Ubungo interchange, imepunguza foleni au imepunguza msongamona kwenye eneo la daraja yaani katika mataa ya Ubungo?

Ubungo interchange, imepunguza foleni au imepunguza msongamona kwenye eneo la daraja yaani katika mataa ya Ubungo?

Watu washajipigia bajeti ya hilo daraja zamani, Alafu wanatuaminisha ni flyover. So imeisha hiyo.
 
Hilo ndio swali langu kwani ninachokiona ni kupunguza kwa foleni katika eneo la mataa pale Ubungo ila mita chache kutoka hapo unakuta na foleni.

Kwa mfano, ukitoka Ubungo Interchange mida ya jioni hasa kuanzia saa moja kasoro usiku mpaka saa mbili, ukifika maeneo ya Mlimani City basi ni mwendo wa foleni mpaka Mwenge. Na hapo bado foleni ya kuelekea unakoenda kutoka Mwenge mfano kwenda Bunju.

Swali la msingi ni je, madaraja haya pekee ndio yataweza kumaliza hili tatizo?

Au tujiulize, kipi kinapaswa kuanza kati ya kujenga madaraja ya mabilioni na kupanua barabara zikiwemo highway na barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji?

Mfano, billion zaidi ya 200 zinazojenga daraja linalopita baharini zingetumika kuboresha/kujenga/ kupanua barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya jiji zisingekuwa na msaada zaidi katika kupunguza tatizo la foleni katika jiji hili?

Je, umefika wakati tuweke restrictions za magari binafsi kuingia katika ya Jiji kwa kuweka tozo maalumu za kuingia katikati ya Jiji?

Na bila kuboresha public transport, itakuwa sahihi kuweka restrictions kwa magari binafsi kuingia katika ya Jiji?
Kama huna ruti za Posta na kariakoo na kutokea Ally Hassan Mwinyi road huwezi elewa tabu ya Barabara hiyo hasa maeneo makutano ya Kinondoni road Kenyatta drive na Ally Hassan Mwinyi .Kingine tambua tu kuwa Washikilia uchumi wa hii nchi Barabara yao kui Ally Hassan Mwinyi Hivyo itakuwa msaada kuharakisha maendeleo ya Nchi Maana new salenda bridge ni muhimu Sana maana huwa wanakwama mpaka masaa mawili kufika Posta.
 
Asante sana ni kuwa anachosema ni kweli hata barabara ya morogoro ukivuka tanesco ni foleni hadi kimara korogwe na sio hapo tuu hata ukitoka tazara ya buguruni ukija mandela road kuanzia buguruni kuitafuta extenal ni mziki au ukimaliza flyover ya ubongo unaenda bugùruni ukifika external kuitafuta tabata nayo ni shida.
 
Hilo ndio swali langu kwani ninachokiona ni kupunguza kwa foleni katika eneo la mataa pale Ubungo ila mita chache kutoka hapo unakuta na foleni.

Kwa mfano, ukitoka Ubungo Interchange mida ya jioni hasa kuanzia saa moja kasoro usiku mpaka saa mbili, ukifika maeneo ya Mlimani City basi ni mwendo wa foleni mpaka Mwenge. Na hapo bado foleni ya kuelekea unakoenda kutoka Mwenge mfano kwenda Bunju.

Swali la msingi ni je, madaraja haya pekee ndio yataweza kumaliza hili tatizo?

Au tujiulize, kipi kinapaswa kuanza kati ya kujenga madaraja ya mabilioni na kupanua barabara zikiwemo highway na barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji?

Mfano, billion zaidi ya 200 zinazojenga daraja linalopita baharini zingetumika kuboresha/kujenga/ kupanua barabara zingine zinazounganisha maeneo mbalimbali ya jiji zisingekuwa na msaada zaidi katika kupunguza tatizo la foleni katika jiji hili?

Je, umefika wakati tuweke restrictions za magari binafsi kuingia katika ya Jiji kwa kuweka tozo maalumu za kuingia katikati ya Jiji?

Na bila kuboresha public transport, itakuwa sahihi kuweka restrictions kwa magari binafsi kuingia katika ya Jiji?
Interchange inapaswa kwenda sambamba na upanuzi wa barabara angalau kila upande kuwe na njia 4.Bila hivyo itakua ni kupunguza msongamano pale kwenye interchange lkn kilometa moja au mbili kutoka pale follen inaanza km kawaida.
 
Namna ya kupunguza foleni dar ni kudiscourage matumizi ya magari binafsi

Serikali ianzishe kitu kinaitwa Congestion fee.

Hii itakuwa ni gharama atakayolipa mtumiaji wa wa gari binafsi dogo lenye namba ya usajiri T ya njano gari lisilo na body.

Let say gari liwe linalipa laki moja kwa mwaka. fedha hizo zitumike kutatua changamoto za barabara mijini.

Au kuwe na Scanner kila gari binafsi linapoingia mjini basi lidaiwe Tsh. 500
 
Kamanda unaonaje ukianza kuwashupalia viongozi wa chama chetu kikuu cha upingaji wanunue angalau kiwanja ili tuanze ujenzi wa ofisi ya makao makuu? Tumekuwa tukipata ruzuku ya mamilioni kila mwezi lakini bado tunapanga kale kajumba ka ufipa, hatuna hata kiwanja. Jitahidi kamanda ili tuondokane na hii aibu ya upangaji, tena vichochoroni!
Na nyie bila kutukamua wananchi kupitia mkono wa serikali hata kupanga mungeshindwa,nyie ni kupe.
 
Haikuwa sawa yaani kwenda mjini hakuna foleni halafu ulazimike ukae kwenye file kwa vile kwenda mwenge au kimara kuna foleni.
 
Foleni lazima ziwepo tu popote pale. Hata majiji makubwa popote pale hapa duniani foleni zipo haziwezi kwisha bali zinapunguzwa tu. ukitaka kusiwe na foleni kajenge barabara kijijini kwenu lakini hapa mjini lazima kuwe na foleni hilo lazima ulielewe. Makali ya foleni huwa yanapunguzwa tu.
Kuna aliyesema foleni inakwisha!?
 
Back
Top Bottom