Ubungo waandamana ofisini kwa DC kudai Maji

Safi sana....sehem zote tukionesha hali kama hii viongozi watashika adabu ....shubamitt
 
Dah nisaidie nimetume boda hapo aniletee dumu hata 6 mkuu. Yani Leo sijaoga kabisa hata kutoka nimeshidwa. Napigia wa magari siwaoni
Me nipo ngerengere chief cjarudi huko
 
endeleeni kunuka vikwapa uko Dar , uku Mvuti maji tunaogeshea nguruwe
 
Sasa wameandamana wameyapata?

Tupunguze dharau. Yani watu wakae mwezi mzima bila maji, wakiandamana wewe waache hujui wamevumilia kiasi gani. Kama umeshiba usimcheke mwenye njaa.
 
Kwani kuandamana ndio kunaleta maji?
Mkuu kuandama ni moja ya njia za kuwasilisha kero kwa mtu ambaye mnaona anawajibu wa kutatua kero zenu. Kwa suala maji wengi tunajua Serikali ndiyo inatuletea Maji kupitia taasisi zake kama dawaso kwa watu wa DSM. Ni ngumu sana kwa mtu wa DSM kujitafutia Maji aidha achimbe kisima kwa wenye Uwezo. Au aite gari za Maji nao pia kwa wenye Uwezo. Kwa mazingira ya DSM hizo ndiyo njia pekee za kupata Maji kama Dawasco hawajasupply Maji, vyanzo Vya Maji viko mbali hawawezi kwenda na ndoo mto ruvu. Nawaonea huruma.
 
Siyo Mji Mzima sema Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Ila kule Kigamboni,Temeke hata Ilala Maji yapo Watu walijitengenezea Mfumo binafsi usiokuwa unategemea serikali kwa maana Watu walichimba visima na Wakiobahatika kupata Maji yasiyo ya Chumvi walisambaza Kama wafanyavyo Dawasa .Hivyo huwezi sikia kero ya Maji Ilala Temeke Wala Kigamboni na Kama ikitokea ni Mara chache Sana . Ebu fikiri Watu wa Mbagala walivyo Wengi vile lakini Wapo kimya au kule Gezaulole au kule Gongo la mboto. Kwa ufupi Manispaa ya Kinondoni na Ubungo ndizo hasa waathirika zaidi hivyo Ondoa neno Mji Mzima..Halafu kumbukeni Ubungo siyo Jiji la Dar es Salaam
 
Wamekosa kazi, unaandamana kuenda kwa DC ambae hatokupa maji, huo Ni utoto ungetumia mda huo kutafuta maji kwingine.
Hapo Kwa DC hatua chache ndy hapo hapo ofisi za DAWASA LUGURUNI zilipo.

Wanainchi wameamua kwenda Kwa DC baada ya kuona hakuna mtetezi.


Walishakwenda DAWASA ofisini na kuonana na engineers,pamoja na viongozi kadhaa bila mafanikio.

Kinachofanyika ni Bomba la kibamba Kwa Mangi (DAWASA)
Linauza maji kwenye magari ambayo huuzia wanainchi Kwa sh 20000 Kwa 1000 litres.

Ili biashara Yao ya maji ifanyike vzr ni lazima wanainchi wafungiwe maji wasiyapate .
Na watu wa magari pamoja na DAWASA kupiga pesa,

Hili Bomba hata hayati MAGUFULI RIP alilipigia sana kelele,
Na lilikoma Kwa kipindi chote yupo madarakani.

Kabla ya kucomment jambo lolote kwanza uwe na ufahamu wa kinachoendelea.
 
Sasa hizo mita nani husoma?

Au hizo mita hupitisha nini hadi namba zibadilike?

Wakala wa Vipimo atueleze
Wanakadiria halafu wanakwambiya ni deni la zamani bill ilichelewa kusomwa.
 
Kwani kuandamana ndio kunaleta maji?
Kelele nyingi humfanya hata muhalifu kuogopa na kukimbia.

Bila maandamano tanzania nzima ingejuwa kama wakazi wa LUGURUNI KIBAMBA hawapewi maji Kwa miezi mitatu Sasa?

Hizi kelele nilishazipiga sana humu,
Lakini hazikupata ufumbuzi.

Go wanainchi go go go.
 
Ukitaka kujuwa DAWASA walikuwa wanafanya makusudi ,

Leo hii baada ya wanainchi kwenda Kwa mkuu wa wilaya,
Wameamua kuyafungulia maji usiku huu LUGURUNI KIBAMBA.,,

Kama maji walikuwa hawana haya waliyofungulia wametoa wapi?

Kweli kelele zinasidia sn.

RIP MAGUFULI.

Watanzania tumezoea kusukumwa ,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…