Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Ubunge Tarime: Wagombea, Kampeni na Uchaguzi

Status
Not open for further replies.
Kwani mbwa haliwi??

You are right! Basi kama analiwa,hasira za kumuua kikatili zinatoka wapi? Yaani kavalishwa fulana mtu unakurupuka na kumuua? kumbe hata kuliwa analiwa? sasa udhalilishaji unakuja je hapo mkuu? Teh teh teh!
 
Hivi kweli vurugu zinaongeza kura zozote? Hivi hatuoni dalili zote zinazoonyesha tunaelekea walikofika Kenya?

Mheshimiwa Masha, shusha jeshi lote la polisi huko Tarime ili kuokoa maisha na mali ya watu. Watu maskini hatutakiwi kabisa kujiingiza kwenye vitu vya kijinga hivi. Umaskini mwingine ni wa kujitakia kabisa. Wakati Tarime mnatiana mapengo na kuharibiana mali, hawa wanasiasa ikifika tarehe 13/10 wanarudi kwao kwenye familia zao huku wamewaachieni machangu kwenu.

Inasikitisha sana!

sasa mbona unam-critisize Bush kila siku,kumbe mawazo yako yako hivyo hivyo? Hakli ya Tarime inahitaji kutulizwa kwa busara kuliko kutumia nguvu.Hayo ni maamuzi ya kiimla,eti ashushe Jeshi lote? so,uchaguzi mkuu ujao,tutaita vikosi vya kulinda amani vya Au au itakuawaje maanke nchi nzima polisi wetu na jeshi hawatatosha.Je likipelekwa jeshi Tarime na vijana wakaamua kupambana na polisi na damu nyingi ikamwagika,je wewe na Masha kweli mtakua mmefanya uamuzi wa busara?
 
•
Kampeni Uchaguzi Tarime ni tifu souurce:Majira

Habari Zinazoshabihiana
• Mtikila aonywa juu ya kampeni Tarime 19.09.2008 [Soma]
• NEC: Jina la Wangwe litumiwe kwa uangalifu 01.10.2008 [Soma]
• CCM yagaragaza tena CHADEMA, NCCR 29.02.2008 [Soma]

Na Waandishi Wetu, Tarime

WIKI moja kabla ya kufanyika uchaguzi mdogo katika jimbo la Tarime, hali ya mambo imezidi kuwa tete, kampeni hizo zikigubikwa na vurugu, uchomaji moto wa sare za vyama, mapigano na sasa hofu imetanda baada ya kuibuka polisi ambao hawana namba za jeshi hilo.

Kutokana na hali ya vurugu, baadhi ya wanadiplomasia wameamua kujitosa kutuliza hali ya munkari inayozidi kuashiria kuvunjika kwa amani siku hadi siku.

Hali ya hofu ya kuhujumiwa nayo imekifanya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kumwandikia barua Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali Said Mwema kulalamika.

Katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba na. CDM/KW/UCH/VOL.1/072/08 kwenda kwa pamoja na Bw. Mwema, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Kamanda wa Polisi wilayani Tarime, chama hicho kimeonesha hofu juu ya kuwepo kwa askari wasio na namba zozote kikidai wanaweza kuwa makada wa CCM waliovalishwa nguo hizo kwa malengo maalum.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Bw. Chacha Okong'o kwa niaba ya Katibu wa chama hicho Wilaya ya Tarime, CHADEMA wamesema iwapo askari hao wanatambulika basi wanafanyakazi kinyume cha sheria kwa kutokuwa na namba.

"Tuna wasiwasi mkubwa kuwa askari hawa kutokuwa na namba zao za kazi ni kuficha wasitambulike hata pale ambapo watakapokuwa wamefanya uonevu kwa wananchi kipindi hiki cha kampeni na siku ya upigaji wa kura," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Sanjari na barua hiyo, CHADEMA pia wamelilalamikia Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuwachukulia hatua baadhi ya watu waliodai ni wafuasi wa CCM ambao waliwateka wafuasi wa chama hicho na kuwapiga hadi kuwajeruhi hadi walipookolewa na wananchi wengine.

Katika barua yao kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, yenye kumbukumbu na. CDM/KW/UCH/VOL.1/071/2008, chama hicho kimesema Septemba 3 mwaka huu watu hao waliwateka vijana hao wafuasi wa CHADEMA na kwenda kuwapa kipigo kwa madai ya kutowaunga mkono.

Barua inaeleza baada ya kufanya unyama huo,wananchi walipata taarifa na kwenda kuwaokoa kisha kuwapeleka polisi ili wapewe fomu maalum namba 3 kwa ajili ya matibabu lakini badala yake, polisi waliwapokea na kuwaweka rumande bila ya kosa.

CHADEMA wanalalamika kupitia barua hiyo kuwa baada ya polisi kubaini kosa hilo, wamefanya kituko katika utawala bora kwa kuwabambikia kesi ya kumvalisha jezi mbwa wakati vijana hao hawakuwa wakishikiliwa kwa suala hilo.

Juzi mbwa aliyeonekana kuvikwa bendera ya CCM iliyokuwa na picha ya mgombea wa ubunge wa chama hicho, alizua tafrani katika kampeni zinazoendelea na kusababisha vyama kutupiana lawama kwa kampeni chafu.

Barua hiyo zaidi inasema pamoja na vijana hao kubambikiwa kesi ya kumvika mbwa bendera lakini awali walishawatambua watatu kati ya watu nane waliohusika kuwateka, lakini hadi sasa polisi wameshindwa kuwakamata watuhumiwa.

"Walitekwa na watu 8 na kuwaingiza katika gari aina ya Nissan Patrol nyeusi (mali ya mmoja wa viongozi wa CCM), gari hili limekuwa pia likitumiwa na Jeshi la Polisi kubeba askari wake kitendo ambacho tayari tumekilalamikia," ilisema barua hiyo.

Hata hivyo alipoulizwa kuhusu malalamiko hayo ya CHADEMA na Majira Jumapili kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Kikosi cha Operesheni Maalum, Bw. Venance Tossi alionekana kujibu kwa jazba na kutotaka kufafanua zaidi.

"Wewe unatakia nini? Wameshindwa kuvaa (namba) na nimekwambia ni polisi na hakuna haja ya kufuatilia jambo hili kama unataka kaandike hiyo ni kazi yako,"alifoka Kamanda Tossi.

