Ubungo interchange, imepunguza foleni au imepunguza msongamona kwenye eneo la daraja yaani katika mataa ya Ubungo?

Watu washajipigia bajeti ya hilo daraja zamani, Alafu wanatuaminisha ni flyover. So imeisha hiyo.
 
Kama huna ruti za Posta na kariakoo na kutokea Ally Hassan Mwinyi road huwezi elewa tabu ya Barabara hiyo hasa maeneo makutano ya Kinondoni road Kenyatta drive na Ally Hassan Mwinyi .Kingine tambua tu kuwa Washikilia uchumi wa hii nchi Barabara yao kui Ally Hassan Mwinyi Hivyo itakuwa msaada kuharakisha maendeleo ya Nchi Maana new salenda bridge ni muhimu Sana maana huwa wanakwama mpaka masaa mawili kufika Posta.
 
Asante sana ni kuwa anachosema ni kweli hata barabara ya morogoro ukivuka tanesco ni foleni hadi kimara korogwe na sio hapo tuu hata ukitoka tazara ya buguruni ukija mandela road kuanzia buguruni kuitafuta extenal ni mziki au ukimaliza flyover ya ubongo unaenda bugùruni ukifika external kuitafuta tabata nayo ni shida.
 
Interchange inapaswa kwenda sambamba na upanuzi wa barabara angalau kila upande kuwe na njia 4.Bila hivyo itakua ni kupunguza msongamano pale kwenye interchange lkn kilometa moja au mbili kutoka pale follen inaanza km kawaida.
 
Namna ya kupunguza foleni dar ni kudiscourage matumizi ya magari binafsi

Serikali ianzishe kitu kinaitwa Congestion fee.

Hii itakuwa ni gharama atakayolipa mtumiaji wa wa gari binafsi dogo lenye namba ya usajiri T ya njano gari lisilo na body.

Let say gari liwe linalipa laki moja kwa mwaka. fedha hizo zitumike kutatua changamoto za barabara mijini.

Au kuwe na Scanner kila gari binafsi linapoingia mjini basi lidaiwe Tsh. 500
 
Na nyie bila kutukamua wananchi kupitia mkono wa serikali hata kupanga mungeshindwa,nyie ni kupe.
 
Haikuwa sawa yaani kwenda mjini hakuna foleni halafu ulazimike ukae kwenye file kwa vile kwenda mwenge au kimara kuna foleni.
 
Kuna aliyesema foleni inakwisha!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…