Ubungo mataa: Trafiki agongwa na pikipiki akikimbilia kusimamisha lori

Kumbuka huyo askari ana mke na watoto, hatujafika huko kuombeana mabaya, Yesu alitupenda kama jinsi tulivyo, Mungu angeangalia maovu Yetu hakika hamna ambaye Angepona, tuombeana badala ya kuchukiana
Ni kwelo Ila hao watu ukiingia kwenye 18 zao hawana huruma kabisa

Kuna siku nilikamatwa kiuonevu kabisa tena wakanitishia kunibadilishia kesi.

Sikuvuka taa ikiwa nyekundu Ila wakasema nimevuka taa ikiwa nyekundu, nilipatwa na hasira nisijue Cha kufanya
Hivyo kwa uchungu sana nasema simuonei huruma traffic yoyote yule
 
Kuna moja kamsimamisha jamaa,jamaa akamwambia nawahi ndege airport kama kuniandikia niandikie niache ,trafiki kagoma kaa mbele ya gari hataki kutoka ,jamaa akamwambia trafik toka nitakugonga ,trafiki akajibu ,gonga tuone ,jamaa akapita naye trafiki amekaa kwenye bonet ya cruiser jamaa akatembea naye Kama movie
 
Movie Gani hii?
 
Askari akiona lorry huwaa wanatokwa na udenda .pole yake
 
Hasira niliokuwa nayo jana nilienda lala mapema sana sababu ningeweza kufanya matukio ya ajabu! Traffic wana uonevu sana na ni vile wanajua hatuna cha kuwafanya yani akiwa road pale!

Yani salama yako uwe na namba ya mkubwa umpigie ili amtishe tishe 😂
 
Buku tano ya kiwi imemvunja miguu. By the way kishandu alisimama kweli?
Anasimamaje 😂 labda kama naye alianguka ila kama chombo iko mstari tunakamua zutu vizuri tu na unaipa kidonge namba 5 😂 chuma inapepea tu! Kwa lile jam hadi aje ainuke ijulikane alipitiwa na boda boda we ushaikamatia external unaitafta jeshini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…