Kuhusu malalamiko ya vijana wa CHADEMA kutekwa Kamanda Tossi hakutaka tena kupokea simu ya mwandishi baada ya kupigiwa kwa mara nyingine.

Naye Mwandishi Wetu anaripoti kutoka Nyamongo, Tarime kuwa vijana wanaoaminika kuwa wafuasi wa CHADEMA walichoma tena sare na kofia za mahasimu wao, CCM, wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi huo uliofanyika eneo la Nyamongo.

Wafuasi hao walionekana wakichoma sare hizo juzi huku wengine wakizichanachana kwa meno, baada ya kuhamasishwa na hotuba ya Mwenyekiti wa Madiwani wa CHADEMA, Bw. Shaaban Mambo.

Huku wakishangilia, vijana hao walizimwagia mafuta ya taa na kuzitia moto sare hizo huku wengine wakigombea na kuzirarua kwa meno

Akizungumza wakati kitendo hicho kikiendelea, Bw. Mambo alionekana kumjibu Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuph Makamba akisema chama chake hakina makubaliano maalumu na vyama vingine ya kurejesheana sare na nyaraka zinazorudishwa na wanchama wanapohama vyama.

Awali Bw. Makamba alieleza kukerwa na kitendo cha kuchomwa bendera na sare za chama hicho akisema si kitendo cha kistaarabu kwani naye anavyo vifaa vingi anavyokabidhiwa na wanachama wa upinzani wanaorejea CCM lakini hawezi kuvichoma moto.

Bw. Mambo alisema kutokana na kutokuwapo makubaliano hayo, chama chake hakina njia nyingine, bali ni kuchoma moto kwa kile alichoeleza kuwa ni kukosa pia "sanduku la kuhifadhia sare hizo."

Akihutubia mkutano huo, Bw. Mambo aliwataka wananchi wa Tarime waache kupenda vyama bali wajenge tabia ya kupenda maendeleo yao.

Bw. Mambo, alitolea mfano wa Nijeria ambayo, imepiga hatua za kimaendeleo kuliko Tanzania kwa kuongozwa kijeshi kwa kipindi kirefu bila viongozi wa vyama vya siasa.

Katika kujaribu kunusu jimbo hilo lisiingie katika umwagaji wa damu zaidi, jana Mabalozi wa Uingereza nchini, Bw. Phillip Parham na wa Kanada, Bw. Staffan Herrstrom walioambatana na ofisa wa Ubalozi wa Uingereza, Bw. Larry Andre walifanya mikutano na wanasiasa jimboni humo.

Baada ya kukukutana na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Msimamizi wa Uchaguzi huo na Kamanda wa Polisi wa Oparesheni Maalumu, Bw. Venance Tossi, mabalozi hao jana mchana walifanya mkutano na viongozi wa CHADEMA.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Oganaizesheni wa CHADEMA makao makuu, Bw. Benson Kigaira, aliwasilisha malalamiko mengi ya chama hicho ikiwemo dai kuwa CCM na Jeshi la Polisi wamekuwa wakihusika 'kutengeneza,' vurugu.

Akizungumza baada ya mikutano hiyo, Bw. Parham alisema ameamua kukutana na viongozi hao baada ya kuangalia na kusoma kwenye vyombo vya habari mambo yanayotokea Tarime, hakuwa tayari kufafanua zaidi.

Uchaguzi wa jimbo hilo unafanyika Jumapili ijayo kuziba na.za ubunge na udiwani zote zikiwa zilizhwa wazi kufuatia kifo cha Bw. Chacha Wangwe.
 
Bila shaka Mkuu Madilu, walioua Mbwa wana kosa, si la jinai, bali la mauaji. Mbona tunaona magari yamebandikwa picha za kampeni nayo hayachomwi moto!!!!!

Niko TARIME kwa sasa tokea Tarehe 18 Septemba naomba kuweka jambo hili sahihi, ukweli ni kuwa mbwa huyo ambaye anajulikana kwa jina la Dudubaya yuko hai hajauawa.
 
Niko TARIME kwa sasa tokea Tarehe 18 Septemba naomba kuweka jambo hili sahihi, ukweli ni kuwa mbwa huyo ambaye anajulikana kwa jina la Dudubaya yuko hai hajauawa.

Huyu mbwa Dudubaya ana uhusiano na mwanamziki Dudubaya? na je kweli mwanamziki Dudubaya naye anatoka Tarime?
 
Tarime: Viongozi wa vyama waanza kupata hofu waingia kimya kimya

Na Frederick Katulanda, Tarime

TAARIFA za kuwasili kwa viongozi wa juu wa vyama vya upinzani kwa ajili ya kampeni wilayani Tarime, sasa zinafanywa kwa siri kubwa kutokana na hofu ya kufanyiwa vurugu na wafuasi wa vyama pinzani katika mikutano yao.

Hofu hiyo inatokana na kushambuliwa kwa viongozi ama kwa kuzomewa au kwa kupigwa na mawe katika mikutano yao kufuatia kuwepo kwa taarifa za wafuasi wa vyama vyote kutaka kulipiza kisasi kwa kuzomea na kushambuliana kwa mawe.

Tangu kuanza kampeni wilayani Tarime Septemba 14, mwaka huu mpaka sasa kuna matukio mbalimbali yanayoonyesha kuwepo kwa mchezo wa kuchafuana.

Kutokana na matukio hayo, ujio wa viongozi wa vyama mbalimbali katika uchaguzi huo umekuwa ukifanywa kwa siri kubwa kutokana na kuhofia kushambuliwa ama kukumbana na vurugu hizo.

Moja kati ya viongozi ambao ujio wao umegeuzwa kuwa siri kubwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe ambaye awali ilisemekana angeingia mjini hapa wiki iliyopita, lakini baada ya taarifa hizo kuandikwa na vyombo vya habari safari yake iliahirishwa.

Sambamba na Mbowe, pia ujio wa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja upande wa Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye alikuwa awasili Jumatatu uliahirishwa baada ya kutangazwa na vyombo vya habari alisitisha safari yake na kuingia jana kimya kimya na kwenda moja kwa moja kata ya Nyamongo ambako ni eneo la madini kwa lengo la kumnadi mgombea wao.

