Ubungo mataa: Trafiki agongwa na pikipiki akikimbilia kusimamisha lori

Ubungo mataa: Trafiki agongwa na pikipiki akikimbilia kusimamisha lori

Mkuu ni wale boda wanaoendesha bila buti wala helmet halafu mwendo wa mbwa😀
Halafu ukute anapiga na singeli au amapiano🤣
images (1) (31).jpeg
 
Kumbuka huyo askari ana mke na watoto, hatujafika huko kuombeana mabaya, Yesu alitupenda kama jinsi tulivyo, Mungu angeangalia maovu Yetu hakika hamna ambaye Angepona, tuombeana badala ya kuchukiana
Ni kwelo Ila hao watu ukiingia kwenye 18 zao hawana huruma kabisa

Kuna siku nilikamatwa kiuonevu kabisa tena wakanitishia kunibadilishia kesi.

Sikuvuka taa ikiwa nyekundu Ila wakasema nimevuka taa ikiwa nyekundu, nilipatwa na hasira nisijue Cha kufanya
Hivyo kwa uchungu sana nasema simuonei huruma traffic yoyote yule
 
Kuna moja kamsimamisha jamaa,jamaa akamwambia nawahi ndege airport kama kuniandikia niandikie niache ,trafiki kagoma kaa mbele ya gari hataki kutoka ,jamaa akamwambia trafik toka nitakugonga ,trafiki akajibu ,gonga tuone ,jamaa akapita naye trafiki amekaa kwenye bonet ya cruiser jamaa akatembea naye Kama movie
 
Movie Gani hii?
 
Katika tukio la kustaajabisha na kushangaza hadi kuacha watu midomo wazi askari wa usalama barabarani aliekuwa kasimana mita chache kutoka mataa Ubungo kama unaelekea barabara ya Mandela (geti la kwanza la kushoto songas) askari ambae alikuwa kasimama hapo akiongea na dereva wa kirikuu alichokamata ameingia barabarani ghafla ili kuwahi kusimamisha lori lilokuwa linapita ndipo alipopata makasa huu pale alipokutana na pikipiki ilokuwa speed maarufu kama kishandu).

Tukio lenyewe ni kuwa huyu trafic alikuwa kashakamata kirikuu kikapaki pembeni kushoto.wakati wanadadiliana na dereva wa kirikuu mara likatoka lori ambalo limetokea mataa linaelekea buguruni,ndipo huyo trafic akakatuza mbele ya kirikuu ghafla kuwahi barabarani ili asimamishe lori kumbe kuna pikipiki ilikuwa speed inapita kushoto mwa hili lori ndik ikamvaa hugo askari hadi kumtupa pembeni na kumburuza.

Kwa ile hali niliyoona kama shughuda yuke askari kaumia sana tena sana maana alikuwa chini haongei wala hajigusi.

Nukuu ya mashuhuda:
Wacha afee wamezoea kula hela yetu hawa, msimguse mwacheni afe.mwisho:kwa ile kauli niliyosikia pale hata sikuangaika kutoa msaada wala kuhangaika kupiga piga.

My take; Polisi jirekebisheni kaeni vizuri na raia wameshawachoka mambo mnayowafanyia. Poleni sana .
Askari akiona lorry huwaa wanatokwa na udenda .pole yake
 
Ni kwelo Ila hao watu ukiingia kwenye 18 zao hawana huruma kabisa
Kuna siku nilikamatwa kiuonevu kabisa tena wakanitishia kunibadilishia kesi.
Sikuvuka taa ikiwa nyekundu Ila wakasema nimevuka taa ikiwa nyekundu, nilipatwa na hasira nisijue Cha kufanya
Hivyo kwa uchungu sana nasema simuonei huruma traffic yoyote yule
Hasira niliokuwa nayo jana nilienda lala mapema sana sababu ningeweza kufanya matukio ya ajabu! Traffic wana uonevu sana na ni vile wanajua hatuna cha kuwafanya yani akiwa road pale!

Yani salama yako uwe na namba ya mkubwa umpigie ili amtishe tishe 😂
 
Buku tano ya kiwi imemvunja miguu. By the way kishandu alisimama kweli?
Anasimamaje 😂 labda kama naye alianguka ila kama chombo iko mstari tunakamua zutu vizuri tu na unaipa kidonge namba 5 😂 chuma inapepea tu! Kwa lile jam hadi aje ainuke ijulikane alipitiwa na boda boda we ushaikamatia external unaitafta jeshini!
 
Back
Top Bottom