Ubungo interchange, imepunguza foleni au imepunguza msongamona kwenye eneo la daraja yaani katika mataa ya Ubungo?

Ubungo interchange, imepunguza foleni au imepunguza msongamona kwenye eneo la daraja yaani katika mataa ya Ubungo?

Barabara zinapanuliwa na madaraja yanajengwa. Njia za kando zinajengwa. Serikali inahamia Dodoma. Ni suala la muda foleni unazozisema zitabaki kuwa historia
 
Kwa kawaida mfumo wa interchange kama ule huwa unaondoa msongamano sehemu ulipojengwa na kuihamishia mahala pengine jirani...

Suluhisho la foleni za kudumu ni:
1.Kuwa na interchange/overpass/umderpass karibu kila junction iliyo busy.

2. Kuwa na flyovers zenye kutembea umbali mrefu "expressways", mathalini uwe na njia isiyoingiliwa toka Kibaha hadi Posta, yenyewe inakuwa na exits na entries sehemu kadhaa tu.

3. Dar isiwe Posta au Kariakoo tu.

4. City trains/BRTs za kutosha
3.ndio njia pekee ya kitaalam,hizo zingine hakuna hata moja inayoweza hata kupunguza tatizo.

maadam nuclear ni posta basi hili balaa ni la milele,nenda nairobi kwenye madaraja kila makutano ukaone balaa lake.

kamji kakiishakuwa kiuchochoro hakuna namna nyepesi tena ya kupambana na foreni.
 
Chato boy kama hata kiswahili tu ni shida. Unadhani akisafiri kwenda nchi za watu anapotakiwa kutumia kizungu Kuna chochote anaambulia? Kwahiyo anaenda nje na kurudi nchini kama alivyoondoka.
Vipi ulishaanza kupata hamu ya wanaume? Maana ulisema huna hamu nao
 
Foleni ya baruti hadi kimara ni tatizo kwa wananchi wenyewe ulaji wa nyama na chips mayai hadi wanashindwa kupanda daraja la kimara hivyo kusababisha watu wengi wanaoenda mbezi kushuka kituo cha korogwe.SURUHISHO ni daradara na mwendo kasi zote ziende mbezi
 
Najiuliza, exposure wanayopata viongozi wetu mbali na elimu zao, haviwasaidii kufanya maamuzi sahihi?

Sidhani kama zinawasaidia ndio maana wanashughulikia reactively matokeo ya chanzo, na sio chanzo chenyewe.

Nikupe mfano : msikiliza Lowasa 1:20 - 3:23 akitumia elimu na exposure yake kutoa suluhisho la foleni ya magari Dar:
 
Daraja linajengwa sehemu ambayo pande mbili hazina mawasiliano kutokana na jiografia ya eneo hasa mito au bahari, kwa hiyo ubungo pale ile ni interchange, sio daraja (Bridge)
Nimefurahi umeliita daraja. Maana tumekuwa tukidanganywa kuwa eti hiyo ni flyover wakati ni DARAJA.

Narudia tena pale Ubungo pana DARAJA. Ndiyo maana foleni haitokwisha
 
Nyumbu ni nyumbu tu, hivi kabla ya Ubungo interchange hakukuwa na foleni Mlimani city na Mwenge? Kwa akili za Ufipa tatizo la foleni Ubungo bado lipo? Mawazo yenu yanaonyesha jinsi mlivyo watupu.
Nyumbu ni wale wanaoamini madaraja ndio suluhisho la foleni katika Jiji la Dar.
 
Hilo ndio swali langu kwani ninachokiona ni kupunguza kwa foleni katika eneo la mataa pale Ubungo ila mita chache kutoka hapo unakuta na foleni.

Kwa mfano, ukitoka Ubungo Interchange mida ya jioni hasa kuanzia saa moja kasoro usiku mpaka saa mbili, ukifika maeneo ya Mlimani City basi ni mwendo wa foleni mpaka Mwenge..Na hapo bado foleni ya kuelekea unakoenda kutoka Mwenge mfano kwenda Bunju.

Swali la msingi ni je, madaraja haya pekee ndio yataweza kumaliza hili tatizo?

Au tujiulize, kipi kinapaswa kuanza kati ya kujenga madaraja ya mabilioni na kupanua barabara zikiwemo highway na barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji?

Mfano, billion zaidi ya 200 zinazojenga daraja linalopita baharini zingetumika kuboresha/kujenga/ kupanua barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya jiji zisingekuwa na msaada zaidi katika kupunguza tatizo la foleni katika jiji hili?

Je, umefika wakati tuweke restrictions za magari binafsi kuingia katika ya Jiji kwa kuweka tozo maalumu za kuingia katikati ya Jiji?

Na bila kuboresha public transport, itakuwa sahihi kuweka restrictions kwa magari binafsi kuingia katika ya Jiji?

Dar inabidi wafanye planning upya ya miundombinu ya barabara kwa ajili ya kutumika miaka 100 ijayo,hivyo vi interchange kupoteza fedha tu.
 
Kamanda unaonaje ukianza kuwashupalia viongozi wa chama chetu kikuu cha upingaji wanunue angalau kiwanja ili tuanze ujenzi wa ofisi ya makao makuu? Tumekuwa tukipata ruzuku ya mamilioni kila mwezi lakini bado tunapanga kale kajumba ka ufipa, hatuna hata kiwanja. Jitahidi kamanda ili tuondokane na hii aibu ya upangaji, tena vichochoroni!
 
Zinakutosha kweli, hivi Ubungo interchange unataka ipunguze foleni Mwenge kuelekea Bunju au Dar hauijui vizuri?
Kazi yake ni kuanzisha mijadala kila lisaa, sio lazima iwe na maana yoyote hilo ni swala jingine kabisa, hapo kashatimiza wajibu wake
 
Foleni za huu mji ni tatizo kuliko global warming!
Kwa hivi ulivyoandika ndio umetoa point ya maana? Foleni ya Dar ni tatizo kubwa kuliko global warming? Are you serious? Au ndio kukurupuka kwenyewe, tuwekee data basi tujiridhishe.
 
Nilikwisha mwambia Mshua siku moja kuwa hizi foleni za Dar are there to stay!

Hata lijengwe daraja aina gani as long as magari ni mengi kuliko barabara foleni itabakia kuwapo tu.
Foleni lazima ziwepo tu popote pale. Hata majiji makubwa popote pale hapa duniani foleni zipo haziwezi kwisha bali zinapunguzwa tu. ukitaka kusiwe na foleni kajenge barabara kijijini kwenu lakini hapa mjini lazima kuwe na foleni hilo lazima ulielewe. Makali ya foleni huwa yanapunguzwa tu.
 
Back
Top Bottom