Kwa upande wa chama cha NCCR-Mageuzi ziara ya mwenyekiti wake James Mbatia nayo iligeuzwa siri kutokana na sababu hizo za usalama. Awali ilitolewa taarifa kuwa alitarajiwa kuwasili na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, lakini ziara hiyo bado ni siri na haijulikani watawasili lini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini alikiri kuwa viongozi hao walikuwa wakitarajiwa kuwasili kwa ajili ya kusaidia kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa chama chao na kwamba wanatarajiwa kuwasili Tarime siku yoyote, bila kutaja siku kwa maelezo kwamba hajapata uthibitisho wa siku hiyo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu.

"Atakuja Mbatia na mheshimiwa Mrema, lakini kwa sasa siwezi kusema wanakuja lini, mpaka uthibitisho toka juu, ila lazima watakuja kwa ajili ya kuwanadi wagombea wetu," alieleza.

Naye Msafiri Mtemelwa wa Chadema alipoulizwa kuhusiana na ujio wa Mbowe alisema anatarajiwa kufika siku yoyote na kwamba, kwa sasa hawezi kuweka bayana.

Kwa upande wa CCM licha ya kuwasili Ngeleja bado wamekuwa kimya kuhusiana na viongozi wengine wanaotarajiwa kuwasili kwa ajili ya kuimarisha kampeni kwa maelezo kwamba, kutoa taarifa katika vyombo vya habari hakusaidii.

Katibu wa CCM wilaya ya Tarime, Idd Stambuli, alisema kampeni ni mikakati, hivyo kutangaza kila kitu ni kuwanufaisha wapinzani wao.

Naye Mussa Juma, anaripoti kuwa mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya, Canada na Marekani wamefika wilayani Tarime na kuahidi kwamba, watapeleka waangalizi katika uchaguzi huo utafanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Viongozi wa chama hicho walidai mbele ya mabalozi hao kuwa polisi na CCM wana njama za kuharibu uchaguzi huo na kusababisha vurugu na mapigano katika eneo hilo.

Wakizungumza na mabalozi Staffan Herrtrom wa Sweeden, Janet Siddall (Canada), Philip Parham (Uingereza) na Balozi Mdogo wa Marekani, Larry Andre, katika Hoteli ya Makoma, viongozi wa Chadema waliopo kwenye kampeni mjini hapa walisema hawana imani kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

Akisoma taarifa ya hali ya uchaguzi huo kwa mabalozi hao, Mkurugenzi wa Mipango wa Chadema, Benson Kigaila alidai kuwa jeshi la polisi limekuwa sehemu ya kampeni ya CCM na limekuwa likisababisha vurugu mjini Tarime.

Kigaila alisema licha ya wao Chadema kupeleka malalamiko mengi polisi juu ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unaofanywa na viongozi na wafuasi wa CCM hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

"Waheshimiwa mabalozi ni kazi maalum gani hiyo ambayo polisi wanaifanya kwa kununua kadi za Chadema, tunaomba mtusaidie kukomesha hali hii ili uchaguzi huu uwe huru na haki," alisema Kigaila.

Alilalamika kuwa vijana wengi wa chama hicho wamekamatwa na wamenyimwa dhamana, lakini vijana wote wa CCM waliokamatwa wameachiwa kwa dhamana akiwemo Emanuel Marwa ambaye alikamatwa baada ya kuvunja kioo cha gari la matangazo la Chadema.

Naye Mkurugenzi wa Uenezi na Habari wa Chadema, Erasto Tumbo, alisema hali ya uchaguzi Tarime inatishiwa na CCM na polisi ambao wamefurika wilayani humo.

Alisema katika mikutano ya hadhara polisi wamekuwa wakijaa na kuwakamata vijana ovyo mitaani ili washindwe kupiga kura.

Wakizungumza mara baada ya taarifa hiyo, mabalozi hao walisema wao wamefika Tarime kujionea hali ya uchaguzi huo baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa vurugu zimekithiri.

Balozi, Parham alisema licha ya kujifunza, wiki ijayo wanatarajia kutuma maafisa wa ubalozi kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi huo.

"Leo tutakutana na viongozi wa vyama na kusikiliza maoni yao kuhusiana na uchaguzi huu, ili tupate taarifa sahihi juu ya uchaguzi huu," alisema Parham.

Mabalozi hao walihoji pia tofauti ya hali ya uchaguzi ya mwaka huu na mwaka 2005 na kuelezwa mwaka huu ni hali mbaya zaidi na huenda amani ikatoweka siku ya matokeo kama hali isipodhibitiwa.

Wakati huo huo, Kamanda wa Operesheni maalum wilayani Tarime, Kamishna Msaidizi wa Polisi Venance Tossi, alisema kuanzia leo jeshi hilo litakuwa linamchukulia hatua kali mtu yeyote atakaye kiuka taratibu za uchaguzi, bila kujali nafasi yake.

"Kuanzia kesho(leo) mtaona nguvu ya dola na kwamba, jeshi letu lipo imara na hatutakuwa na msamaha kwa mtu yoyote atayevuruga amani, bila kujali nafasi yake," alisema Tossi.

Alisema kikosi cha polisi wengine 300 pamoja na magari maalumu kinatarajiwa kuwasili kuanzia leo mjini hapa, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa huru na amani.

Kabla ya kukutana na waandishi jana na kutoa kauli hiyo, Kamanda Toss akiwa pamoja na mkuu wa kikosi cha askari wa kuzuwia fujo FFU nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Trasphory Anaclet walikutana na mabalozi hao na kufanya mazungumzo katika kituo cha polisi Tarime.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema chama kitachoshindwa kinapaswa kwenda mahakamani na wala siyo kuanzisha vurugu.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya maafisa wa Tume ya Uchaguzi, vyama vya siasa na jeshi la polisi, Manumba alisema kuna taarifa za kufanyika vurugu iwapo chama fulani kitashindwa na kingine kushinda.

Aliwakumbusha viongozi wa vyama hivyo kuwa njia pekee za kupinga matokeo kwa upande ambao hautoridhika ni kuzingatia sheria kwa kwenda mahakamani badala ya kuingia mitaani kufanya vurugu ambazo zitasababisha hali kuwa tete wilayani Tarime.

"Ninafahamu kuwa uchaguzi unafanyika na mshindi atatangazwa, walioshinda watafurahi na kushangilia na walioshindwa watahuzunika na kulalamika, lakini njia pekee ni kwenda mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na si kufanya fujo," alionya.

Alisema vyama vya siasa vinapaswa kuwaeleza wafuasi wao kuwa na subira hadi mwisho wa uchaguzi na kwamba, jeshi hilo lipo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika mazingira salama na kwa haki na kwamba, wapo tayari kukosolewa wanapoona linakwenda kinyume na wajibu wake.

Vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na DP ambavyo vilisisitiza kuwa lisimamie sheria.

Katika hali nyingine wanafunzi 64 wa shule ya sekondari ya Rebu, waliopata ajali ya gari juzi katika eneo la Msati nje kidogo ya mji wa Tarime wameruhusiwa kutoka hospitali ya wilaya ya Tarime, huku wengine 33 wakiwa bado wamelazwa kutokana na majera makubwa waliyopata.
 
fadhali kwa kuwa hajauawa; maana ulikuwa uuaji mbaya sana wa kisiasa; na hiyo itakuwa nuksi kwa GREEN PARTY; Amani iwepo lakini sio police kulazimisha watu na kununua kadi za watu; hicho ndio kimewapeleka huko? chonde chonde siasa si uhasama; na si lazima ushinde kwani wewe nani?
 
habari za saa hii.
Ikiwa kwlei mbwa ameuliwa basi ni kosa limefanyika na waliomuuwa wamefanya makosa. lakini suala la mbwa kuveshwa fulana walioanza kitendo hicho ni wana CCM waliwahi kumvesha mbwa fulana na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Shariff Hamad siku tume ya uchaguzi zanzibar ili[pomtangaza mshindi Rais Amani Karume walimvalisha fulana na kuongozana na kundi la wana CCM kwa maandamano huku wakiongozwa na bendi ya vijana wa CCM barabarani kwa mbwembwe zote kial mmoja aliwaona na waandishi wakapiga picha kibao kulikuwa na mbwa wawili mmoja dume na mwengine mke aliitwa Maalim Seif na mwengine aliitwa Bi Awena mke wa Maalim Seif.
kwneye mtandano wa CNN picha hiyo ilikuwemo na mpiga picha wa The Guardian nadhani sana anayo maana alikuwepo zanzibar kipindi hicho.

Kwa ufupi mimi sijaliona jipya lililofanyika katika kampeni za Tarime hadi sasa naona yaliofanyika yote ikiwemo kuuawa watu na kupigwa mapanga au kuzuwiwa wasifanye kampeni yote hayo yameshawahi kufanyika zanzibar na zaidi kuliko hayo.

sio kama nasema hayo yameshawahi kufanyika ndio kuhalalisha vitendo viovu no namaanisha mambo kama hayo yameshawahi kufanyika na zaidi inagwa ni vitendo vibaya na vinastahiki kulaaniwa na kila mpenda amani nchini.
Mungu tuweke tuone mengi maana tumeshashuhudia mengi sana kwa macho yetu sasa tunasikia kwa masikio tu
 
"Without knowledge, there is no freedom." — Anon."
Even if you have knowledge you can still not b free if those holding your freedom have not released it........or when you are acting at the auspices of someone.........in that case even if you are knowledgeable to great extent you will not be free to act.

Knowledge is defined (Oxford English Dictionary) variously as (i) expertise, and skills acquired by a person through experience or education; the theoretical or practical understanding of a subject, (ii) what is known in a particular field or in total; facts and information or (iii) awareness or familiarity gained by experience of a fact or situation.
 
Hii inakumbusha ile case iliyoamuliwa na hakimu wa kibongo eti mbwa auwawe kwa kuwa amepewa jina la "IMMIGRATION", bongo kuna mambo kila kitu ni Ze Comedy tu.
 
Huyu mbwa Dudubaya ana uhusiano na mwanamziki Dudubaya? na je kweli mwanamziki Dudubaya naye anatoka Tarime?

NILIBAHATIKA KUONGEA NA MMOJA WA WASHITAKIWA WA KESI YA KUMVISHA VULANA MBWA HUYO AMBAYE NI (Jina nalihifadhi kwa sasa) HANA UHUSIANO NA DUDUBAYA WA MOJA KWA MOJA ISIPOKUWA JINA LAKE LIMETOKANA NA MWANAMZIKI HUYO DUDUBAYA WAKATI ALIPOVUMA SANA NDIPO WALIPOAMUA KUMPATIA JINA HILO HUYU MBWA.
 
Date::10/4/2008
Tarime: Viongozi wa vyama waanza kupata hofu waingia kimya kimya

mabalozitarime.jpg

Kamanda wa Kikosi cha Operesheni, Jeshi la Polisi Tanzania, Venance Tossi, na Mkuu wa Kikosi cha Kuzuia Fujo (FFU), Anavlet Trasphery, wakiwa na mabalozi Janet Siddall wa Canada, Phillip Parham wa Uingereza na Staffan Herrtrom wa Sweeden, waliofika Tarime Ijumaa kujionea hali ya uendeshaji wa kampeni za kisiasa wilayani huko.

Na Frederick Katulanda, Tarime
Mwananchi

TAARIFA za kuwasili kwa viongozi wa juu wa vyama vya upinzani kwa ajili ya kampeni wilayani Tarime, sasa zinafanywa kwa siri kubwa kutokana na hofu ya kufanyiwa vurugu na wafuasi wa vyama pinzani katika mikutano yao.

Hofu hiyo inatokana na kushambuliwa kwa viongozi ama kwa kuzomewa au kwa kupigwa na mawe katika mikutano yao kufuatia kuwepo kwa taarifa za wafuasi wa vyama vyote kutaka kulipiza kisasi kwa kuzomea na kushambuliana kwa mawe.

Tangu kuanza kampeni wilayani Tarime Septemba 14, mwaka huu mpaka sasa kuna matukio mbalimbali yanayoonyesha kuwepo kwa mchezo wa kuchafuana.

Kutokana na matukio hayo, ujio wa viongozi wa vyama mbalimbali katika uchaguzi huo umekuwa ukifanywa kwa siri kubwa kutokana na kuhofia kushambuliwa ama kukumbana na vurugu hizo.

Moja kati ya viongozi ambao ujio wao umegeuzwa kuwa siri kubwa ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe ambaye awali ilisemekana angeingia mjini hapa wiki iliyopita, lakini baada ya taarifa hizo kuandikwa na vyombo vya habari safari yake iliahirishwa.

Sambamba na Mbowe, pia ujio wa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja upande wa Chama Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye alikuwa awasili Jumatatu uliahirishwa baada ya kutangazwa na vyombo vya habari alisitisha safari yake na kuingia jana kimya kimya na kwenda moja kwa moja kata ya Nyamongo ambako ni eneo la madini kwa lengo la kumnadi mgombea wao.

