Mkuu sidhani kama hili ni suala linalohitaji mtaalamu au utaalamu, la hasha tunahitaji kuwa na mipango bora na endelevu tu...
Jambo la miaka 10, 20 au 30 ijayo linapaswa kupangwa leo, we need to be more proactive than reactive...
Mathalani, chukulia mfano namna muingiliano wa barabara kuu na barabara za pembeni ulivyojengwa Mbezi Mwisho...
Kwa nchi za wenzetu huwezi ukapata barabara iendayo mikoani/interstates zile zinakuwa na muingiliano na barabara za ndani ya mji...
Pale Mbezi Mwisho, sijui Temboni, Kwa Msuguri etc, kulipaswa kusiwe kabisa na ama T-junctions au Cross-junctions maana hizi ndio zilizozalisha foleni kila tunapojua sasa kuwa pana foleni...
Sasa sisi barabara ya mkoani kwenda Moro hata mbuzi, bata, ng'ombe wanaweza jikatizia tu