda kujaribu kumbadili mtu ambaye unajua hawezi kubadilika. Badala yake ni muhimu kutumia hiyo nguvu kwa watu wa katikati ambao kuna uwezekano wa kubadilika.
Mfano ni kuwa wewe umekuwa ukimtetea fisadi mtikila swahiba wa fisadi Rostam Aziz. Unapindisha maneno kwa njia ambayo wengine hawawezi kugundua. Hufanyi wazi wazi kama Masatu na Mkamap
Asha
Mfano ni kuwa wewe umekuwa ukimtetea fisadi mtikila swahiba wa fisadi Rostam Aziz. Unapindisha maneno kwa njia ambayo wengine hawawezi kugundua. Hufanyi wazi wazi kama Masatu na Mkamap
Asha
Kumbe Mtikila naye fisadi? Mimi siwezi kumweka Mtikila kwenye kundi la mafisadi japo pia siwezi kuweka kwenye kundi la waadilifu, ni mganga njaa hapo katikati.
Lakini pia kupinga watu kumpiga Mtikila haina uhusiano na kutetea ufisadi. Hata ingelikuwa MKapa au Ballali kapigwa bado ningeandika vile vile kama nilivyoandika kwa Mtikila. Naheshimu utawala wa sheria na sio watu kujichukulia madaraka mikononi mwao.
Mnapotosha kabisa maana ya neno fisadi, sishangai siku hizi hata katibu wa kijiji akifanya kosa anaambiwa ni fisadi. Itafika mahali hilo neno litachuja kiasi kwamba halitaumiza mtu tena, maana kila mtu ataitwa fisadi kwa njia moja ama nyingine.
Kama huo ndio ushahidi wako wa mimi kutetea mafisadi basi uko weak kweli kweli, hata kwenye mahakama ya kijiji huwezi kushinda kwi kwi kwi!!!
Sio kupigwa tu. Ulimtetea kwenye lile sakata ya yeye kuhongwa fedha na Rostam Aziz. Ulisema Mtikila ndio kiongozi bora zaidi wa upinzani.
Kwani hujui kuwa Mtikila ni FISADI?
Asha
Ben,
Inaelekea tatizo lako ni Mtanzania, uko tayari kupotosha kila kitu. Wapi mimi nimeshabikia sera za jino kwa jino? Highlight hata sehemu moja ambapo nimeshabikia vurugu. Kuanzia leo sitachangia tena hoja yako yoyote maana hakuna tija. Mijadala ikigeuka kuwa Ben au Mtanzania inakuwa haina tija tena. Nimekubali kutokukubaliana na wewe na sio mwisho wa dunia. Afadhali kutumia muda wangu kwa mambo yanayoongeza tija kuliko ubishi usio na maana yoyote. I am not prepared to go that low!
Mbowe anawakopesha lini milion kadhaa mkakodi helkopita kenya ili mje mfanye mshambulizi ya Anga huko Tarime.Harafu mkipata hilo jimbo fedha zote za posho mda wote mlipe deni la Helkopita mpaka 2010 ndio deni liishe.Harafu 2010 mmkope tena mpae na helkopita na deni liishe 2015 harafu 2015 mmkope tena.kwi kwi kwi kwi kwi kwi.
Mkitoka hapo mjiridhishe kwa kusema serikali inaua vyama vya upinzani.Teh teh teh teh teh.
Wapelekeeni Tarime helkopita lifanye maangamizi .
Si afadhali CHADEMA wanokopa kuliko Hilo jinamizi CCM linalowaibia walalahoi ili kufanya kampeni.At least CHADEMA wanakopa ili kuongeza sauti za watetezi wa Watanzania bungeni ili kupambana na Majambazi ktk bunge.
Kuu,umesoma kutokana na kodi za watanzania na wanategemea a lot from you na sio hizi low unazomwaga hapa.Wewe bado nio mwanafunzi,go back to school bro maana naona unatumia muda wako vibaya kumwaga low hapa badala ya kuutumia vizuri ili kuja kusaidia kuleta mabadiliko au huoni kama kuna haja ya mabadiliko Tanzania? Sijui una tatizo gani kuwashabikia mafisadi na kikwazo kikuu katika kupiga hatua kimaendeleo.Are you out of your mind or what?
si kuna thread ya Uchaguzi Tarime au?