Kwa upande wa chama cha NCCR-Mageuzi ziara ya mwenyekiti wake James Mbatia nayo iligeuzwa siri kutokana na sababu hizo za usalama. Awali ilitolewa taarifa kuwa alitarajiwa kuwasili na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Mrema, lakini ziara hiyo bado ni siri na haijulikani watawasili lini.

Akizungumza na gazeti hili jana, Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, Joseph Selasini alikiri kuwa viongozi hao walikuwa wakitarajiwa kuwasili kwa ajili ya kusaidia kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa chama chao na kwamba wanatarajiwa kuwasili Tarime siku yoyote, bila kutaja siku kwa maelezo kwamba hajapata uthibitisho wa siku hiyo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu.

“Atakuja Mbatia na mheshimiwa Mrema, lakini kwa sasa siwezi kusema wanakuja lini, mpaka uthibitisho toka juu, ila lazima watakuja kwa ajili ya kuwanadi wagombea wetu,” alieleza.

Naye Msafiri Mtemelwa wa Chadema alipoulizwa kuhusiana na ujio wa Mbowe alisema anatarajiwa kufika siku yoyote na kwamba, kwa sasa hawezi kuweka bayana.

Kwa upande wa CCM licha ya kuwasili Ngeleja bado wamekuwa kimya kuhusiana na viongozi wengine wanaotarajiwa kuwasili kwa ajili ya kuimarisha kampeni kwa maelezo kwamba, kutoa taarifa katika vyombo vya habari hakusaidii.

Katibu wa CCM wilaya ya Tarime, Idd Stambuli, alisema kampeni ni mikakati, hivyo kutangaza kila kitu ni kuwanufaisha wapinzani wao.

Naye Mussa Juma, anaripoti kuwa mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya, Canada na Marekani wamefika wilayani Tarime na kuahidi kwamba, watapeleka waangalizi katika uchaguzi huo utafanyika Oktoba 12, mwaka huu.

Viongozi wa chama hicho walidai mbele ya mabalozi hao kuwa polisi na CCM wana njama za kuharibu uchaguzi huo na kusababisha vurugu na mapigano katika eneo hilo.

Wakizungumza na mabalozi Staffan Herrtrom wa Sweeden, Janet Siddall (Canada), Philip Parham (Uingereza) na Balozi Mdogo wa Marekani, Larry Andre, katika Hoteli ya Makoma, viongozi wa Chadema waliopo kwenye kampeni mjini hapa walisema hawana imani kuwa uchaguzi huo utakuwa huru na haki.

Akisoma taarifa ya hali ya uchaguzi huo kwa mabalozi hao, Mkurugenzi wa Mipango wa Chadema, Benson Kigaila alidai kuwa jeshi la polisi limekuwa sehemu ya kampeni ya CCM na limekuwa likisababisha vurugu mjini Tarime.

Kigaila alisema licha ya wao Chadema kupeleka malalamiko mengi polisi juu ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unaofanywa na viongozi na wafuasi wa CCM hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

“Waheshimiwa mabalozi ni kazi maalum gani hiyo ambayo polisi wanaifanya kwa kununua kadi za Chadema, tunaomba mtusaidie kukomesha hali hii ili uchaguzi huu uwe huru na haki,” alisema Kigaila.

Alilalamika kuwa vijana wengi wa chama hicho wamekamatwa na wamenyimwa dhamana, lakini vijana wote wa CCM waliokamatwa wameachiwa kwa dhamana akiwemo Emanuel Marwa ambaye alikamatwa baada ya kuvunja kioo cha gari la matangazo la Chadema.

Naye Mkurugenzi wa Uenezi na Habari wa Chadema, Erasto Tumbo, alisema hali ya uchaguzi Tarime inatishiwa na CCM na polisi ambao wamefurika wilayani humo.

Alisema katika mikutano ya hadhara polisi wamekuwa wakijaa na kuwakamata vijana ovyo mitaani ili washindwe kupiga kura.

Wakizungumza mara baada ya taarifa hiyo, mabalozi hao walisema wao wamefika Tarime kujionea hali ya uchaguzi huo baada ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa vurugu zimekithiri.

Balozi, Parham alisema licha ya kujifunza, wiki ijayo wanatarajia kutuma maafisa wa ubalozi kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi huo.

“Leo tutakutana na viongozi wa vyama na kusikiliza maoni yao kuhusiana na uchaguzi huu, ili tupate taarifa sahihi juu ya uchaguzi huu,” alisema Parham.

Mabalozi hao walihoji pia tofauti ya hali ya uchaguzi ya mwaka huu na mwaka 2005 na kuelezwa mwaka huu ni hali mbaya zaidi na huenda amani ikatoweka siku ya matokeo kama hali isipodhibitiwa.

Wakati huo huo, Kamanda wa Operesheni maalum wilayani Tarime, Kamishna Msaidizi wa Polisi Venance Tossi, alisema kuanzia leo jeshi hilo litakuwa linamchukulia hatua kali mtu yeyote atakaye kiuka taratibu za uchaguzi, bila kujali nafasi yake.

“Kuanzia kesho(leo) mtaona nguvu ya dola na kwamba, jeshi letu lipo imara na hatutakuwa na msamaha kwa mtu yoyote atayevuruga amani, bila kujali nafasi yake,” alisema Tossi.

Alisema kikosi cha polisi wengine 300 pamoja na magari maalumu kinatarajiwa kuwasili kuanzia leo mjini hapa, ili kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kwa huru na amani.

Kabla ya kukutana na waandishi jana na kutoa kauli hiyo, Kamanda Toss akiwa pamoja na mkuu wa kikosi cha askari wa kuzuwia fujo FFU nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP), Trasphory Anaclet walikutana na mabalozi hao na kufanya mazungumzo katika kituo cha polisi Tarime.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba alisema chama kitachoshindwa kinapaswa kwenda mahakamani na wala siyo kuanzisha vurugu.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja baina ya maafisa wa Tume ya Uchaguzi, vyama vya siasa na jeshi la polisi, Manumba alisema kuna taarifa za kufanyika vurugu iwapo chama fulani kitashindwa na kingine kushinda.

Aliwakumbusha viongozi wa vyama hivyo kuwa njia pekee za kupinga matokeo kwa upande ambao hautoridhika ni kuzingatia sheria kwa kwenda mahakamani badala ya kuingia mitaani kufanya vurugu ambazo zitasababisha hali kuwa tete wilayani Tarime.

