Ubungo mataa: Trafiki agongwa na pikipiki akikimbilia kusimamisha lori

We mzee punguza hasira😂 utakuja fanya kitu mbaya 😂😂
Hawa nasikia huko sahv wamejaa mwendo wa bao tu,ila dawa yao watu wapaki magari

Ova
 
INABIDI POLICE WAWAPE MAFUNZO TRAFIC WAO NAMNA YA KUSIMAMISHA MAGARI

OVA
 
Traffic wameacha kazi ya kuangalia usalama barabarani na kujiingiza katika kupokea rushwa kutoka kwa magari ya mizigo na abiria. Sijawahi kusikia takukuru imemkamata traffic!
 
Kumbuka huyo askari ana mke na watoto, hatujafika huko kuombeana mabaya, Yesu alitupenda kama jinsi tulivyo, Mungu angeangalia maovu Yetu hakika hamna ambaye Angepona, tuombeana badala ya kuchukiana
Yeye anaowaonea hawana wake na watoto?
 
Pale wanakaaga mpaka mida ya saa mbili usiku kuelekea saa tatu tena wanajificha, ili daladala zikisimama tu pale kwenye power plant wanazikamata.
 

Ungepiga picha aisee.
 
Hawa watu ni shida sana, wanatakiwa kujirekebisha maana wameshaweka uadui kati yao na watu wanaomiliki vitu vya moto
Hakika. Wana kazi wanatakiwa kufanya kwa kweli
 
Naungana na kauli ya hao mashuhuda kwa kuwapa free lunch mchana wa leo.
 
hao jamaa wana roho mbaya sana, kuna mmoja alinikamata iringa akaniambia NAKUANDIKIA MAKOSA MAWILI kabla hata sinauliza ufafanuzi akaingia kwenye gari lake akajifungia kwamba hataki kutoa maelezo ya hayo makosa. Kweli badae nilivoangalia nikakuta makosa mawili.
 
jamaa aliwekewa barrier mikese,tajiri akapigiwa simu,watalii wakawahishwa airport na mtu mwingine ila jamaa alibawekwa ndani kwanza,ila kwenye kesi baadaye jamaa alikuja kushinda
Mwambie siku nyingine awe anajishusha, yaani awe myenyekevu, omba msamaha, eleza umuhimu wa hiyo safari, binadamu tumeumbwa na moyo wenye majuto.
Nitakupa kisa kimoja.
Nina rafiki yangu ana mtoto wa kiume mtumdu kidogo. Siku moja alimkosea, sikujua ilikuwa ni nini, lakini jamaa yangu alikuwa amekasirika sana. Alimtandika bakora mbili za nguvu makalioni, ajabu yule mtoto(5-6 years) hakulia, badala yake alimwomba msamaha baba yake kwa unyenyekevu mkubwa ule wa kitoto. Baba akamwacha huku akisonya na kuingia ndani.
Yule mtoto alitoka pale akazunguka nyuma ya nyumba, akakaa chini huku amejikunyata, kichwa katikati ya magoti akilia taratibu. Baba alipochungulia dirishani na kumuona katika hali ile, alitokwa machozi ya kiutu uzima. Alihuzunika!! Hasira zikamwisha.
 
Niliwasikia mahali wakielimisha waenda kwa miguu namna ya kuvuka barabara, kumbe zilikuwa ni chenga tu zile.......
 
usiridhi maadui wala marafiki, wewe ungetoa tu msaada uende zako, kama una gari unambeba,unmpeleka muhimbili na kumkabidhi, uhai ni bora kuliko kitu chochote, tenda wema uende zako na usisubiri malipo.

P{olisi hasa traffik wanaudhi sana, unakuta unawahi hospitali, wanakukamata, wanataka hela hawajali unakwenda wapi, lakini tumuachie Mungu, tuwapende mpaka washangae.
 
Kiduku na ndala anavaa kama zinataka kuanguka na pikipiki anakalia upande hanyooki kama wengine
Hii style ya ukaaji wa hawa boda boda huwa inanichekesha sana na ndala anavaa kama kaegesha tu🤣🤣🤣
 
Kuna tatizo lingine kubwa, Nathan Hili linamhusu Mheshimiwa mkuu wa Mkoa kwa Msaada, eneo LA gerezani, Kuna genge LA watu wanne na wanatembea na Bajaji na reflector Nyekundu!! Ila najua kuna taasisi imewatuma!! Eneo limevurugwa sana na biashara na hakuna parking!! Wameandaa maeneo kama sita (6) hapa Kariakoo Gerezani na kuchapisha vibao "taxii" parking na kukaa pembeni, Ukijikuta umeona ni kama parking ukikaribia kupark wanakuja na kukutisha na kukufungia gari na kudai Rushwa!! Jamani Tumefikaje hapa kuwaajiri hawa Majizi!? Ni rahisi kwenda pale na kuwakuta hawana hata tone LA aibu!! Mheshimiwa Makala (Mkuu wa mkoa) tuokoe na matapeli hawa wanatuharibia nchi!! Karibia na Shule ya Kisarawe maeneo hayo na wapo matapeli wanne!! Wanadai rushwa bila aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…