“Ninafahamu kuwa uchaguzi unafanyika na mshindi atatangazwa, walioshinda watafurahi na kushangilia na walioshindwa watahuzunika na kulalamika, lakini njia pekee ni kwenda mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake na si kufanya fujo,” alionya.

Alisema vyama vya siasa vinapaswa kuwaeleza wafuasi wao kuwa na subira hadi mwisho wa uchaguzi na kwamba, jeshi hilo lipo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika katika mazingira salama na kwa haki na kwamba, wapo tayari kukosolewa wanapoona linakwenda kinyume na wajibu wake.

Vyama vilivyoshiriki katika kikao hicho ni CCM, Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na DP ambavyo vilisisitiza kuwa lisimamie sheria.

Katika hali nyingine wanafunzi 64 wa shule ya sekondari ya Rebu, waliopata ajali ya gari juzi katika eneo la Msati nje kidogo ya mji wa Tarime wameruhusiwa kutoka hospitali ya wilaya ya Tarime, huku wengine 33 wakiwa bado wamelazwa kutokana na majera makubwa waliyopata.
 
Date::10/5/2008
Majina 200 ya wapiga kura yatoweka Tarime
Na Mussa Juma, Tarime
Mwananchi

IKIWA imesalia takriban wiki moja kabla ya uchaguzi wa mbunge na diwani wa Tarime kufanyika, mauzauza yamechukua nafasi yake baada ya majina ya wapiga kura zaidi ya 200 kutoonekana kwenye vituo mbalimbali mjini hapa.

Mbali na majina kutoweka katika vituo walivyojiandikisha, majina ya wapiga kura wengine yamewekwa katika orodha ya wapiga kura waliohama wilaya hiyo.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kubandikwa majina hayo, katika vituo vya Chuo cha Ualimu Tarime na vituo vya kitongoji cha Starehe na Nyasangura B , Tarime A, B na C vyote vya mjini Tarime, baadhi ya wapiga kura walilalamika kutoona majina yao na wengine kuandikwa kuwa wamehama.

Katika kituo cha Chuo cha Ualimu, majina 64 yaliorodheshwa kuwa hawatapiga kura kwa kuwa wamehama au kuna makosa wakati wa kujiandikisha, wakati kituo cha Tarime C watu 41 wamezuiwa kupiga kura huku kituo cha Tarime B watu 62 wamezuiwa na Tarime Mjini watu 60 hawatapiga kura.

Mwenge Alli, mwenye shahada namba 44622111 ambaye alikuwa amejiandikisha katika kituo hicho, alisema jina lake halimo kwenye orodha ya wapiga kura.

Alisema alijiandikisha katika kituo hicho katika zoezi la pili la marudio Agosti 20 mwaka huu mbele ya mwenyekiti wa serikali ya kitongoji hicho, Kenguru Tagaya, ambaye pia jana alikuwepo katika kituo hicho.

“Hapa jina langu halipo na nimetembea vituo vyote hapa mjini hakuna jina langu,” alilalamika Alli.

Naye Mwita Marwa alisema jina lake halipo katika kituo cha Nyasangurwa B alipoandikishwa na baada kufika katika kituo hicho aliambiwa aende kituo cha Starehe ambapo pia hakukuta jina.

Kijana mwingine, Samweli Lazaro alilalamika kukuta jina lake kati ya majina ya watu ambao hayataruhusiwa kupiga kura kwa maelezo kwamba amehama wilaya hiyo.

“Sasa hawa watu wa ajabu eti mimi nimehama, na (mwenzake) Jordan naye kaandikwa amehama huu ni mpango wa kutuzuia kupiga kura,” alilalamika Lazaro.

Katika kituo cha Chuo cha Ualimu Tarime, kundi la walimu pia lilikuwa linalalamikia kutoona majina na wengine kuandikwa kuwa wamehama na hivyo kutoruhusiwa kupiga kura.

“Tunaomba tume cha uchaguzi irekebishe haya mambo... Huu ni uhuni na ni njama kwani haiwezekani sisi kusomeka tumehama na wengine majina hayapo,” alisema mwanachuo mmoja ambaye aliomba kutotajwa jina gazetini.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Starehe, Tagaya, ambaye jana alikuwa akishuhudia malalamiko hayo, alionyesha kushangazwa na mauzauza hayo.

"Hapa tusilalamikie chama fulani kwani kuna watu wa CCM ambao hawapo na Chadema pia hawapo... Ni makosa ya tume nadhani yatarekebishwa," alisema Tagaya.

Hata hivyo, akizungumzia malalamiko hayo, msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Tarime, Trasias Kagenzi alikiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa hiyo ndiyo sababu iliyowafanya wabandike majina mapema.

“Inawezekana haya ni matatizo ya uchapaji kwenye kompyuta hivyo wale wote wenye malalamiko wayafikishe ofisi za tume ili turekebishe mapema,” alisema Kagenzi.

Alifafanua kuwa kwa wale ambao wameandikwa kuwa wamehama inawezekana wamejiandikisha mara mbili au pia ni tatizo la

kompyuta na wao wanapaswa kufikisha malalamiko yao ofisi za wasimamizi wa uchagizi kuanzia kata ili yapatiwe ufumbuzi.

Alisema halmashauri yake itahakikisha kila mtu mwenye haki ya kupiga kura anapata nafasi hiyo bila ya wasi wasi na ambao hadi mwisho hawatapiga ni lazima watakuwa na matatizo mengine.

“Hii ni wilaya ya mpakani inawezekana kabisa kuna ambao wamebainika sio raia hivyo hawana haki ya kupiga kura na kuna wengine katika kujiandikisha wametaja majina tofauti hivyo lazima wawe makini,” alisema Kagenzi.

Wakati huohuo, Kagenzi amewataka wakazi wa Tarime kupuuza uvumi kuwa ameshinikizo na CCM kuwa ni lazima akitangaze chama hicho kuwa washindi katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo katika nafasi za ubunge na udiwani la sivyo ataondolewa kazini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, msimamizi huyo alisema amesikia maneno mitaani na kupokea barua toka katika chama kimoja, ambacho hata hivyo hakukitaja jina, kuwa amepokea maagizo kuwa ni lazima awatangaze wagombea wa CCM kuwa washindi.

''Napenda kuliweka wazi suala hili kuwa mimi ni mtu mwenye msimamo na sijapokea shinikizo lolote kwani ninaviheshimu vyama vyote ambavyo vinashiriki uchaguzi huu na nakanusha kupokea haya mashinikizo kuwa nikitangaza CCM imeshindwa nitahamishwa au kuondolewa kazini,'' alisema Kagenzi.

Alisema yeye kama msimamizi wa uchaguzi hana mamlaka ya kutangaza mshindi ambaye hakupata kura nyingi kwani matokeo huanza kuhesabiwa katika vituo na kila kituo kinakuwa na wakala.

''Haya maneno nayasikia tena wengine wanaotamka ni viongozi wakubwa tu wa vyama (hakuwataja), lakini naamani wanajua utaratibu wa uchaguzi kuwa mimi ni mtu wa kutangaza tu kazi yote inafanywa kwenye vituo," alisema Kagenzi.

Akizungumzia malalamiko toka Chadema kuwa ameshinikizwa na CCM kupewa majina ya mawakala mapema ili waweze kujulikana na kununuliwa, msimamizi huyo pia alikanusha.

Licha ya kuvitaka vyama vyote kuwasilisha majina ifikapo Oktoba sita, hadi leo (jana) hakuna chama kilichofanya hivyo," alisema.

"Niliwaandikia barua tangu Septemba 24 kuwataka wanipe majina na hii ni kwa mujibu wa taratibu, lakini vyama vyote havijaleta na hili lilitokana na kuongezwa vituo vya kupiga kura kutoka 369 hadi 406,"alisema Kagenzi.

Alisema mwisho wa kupokea majina hayo ni leo.

Katika uchaguzi huo mdogo wa jimbo la Tarime ambao utafanyika Oktoba 12, jumla ya watu 146,510 wanatarajiwa kupiga kura na upinzani mkubwa upo kati ya CCM na Chadema. Vyama vingine ni NCCR-Mageuzi na DP.s

Wakati huohuo gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) litomiwalo wakati wa kukabili ghasia, maarufu kama kojozi, limewasili kutoka jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Operesheni Maalumu wa Polisi, Venance Tossi alisema kuwa gari hilo limewasili sambamba na askari wengine 300 kwaajili ya kutuliza ghasia.

Hata hivyo, baadhi ya askari polisi walioletwa mjini hapa kwa ajili ya kulinda usalama wameanza kulalamikia posho wanayopewa ya Sh 1,000 kwa siku ingawa wanapewa malazi na chakula bure. Wanadai hali hiyo inawafanya waishi maisha magumu.
 
Hii mwananchi ya lini? Sikuiona kwenye gazeti la leo!
Lakini NEC wajihadhari, wasije kupandisha hasira za hawa ndugu zetu bila sababu ya msingi. Nao watulie tu, nadhani nia ya kubandika majina mapema ni kubaini kasoro kama hizo na kuzirekebisha kabla ya siku ya kupiga kura, la muhimu ni kuwa wafikishe malalamiko yao panapohusika ili yashughulikiwe, wasiishie kuzungmza na waandishi tu
 
[Source Tanzania Daima]

Mshtuko mpya Tarime

na Kulwa Karedia, Tarime

ZIKIWA zimesalia siku sita kabla ya kupiga kura Oktoba 12 mwaka huu, hali ya wasiwasi na mshtuko imewakumba mamia ya wapiga kura kutokana na baadhi yao kutokuwamo kwenye orodha ya watu wanaotakiwa kupiga kura siku ya uchaguzi.

Hali hiyo imetokea siku moja tu baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutoa orodha ya majina ya watakaopiga kura katika jimbo hilo Jumapili ijayo.

Wananchi hao walieleza mshtuko huo jana mjini hapa baada ya kutembelea vituo mbalimbali kulikobandikwa majina yao na baadhi yao kubaini kuwa majina yao hayamo kwenye orodha hiyo, licha ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

Mmoja wa wananchi hao, Mwenge Ally, mwenye shahada namba 44622111, alisema baada ya kufika kwenye kituo chake alichojiandikishia cha Tarime C, jina lake halikuwapo, hali ambayo inamfanya kukosa haki yake ya kupiga kura.

“Nimeshangazwa na hali hii, nimekuja hapa kuangalia jina langu lakini halipo... sasa sijui hatima yake nini, shahada yangu hii hapa jamani, inawezekana huu ni mpango uliofanywa na tume ili nikose haki yangu ya msingi,” alisema Ally.

Mbali ya Ally, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji katika eneo hilo, Kengula Tagaya, alisema katika kituo B, zaidi ya majina 62 hayamo kwenye orodha hiyo na huenda wasipige kura siku hiyo.

“Ni kweli kumetokea matatizo makubwa hapa, hawa wananchi walijiandikisha mimi mwenye nikiwepo, sasa nashangaa kuona majina hayapo... lakini kibaya zaidi ni pale baadhi ya majina yanayotolewa yanaonyesha eti wengine wamehama, jambo ambalo si kweli,” alisema Tagaya.

Katika kituo hicho, zaidi ya wananchi 41 majina yao hayakurudi kwa sababu mbalimbali, zikiwemo wengine kuhama makazi au kujiandikisha zaidi ya mara mbili.

Mbali ya kituo hicho, katika kituo cha Tarime mjini, zaidi ya majina 60 yamerudi bila ya kuwa na namba, hivyo kukosa haki yao ya kupiga kura siku hiyo.

Naye Samweli Lazaro Chacha, kwa upande wake alisema amesikitishwa na kitendo cha NEC kurudisha jina likiwa limewekwa kwenye orodha ya wakazi waliohama eneo hilo.

“Nashangaa sana kuona tume inarudisha jina langu na kusema eti mimi nimehama. Huu ni ujanja unaofanywa ili tusichague chama tunachokipenda, huu ni mchezo mchafu ambao tume imezoea kuufanya kila uchaguzi unapokaribia,” alisema Chacha.

Akijibu malalamiko hayo, Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Trasias Kagenzi, alisema tume yake imepokea malalamiko hayo na hatua zinachukuliwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya siku ya uchaguzi.

“Suala hili nimelisikia, napenda kukuhakikishieni kwamba tunafanya marekebisho ya haraka ili wote ambao majina yao hayapo, yaingizwe kwenye orodha ya wapiga kura,” alisema Kagenzi.

Kagenzi alisema moja ya tatizo la wakazi wa Tarime, wamekuwa wakichanganya majina wakati wa kujiandikisha, jambo ambalo husababisha majina yao kubadilika wakati wa kuandikwa kwenye kompyuta,” alisema Kagenzi.

Alisema kwa wananchi wa maeneo ya vijijini, wanapaswa kupeleka malalamiko yao haraka kwa viongozi walioteuliwa na tume kusimamia uchaguzi huo katika maeneo yao ili kufanyiwa marekebisho.

Mkurugenzi huyo alisema, jumla ya wapiga kura 146,510 wamejiandikisha katika uchaguzi huo na vituo 407, vinaratajiwa kutumika siku ya uchaguzi.

Katika hatua nyingine, Kagenzi amesema hayuko tayari kupindisha matokeo, hata akilazimishwa kufanya hivyo kwa mtutu wa bunduki.

Msimamizi huyo alilazimika kutoa kauli hiyo, kukanusha uvumi kwamba kuna shinikizo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwamba lazima amtangaze mgombea wa chama hicho, Christopher Kangoye, kuwa mshindi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana, Kagenzi aliwataka wana Tarime kupuuza maneno hayo kuwa hajapewa shinikizo lolote la kutangaza wagombea ubunge na udiwani na wala hana mamlaka kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

“Nawaomba sana wana Tarime na watu wengine kuachana na uvumi huu, kwani mimi sina mamlaka ya kutangaza mshindi kwa shinikizo, ninachoweza kusema ni kwamba nitafuata sheria zote za uchaguzi,” alisema Kagenzi.

Alisema hatakubali kuyumbishwa kwa kafuata matakwa ya watu fulani ambao wanataka kushinda kiti hicho kwa nguvu.

“Siku zote nimekuwa mtu mwenye msimamo katika kazi yangu... nazingatia sheria za uchaguzi, sijapokea barua kutoka chama chochote, ikiwemo CCM, naviheshimu vyama vyote vinavyoshiriki uchaguzi huu,” alisema Kagenzi.

Alisema baadhi ya madai yanayotolewa ni kwamba CCM isiposhinda katika uchaguzi huo, atahamishwa kituo cha kazi, lakini alisisitiza kuwa sheria za uchaguzi haziruhusu kitu kama hicho hata siku moja.

Kagenzi alisema msimamizi wa uchaguzi atamtangaza mshindi yule tu atayekuwa amepata kura nyingi baada ya kuhesabiwa na kukubalika kwa pande zote mbili.

“Kumekuwa na tabia ya watu kutoa lugha ambazo hazifai, tena nasikia ni viongozi wakubwa kabisa katika vyama vyao, napenda kutumia nafasi hii kusema hakuna kitu kama hicho,” alisema Kagenzi.

Kuhusu malalamiko yaliyotolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa ameshinikizwa na CCM kutangaza majina ya mawakala mapema ili wajulikane na kununuliwa na chama hicho, msimamizi huyo alikataa kuhusika na suala hilo.

Alisema leo ndiyo siku ya mwisho ya kuwasilisha majina ya mawakala wote wa vyama lakini hakuna chama kiichotekeleza agizo lake.

“Mimi niliwaandikia barua tangu Septemba 24, wanipe majina na hii ni kwa mujibu wa taratibu, lakini vyama vyote havijaleta na hii ilitokana na kuongezwa vituo vya kupigia kura kutoka 369 hadi 406,” alisema Kagenzi.

Katika uchaguzi huo mdogo, jumla ya wapiga kura 146,510 wanatarajiwa kupiga kura, na upinzani mkubwa upo kati ya CCM na Chadema.

Katika hatua nyingine, CCM, inadaiwa kufanya mikutano ya siri nyumbani kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, (NEC), Christopher Gachuma na kupitisha maazimio ambayo wanaamini yatakisaidia chama hicho kushinda uchaguzi huo.

Habari za kuaminika zilizopatikana jana kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho waliohudhuria mkutano huo, ambao ulifanyika katika Kijiji cha Komaswa, walisema moja ya mkakati uliopangwa ni kuhakikisha CCM inaibuka na ushindi kwa namna yoyote ile.

“Ni kweli kikao hiki kilifanyika nyumbani kwa Gachuma na kupanga mikakati mizito ya kuhakikisha CCM inashinda uchaguzi huo kwa namna yoyote ile... lakini hii imetokana na hali halisi ya upinzani uliopo,” kilisema chanzo hicho.

Moja ya azimio linalodaiwa kupendekezwa kwenye kikao hicho ambacho kilifanyika siku za Alhamisi na Ijumaa iliyopita na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu, akiwemo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Pius Msekwa, ni kuhakikisha kila mpiga kura na viongozi wa serikali za mitaa wanapewa pesa siku moja kabla ya uchaguzi.

Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kuwa vikao hivyo kwa kauli moja vilikubaliana kwamba mawakala watakaopitishwa na chama na kupangwa vituoni, kila mmoja atakabidhiwa kitita cha sh 300,000.

Mbinu hiyo inadaiwa kuwa sehemu ya mkakati wa kutaka kulikomboa jimbo hilo ambalo lilikuwa likiongozwa na marehemu Chacha Wangwe (Chadema), aliyefariki dunia kwa ajali ya gari mjini Dodoma.

Katibu Mkuu wa CCM, Makamba, alipopigiwa simu na gazeti hili ili kutaka kupata ufafanuzi wa suala hilo, alijibu kwa kusema: “Sasa ndugu yangu mimi nikusaidie nini, sina cha kukwambia,” alisema na kukata simu.

Hivi sasa hali ya ulinzi imezidi kuimarishwa kukabiliana na vurugu, ambapo juzi gari linalotumika kumwaga maji ya pilipili, yanayowasha mwilini, limewasili, tayari kukabiliana na vurugu zinazoweza kutokea siku hiyo.

Hivi sasa gari hilo ambalo limewahi kutumika kwenye uchaguzi mkuu visiwani Zanzibar kukabiliana na vurugu, limeegeshwa kwenye Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Tarime, huku likiwa chini ya uangalizi wa askari na waandishi wa habari wamezuiliwa kulipiga picha.
 
Hah! waanzilishi wa Vurugu ni CCM na sasa CHADEMA MSIKUBALI KUHUJUMIWA.TUMECHOKA
 
Kuna kila dalili ile ripoti ya Tarime yaweza kutolewa wakati wowote kabla ya uchaguzi Jumapili...
 
...ya hoja binafsi bungeni ya marehemu Wangwe au ya Jukwaa la Wahariri kuhusu yaliyojiri wakati wa msiba wake Tarime?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom